Baadhi ya wanaume wa Dar tatizo ni nini?

Baadhi ya wanaume wa Dar tatizo ni nini?

We unesemwa hadharani na wewe umekuja kuwasema mafichoni hamna tofauti wote wewe na hao ni wanafki na wambea
Asante. Lakini tambua hapa ni elimu.

Wadadisi wanasema bora ukatoe ripoti polisi kuliko kuyafanya yako.

Kwa maana hiyo kwa mtizamo wako ukienda polisi wewe ni mbea na mnafiki.

Kwangu mitandao ya jamii ni zaidi ya polisi.

Wewe ni mwanaume wa ***. Mbona hasira sana.
 
Humu JF ili ujulikane upesi au utambulike kuwa na Wewe leo ume log in ni lazima ama umfuate fuate GENTAMYCINE au umtaje tu na zaidi ya hapo hutoweza kujulikana. Najiona mshindi sana kwani nawachezesheni mziki ninaoupenda kila siku na mnaufuta vilivyo. Akhsante Mwenyezi Mungu kwa aina hii ya upako na tunu ya mvuto uliyonipa.
Na leo umepiga shati la njano kama ugali wa yanga.
 
Pole mkuu. Inaonekana una frustration za kuhamishiwa mkoani na digrii yako huku wajanja hawajamaliza hata fom four wanaishi kibabe hapa town...
Karibu tena Dar. Ukija usifikie gest. Njoo ulale na kula bure kwangu. Wana JF sote ni ndugu...
 
Pole mkuu. Inaonekana una frustration za kuhamishiwa mkoani na digrii yako huku wajanja hawajamaliza hata fom four wanaishi kibabe hapa town...
Karibu tena Dar. Ukija usifikie gest. Njoo ulale na kula bure kwangu. Wana JF sote ni ndugu...
Mkuu sikuhamishwa. To put the record straight niliomba kuhama.

Kuongezea sifikii guest nafikia kwangu.

Kuongezea zaidi unaonyesha hii tabia umeiona na umeipenda. Sio tatizo. It's your call.

Mimi inanitia shaka.
 
Nina miezi kadhaa sipo Dar kwa sababu ya majukumu ya kikazi.

Niliporudi, juzi kati tulienda sehemu na mama watoto, nikawa natoa hela kwenye mtandao. Kuna wazee walikuwa wamekaa pembeni kama kawaida nikawasabahi na nikaendelea na yangu.

Baada ya kutoka pale mama watoto akaniuliza. Hivi watu siku hizi wakoje? Nikamuuliza kwani vipi? Akaniambia wale wazee walikuwa wanatuzungumzia sisi. Nikamuuliza kivipi? Akasema walikuwa wanaulizana kama sisi ni mke na mume kwa sababu wanaona tunafanana. Nikamuuliza uliwasikia kweli? Akajibu ndiyo.

Dah nikamwambia wife siku hizi watu hawakuteti nyuma ya nyumba kama zamani siku hizi watu wanakuteta huku unasikia ili ujibu mapigo wapate sababu.

Wiki hii nipo Dar. Leo nikawa nimeenda sehemu katika kuongea na simu nikawa nafuatilia issue moja ya kikazi. Kumbuka kwa sasa nipo mkoani kwa hivyo nilivyokuwa naongea na jamaa nikamweleza mimi ni fulani kutoka mkoa fulani ili anielewe. Basi tukaongea tukamaliza.

Wakati naondoka yule dereva pembeni yangu ambaye alikuwa amebeba wanawake kwenye gari akawa anawauliza kama kweli nafanya kazi mkoa niliotaja kwenye simu, kwa sababu nilimsikia nikamtizama kama dakika tatu hivi lakini akawa amekauka kama sio yeye aliyewauliza wale akina dada.

Dah nilimumaind sana yule jamaa. Sana sana tu. Ila nikasema moyoni shetani hawezi kunishauri cha kufanya.

Nikaondoka kwa sababu sihitaji kumdhibitishia mtu kwamba nasema ukweli. Na wakati mwingine maneno huwa hayatoshi kufikisha ujumbe. Na ziada ya maneno ni vitendo na gharama yake ni kubwa ukizingatia muda utakaopoteza.

Ni swali tu kwa baadhi ya wanaume wa Dar. Nini kimewakuta. Mbona mnakuwa kama wanawake. Kuna wanaume wengine humu JF wanaadika " wewe muongo" lakini wao hawana ukweli. Hawana data.

Amua tu kuwa dume au jike mbona operation zipo. Kama unahamu ya kuhamia upande mwingine amua tu na kama huwezi tuliza hizo pu*** zako zisizo z**.

Dume zima unaafuatilia mambo ya watu. Nikiongeza matatizo yangu kwako utaweza wewe?

Tutafute maendeleo. Achana na mambo ya watu.
Kwahio hii tabia imeibuka hio miezi michache uliokuwa nje ya Dar? Kama nimekuelewa vizuri wewe ni wa Dar ila uko nje kwa miezi kadhaa.
 
Kwahio hii tabia imeibuka hio miezi michache uliokuwa nje ya Dar? Kama nimekuelewa vizuri wewe ni wa Dar ila uko nje kwa miezi kadhaa.
Ni kweli mkuu.

Najiuliza nini kimewapata?

Tabia haina muda maalum wa kubadilika.

Nahisi hii miezi michache labda imeleta mabadiliko. Au labda sikuwa maakini kung'amua haya mabadiliko.

Sijui wewe unaonaje mkuu. Unawatetea mkuu?
 
Ni kweli mkuu.

Najiuliza nini kimewapata?

Tabia haina muda maalum wa kubadilika.

Nahisi hii miezi michache labda imeleta mabadiliko. Au labda sikuwa maakini kung'amua haya mabadiliko.

Sijui wewe unaonaje mkuu. Unawatetea mkuu?
Hao wanaume wa Dar wasikusumbue, wakitishwa na panya road wanajaaa 10 kwenye suzuki 4WD.
 
Hao wanaume wa Dar wasikusumbue, wakitishwa na panya road wanajaaa 10 kwenye suzuki 4WD.
Asante mama mtumishi. Nilivyomtizama yule dereva kwa takriban dakika tatu hakunitazama. Kama vile hakusema kitu.

Sasa mimi na wewe tunajua mchawi huja usiku ili usimwone. Na kesho yake anakusalimia kama sio yeye.

Ndiyo walewale.
 
Back
Top Bottom