kalamata
Senior Member
- Apr 16, 2011
- 144
- 29
Hili lipo wazi kabisa. Inajulikana sasa kuwa baadhi ya Wazanzibari wanaitaka Zanzibar yao kwa hali na mali. Wako wahafidhina toka kada mbalimbali huko visiwani walio wazi na walio ufichoni ambao, katika siasa, uchumi, n.k. wakitaka kujitenga na Tanganyika. Hili linathibitishwa na kauli za kina Jussa na wengine, na hii ni baada ya kuona kuwa Zanzibar ina rasilimali kadhaa ikiwa ni mafuta na gesi.
Baadhi ya Wazanzibari walioko visiwani hawasiti kuonyesha hisia zao juu ya nia hii ya kujitenga. Wazanzibari walioko Tanganyika hawaonyeshi dalili yoyote ya wazi ya kupingana na ndugu zao wa visiwani, kama kwa njia ya makongamano na hata taarifa rasmi kwa umma. Hili suala wanaachiwa tu viongozi kulisemea wakati walengwa wakuu ni wananchi wa kawaida. Baadhi ya Wazanzibari walio Bara wanafaidika sana na utulivu, amani na uelewa wa watu wa Bara. Watanganyika walioko visiwani hawana amani kama hawa wazanzibari wa Bara.
Enyi wazanzibari mlioko Bara toeni tamko kulaani manyanyaso wayapatayo wa Bara huko visiwani, la tunajua lenu moja. Mnachuma Bara kama waasia wanavyochuma Tanzania. Toeni tamko sasa.
@Raia Fulani
Ndugu yangu hebu kuwa mwadilifu,sasa unasema sisi Wa-zanzibar tuishio Bara tutoe tamko,mimi kwa kweli sikuelewi,tutoe tamko gani?sisi wazee wetu wapo hapa tangu enzi hizo,tumezaliwa huku bara,tumesoma huku bara na hatuja wahi kusikia wabara wakitubagua kwa chochote kikubwa ni kutuita wapemba,na hicho ni kitu cha kawaida wala hakituudhi,hio ni kama LAKAB yetu,cha msingi ni kua hao ndugu zetu huko nyumbani znz wasilete choko choko na kutugombanisha wenyewe kwa wenyewe.sisi wote ni wamoja,kama ni makosa basi walioyafanya ni hao wanaoitwa waasisi,vp tuhukumiwe sisi kwa makosa walioyafanya wao?