Baba Chanja na mama Chanja!!

CHAI CHUNGU

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2012
Posts
7,113
Reaction score
943
Siku moja baada ya kupata chakula cha mchana "baba Chanja na mama Chanja waliamua kubadilishana mawazo kama ifuatavyo.
Baba Chanja:hivi mama Chanja mimi nikifa leo au kesho jee utaolewa na mwanaume mwingine?
Mama Chanja:ndio mume wangu ntaolewa.
Baba Chanja:na huyo mume mtalala nae ktk kitanda hikihiki tunachokilalia?
Mama Chanja:Ndio mume wangu.
Baba Chanja:Na nguo zangu utampa pia?
Mama Chanja:Ndio mume wangu ntampa,na tena lile shati jeupe litampendeza sana.
Baba Chanja:Mhh,kwahiyo ata vile viatu vyangu nilivyovinunua juzi juzi mjini pia utampa?
Mama Chanja:hapana hivyo sitampa.
Baba Chanja:Kwanini vitu vyote umpe isipokua viatu tuu???
Mama Chanja:Miguu yenu haiendani!!!!!
Teh teh teh.
 
Wakina mama chanja siyo mchezo!
Tukaeni nao kwa akili sana!
 
Duh si bora tu baba chanja amuachie jamaa arithi acje kupewa sumu jamaa akarithi shati jeupe
 
Yaani mtu anajulikana aiseee roho inauma niaje sitalala kabisa
 
Mama chanja kilaza baba chanja akili mingi kashakamata mwizi wa mali zake...safii
 
Hapo baba Chanja inabidi ale mpaka kile kichanja kabisaa jamaa hata akirithi potelea mbali
 
kulalalaleki huyo wife anaweza akajuta kwa majibu yake ya kimbwiga..!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…