Baba apewe heshima sawa na anayopewa mama

ichumu lya

JF-Expert Member
Aug 11, 2016
2,605
2,729
Umetoka shule umekuja nyumbani kwa likizo unamkuta baba yako hayupo unamuuliza mama yako kuhusu baba yako anakuambia baba yako yupo kazini.

Unakaa hapo nyumbani kwenu mwezi mzima Muda wote upo na mama yako Mara likizo imeisha baba yako anakukuta uko chumbani kwako unapanga mabegi anakupatia shilingi Laki nane ya ada Unamuomba ela ya matumizi anakupatia shilingi 80,000 unamwambia haitoshi anakuambia maisha ni magumu unatoka hapo umenuna unakwenda sebuleni Mama yako anakuuliza kwa nini umenuna? Unamwambia Baba kanipa ela haitoshi mama anatoa shilingi 30,000 anakupatia unafurahi unaingia facebook unaandika

"NANI KAMA MAMA? MAMA NI MUNGU WA PILI WA DUNIANI"
Unajua kama baba yako baada ya kukulipia ada anakwenda kazini kwa miguu kwa sababu maisha ni magumu? Unajua kama hiyo shilingi 30,000 aliyokupatia Mama yako amepewa na Baba yako? Unajua kama umesoma kutoka Chekechea mpaka hapo ulipo kwa jasho la Baba yako.

ACHENI UBAGUZI WA WAZAZI HUU UBAGUZI WA WAZAZI SIJUI UTAISHA LINI?
Kwa ufupi hii ndio siri ya Wababa kufa haraka.
FB_IMG_1612633051795.jpg
 
Umenigusa sana ndugu yangu, ninaumia sana nikiona jamii nzima inavyomtenga BABA,
Cha ajabu kubwa hata mtoto wa kiume , kijana bila aibu anathubutu kusema hakuna kama mama kweli ? ? na wewe ni baba wa kesho tu ,

Hiyo kesho mke wako ulie muoa kutoka kwao kwa jasho lako la mahari, ukaja ukampa mbegu yako
mkapata watoto ukawasimamia maisha yote pamoja na kuwasomesha leo hii
Wanakuteta , wanakutenga, kubagua, NASEMA HIYO NI LAANA NA MALIPO YAKE NI HAPA HAPA DUNIANI.
 
Kwa hii picha kweli acheni baba aheshimiwe jamani 😂😂😂!!!
Hio mashine ina zaidi ya Tani moja 😂😂
 
Umenigusa sana ndugu yangu, ninaumia sana nikiona jamii nzima inavyomtenga BABA,
Cha ajabu kubwa hata mtoto wa kiume , kijana bila aibu anathubutu kusema hakuna kama mama kweli ? ? na wewe ni baba wa kesho tu ,

Hiyo kesho mke wako ulie muoa kutoka kwao kwa jasho lako la mahari, ukaja ukampa mbegu yako
mkapata watoto ukawasimamia maisha yote pamoja na kuwasomesha leo hii
Wanakuteta , wanakutenga, kubagua, NASEMA HIYO NI LAANA NA MALIPO YAKE NI HAPA HAPA DUNIANI.
Daaaaahh uzi huu unachonyota rohoni. Nimeumia sana
 
Yaani kuna mpasuko mkubwa sana baina ya mama na baba m naonakwa sabab mama kakutunza miezi tisa ila jamii imemezeshwa mama n kili kitu
 
Mtoto anaanza kuona thamani ya baba baada ya yeye kuanza kujitegemea na familia yake inamuangalia kwa kila jambo.
 
yaaan kuna mpasuko mkubwa sana baina ya mama na baba m naonakwa sabab mama kakutunza miezi tisa ila jamii imemezeshwa mama n kili kitu
Bila kuolewa Bila mbegu + huduma ANGETUNZA NINI ? ?

Ukiona mtu anabagua wazazi hakika huyo anamapungufu aidha ni sawa na kilema au HAJITAMBUI kwani hakupata malezi stahili huyo ni wa kumpa POLE TENA POLE SANA MPUUZE TU

BABA NI BABA TU hata kama ana madhaifu, je ungekuta baba yako ni kiwete ungemdharau ?

Mijadala hii inaonyesha dhahili kwamba jamii yetu ni kizazi chenye malezi mabovu, dhaifu, wagonjwa wa kisaikolojia wote.

 
Back
Top Bottom