Baadhi ya watu wanajiuliza kwanini ''bwana yule'' hapati tena siri za Ikulu?

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
12,948
2,000
Nimeona sehemu nyingi baadhi ya watu wakijadili kuhusu ''bwana yule'' huku wengine wakimbeza lakini wengine wakiuliza kimetokea nini kwa sasa ''bwana yule'' hapati tena siri za Ikulu.

Kwa wasiojua vizuri wameenda mbali zaidi na kudai eti kwa sasa siri za Ikulu zimethibitiwa na uongozi mpya!

Napenda niwasaidie kwa kuwaambia kuwa hakuna siri za Ikulu zilizothibitiwa ila wale waliokuwa wanatoa siri za Ikulu na kuzipeleka kwa ''bwana yule'' kwa sasa ndio hawa ambao wako madarakani. Kwa maana nyingine, kwa sasa ndio walioshika Ikulu/utawala moja kwa moja. Yaani sio tena watoa ushauri bali kwa sasa ni wabunifu na wasimamia utekelezaji.

Biashara yao na ''bwana yule'' ya kumpa siri za Ikulu iliisha siku ambayo Rais Samia aliapishwa kuwa Rais wa Tanzania!

Haishangazi kuona kwa sasa ''bwana yule'' anawashambulia sana baadhi ya wale waliokuwa wanampa siri za Ikulu baada ya kugundua hawataki tena mahusiano naye. Yaani kwa sasa wamemalizana naye!

Nasikia kwa sasa wale wale waliokuwa wanampatia siri za Ikulu wana mpango wa ''kumnyamazisha'' ili huko mbeleni asije akatumia umaarufu waliomuwezesha wao wenyewe kuichafua serikali yao. Kibaya zaidi, wanamjua vizuri kwa maana kuwa, wanazijua nguvu zake na udhaifu wake(strengh and weakness) kwa sababu ndio walimuwezesha kupata umaarufu kwenye mitandao ya kijamii. Hata kupata kitambulisho cha ''blue tick'' ilikuwa ni jitihada za baadhi ya wale waliokuwa wanampatia siri za Ikulu.

Baada ya kukosa ushirikiano kwa sasa ''bwana yule'' anafanya jitihada za kuwa karibu na wenyeCHADEMA ili apate uungwaji mkono kwenye mitandao! Kwa wanaofahamu historia ya ''bwana yule'' watajua kuwa huko nyuma hakuwahi kuipenda/kuishabikia CHADEMA hasa hakumpenda Mwenyekiti Mbowe na aliwahi kumshambulia sana akidai mwizi wa pesa za chama.

Huko mwanzo, ''bwana yule'' alikuwa ni mwanaCCM lakini baadaye akawa ''mwanaACT-Wazalendo'' kabla ya ujio wa Maalim Seif na kundi lake! Wakongwe wa siasa nchini wanajua kuwa ACT-Wazalendo ni ''stepping stone'' kwa wanaCCM! Kwa maana nyingine, ACT-Wazalendo ni kama fimbo ya kuchapiana wanaCCM kwa wanaCCM!

Hasira za ''kutoswa'' zinamfanya aanze ''revenge'' kwa waliomtosa kwa kutumia ''platform'' za CHADEMA.

''bwana yule'' anajua bila kupata sapoti ya wanaCHADEMA hawezi kuendelea kuwa ''relevency'' kisiasa katika dunia ya mitandao kwa sababu CHADEMA ni kundi pekee la kisiasa nchini ambalo hajapoteza uungwaji mkono.

Hoja iliyopo kwa sasa ni kujua kama ''kinyago'' walichokichonga walioko madarakani kwa sasa kitawatisha au watakiangamiza kabla hakijaanza kuleta madhara!
 

Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
17,977
2,000
Mkuu, Magu hayupo tena.

Kama mrija wako umekatwa, jifunze kula kwa jasho kama wengine.

Mimi mwenyewe namfuatilia huyo unayemsema. Haelekei kabisa kuwa kundi la watu walioshika madaraka sasa hivi.

Mfano wewe sasa hivi kwa maandiko yako, unaonekana dhahiri umetupwa nje.
 

4 7mbatizaji

JF-Expert Member
Dec 8, 2019
2,444
2,000
Huwezi kuja na theory moja tu bila kufikilia theory nyingine unapozungumzia Jambo fulani, au unapotaka tatua Jambo fulani.

Wenda pia bwana yule kaombwa ushirikiano baada ya kuona hawezekaniki, kutokana na uwezo wake mkubwa, chini ya jua Kuna Mambo mengi, BWANA yule mtandao wake Sio wa dunia hii,ila pia kipaji na uwezo wake binafsi ukiangalia sio wa kawaida
 

mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
23,326
2,000
Huwezi kuja na theory moja tu bila kufikilia theory nyingine unapozungumzia Jambo flan, au unapotaka tatua Jambo flan
Wenda pia bwana yule kaombwa ushirikiano baada ya kuona hawezekaniki, kutokana na uwezo wake mkubwa, chin ya jua Kuna Mambo mengi, BWANA yule mtandao wake Sio wa dunia hii,ila pia kipaji na uwezo wake binafsi ukiangalia sio wa kawaida
Aaaah we.

Hawezekaniki!! .
Kwa taarifa yenu,huyo mtu anafahamika mpaka anapoenda kunya.
Alikuwa anatumika kujaribu kumsahihisha bwana mzee,hasa baada ya kuonekana dingi si tu hashauriki, bali hapendi kuendeshwa.
 

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
12,948
2,000
Mkuu, Magu hayupo tena.

Kama mrija wako umekatwa, jifunze kula kwa jasho kama wengine..
Mkuu;
Kunijadili mimi hakuweza kuiondoa hoja yangu bali utakachokipata ni furaha ombwe ya moyo wako!

Kutupwa kwangu au la kusikusumbue bali niachie mimi!

Jikite kwenye hoja na kama unadhani hakuna hoja basi unaweza kupuuuza na kuondoka!

Unasema huyo ninayemsema haelekei kuwa katika kundi la walioko madarakani! Huoni kuwa unachosema ndicho chimbuko la kinachoendelea kwa sasa ambapo kutoswa ndiko kunamfanya aanze kuwashambulia!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom