Baadhi ya Watanzania na Matumizi Potofu ya Dhana Jumlishi (Generalization)

Umkonto

JF-Expert Member
Dec 27, 2018
2,121
3,641
Kwa tafsiri isiyo rasmi. Dhana jumlishi (Generalization) ni kitendo cha kuhusisha watu au vitu vyote na jambo au hali fulani.

Dhana hii jumlishi (generalization) imekuwa ikitumiwa kimakosa na baadhi ya Watanzania, wanapokuwa wanaelezea jambo fulani ambalo limetokea ngazi ya jamii, taifa au kimataifa. Kwa mfano, Mtanzania mmoja akivurunda, unaweza kumsikia mtu akisema: "Watanzania ni wajinga sana". Je, ni kweli hakuna Mtanzania mwenye uelewa?

Pia, jambo fulani linatokea Tanzania kama vile mbunge kuruka sarakasi bungeni, lakini mtu anasema: "Wanasiasa wa Afrika wana shida". Hapa mtu huyo anakuwa anajumlisha Waafrika wote. Lakini tujiulize, je, ni kweli Wanasiasa wote wa Afrika wana shida? Hakuna wenye unafuu?

Au Wamachinga wakipanga bidhaa hadi barabarani baadhi ya maeneo hapa Tanzania, unakuta mtu fulani anasema: "Wafrika ni wajinga". Je, ni kweli, nchi zote za Afrika wamachinga hawana utaratibu wa kufanya biashara mpaka kupanga bidhaa barabarani? Hapo Botswana tu wamepiga hatua, mambo yao yameratibiwa vizuri tu!

Zipo sababu dhahania ambazo tunaweza kusema zinasababisha baadhi ya Watanzania kujumlisha mambo. Mojawapo ni kukosa "exposure". Hapa namaanisha baadhi ya Watanzania hawafahamu maisha ya nje ya jamii husika au Tanzania hata kwa kufuatilia tu mitandaoni!, ndio maana wanahisi kinachotokea Tanzania ndicho kinatokea Afrika nzima, au kinachotokea kwenye jamii aliyomo ndicho kinatokea Tanzania nzima. Sikatai kwamba, kuna vitu tunafanana Afrika lakini si kila kinachotokea Tanzania ndio kinatokea Afrika nzima.

Ieleweke, bara la Afrika ni kubwa, na pia kuna nchi zimepiga hatua katika nyanja za kijamii, kisiasa, na kiuchumi kuliko Tanzania. Kwa mfano, kidemokrasia, Ghana wamepiga hatua zaidi kuliko Tanzania, hivyo si sahihi kusema Afrika hakuna Demokrasia kwa sababu tu magumashi yametokea Tanzania.

Maneno gani ya kutumia ili kuepuka dhana Jumlishi (Generalization)?

Ili kuepuka dhana jumlishi, tumia maneno kama vile "baadhi ya" au "wengine". Kwa mfano sema, "baadhi ya Watanzania wanaamini katika ushirikina" kuliko kusema: "Watanzania ni washirikina" wakati kuna Watanzania siyo washirikina. Au sema: 'Watanzania wengine ni wababaishaji", na siyo kusema: "Watanzania ni wababaishaji"

Mwisho, kama jambo linatokea kwenye jamii yako au nchi yako, hebu jikite huko huko kuliko kujumjulisha mambo.


Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Samaki mmoja akioza wote wameoza.

Kwa wanasiasa wa afrika kupata mwadilifu sahau.

#MaendeleoHayanaChama
 
FB_IMG_1653208980724.jpg
 
Samaki mmoja akioza wote wameoza.

Kwa wanasiasa wa afrika kupata mwadilifu sahau.

#MaendeleoHayanaChama
Je, ni sahihi msomi Mtanzania mmoja akizingua na kusema "Watanzania huwa tunaenda shule kusomea ujinga?"

Kwani hakuna Wasomi wa Kitanzania wenye matokeo chanya kwenye jamii?

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Pamoja na kwamba mtamkaji (anaye-generalise) hana uhakika wa 100%, ila mambo yanayoihusu Tanzania na Afrika yanashabihiana mno..mulika muktadha wa mchezo wa soka kama mfano..angalia figisu,waamuzi, viwanja duni, nenda Benin, malawi, gambia, tz, gabon huko botswana kwako ni hadith ileile
 
"Wanawake wa miaka hii wapo kimaslahi zaidi" hii statement nayo inahitaji exposure gani kuafikiana nayo..ni fair generalisation.
 
Kuna sehemu ya kutumia neno "baadhi" ila kuna sehemu inabidi utumie neno "wengi". Haya jaza sehemu zilizoachwa wazi
1. Bodaboda .......(wengi/baadhi).....ni....
2. Mafundi ujenzi........ni........
 
Back
Top Bottom