Baba amwua mwanaye kwa kumkanyaga kifuani

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
274
Katika hali isiyo ya kawaida, Hassan Omary, mkazi wa Kata ya Kiungi Madukani katika wilaya ya Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro, amemwua mwanaye wake Joseph Hassan (1.3) kwa kumkanyaga kifuani kutokana na hasira baada ya mkewe kukimbia alipotaka kumchinja kwa panga.

Tukio hilo la kusikitisha limetokea usiku wa kuamkia jana mkoani humo wakati baba huyo aliporejea kutoka kunywa pombe na alipofika katika nyumba wanamoishi, baada ya kuingia ndani, alianza kumpiga mkewe, Anna Hassan, na ndipo alipoamua kuchukua panga kwa nia ya kumchinja. Kuona hivyo, mkewe aliamua kukimbia ili kuokoa maisha yake, lakini mumewe alianza kumfuata lakini alishindwa kumkamata.

Purukshani hizo zilisababisha mtoto wao mchanga kuanza kupiga kelele huku akimfuata baba yake ambaye alimbeba kisha kuingia naye ndani na kumlaza chini na kuanza kumkanyaga kifuani, hali iliyosababisha mtoto huyo kulia kwa uchungu huku akitokwa na damu mdomoni. Kutokana na kelele hizo, mama yake ambaye alikuwa amejificha nyumba ya jirani alirejea na kumkuta mumewe akimkanyaga mtoto huyo ndipo alipopiga mayowe ya kuomba msaada kwa majirani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Lucas Ng'obhoko, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mtuhumiwa huyo anashikiliwa na polisi. Ameongeza kuwa mtoto huyo alifia njiani wakati akikimbizwa hospitalini kwa ajili ya matibabu.

from: Baba amwua mwanaye kwa kumkanyaga kifuani -
 
Goosh what a beast!!!! Why kill an innocent child? Hasira hasara, I hope justice takes its course....Mungu amfariji huyo mama Anna. I feel for her
 
Jamani very sad. Mtoto amekosa nini? Jamani wanaume na hizi pombe punguzeni. Ona sasa imebakia majuto. Lo pole sana dada Anna. Mungu huyo huyo aliyekupa huyo mtoto atakupatia mwingine.
 
Lately, Kilimanjaro has become a home for bizarre incidents.
What is going on peoples mind????
 
Lately, Kilimanjaro has become a home for bizarre incidents.
What is going on peoples mind????

jamani, kilimanjaro itazamwe kwa darubini. Ni kweli kuwa maovu na waovu wako kila mahali ila kwa mwaka huu kili imenmwanga damu nyingi tena ya watoto. Tumurudie mola.
 
Back
Top Bottom