Baadhi ya wanaChadema Iringa wataka Mbunge wao aachia nafasi za kisiasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baadhi ya wanaChadema Iringa wataka Mbunge wao aachia nafasi za kisiasa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Jan 15, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 15, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  Chadema Iringa wampa mbunge wao siku 7 ajiuzulu

  Imeandikwa na Frank Leonard, Iringa; Tarehe: 14th January 2011 @ 23:40

  HALI ya kisiasa ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Jimbo la Iringa Mjini si shwari.

  Hali hiyo inatokana na kuibuka kwa kundi la baadhi ya wanachama linalompinga mbunge wao, Mchungaji Peter Msigwa na kumtaka ajiuzulu nafasi ya uongozi wa chama ndani ya siku saba.

  Msigwa ambaye ni mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini kupitia chama hicho, pia ni mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Iringa.

  Kundi hilo linaloongozwa Abuu Changawa aliyekuwa mgombea udiwani wa kata ya Kwakilosa na ambaye pia ni Kaimu Mwenyekiti wa kata hiyo, mjini hapa, lilitoa tamko linalomtaka Mchungaji Msigwa kujiuzulu wadhifa wake wa uenyekiti juzi lilipokuwa likizungumza na wanahabari katika ukumbi wa Luxury Bar, mjini hapa.

  Changawa na kundi lake hilo, wanamtuhumu Mchungaji Msigwa kukihujumu chama hicho wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu na uchaguzi wenyewe, tuhuma ambazo Mchungaji Msigwa amekanusha kuhusika nazo pamoja na kupuuza ombi linalomtaka kujiuzulu baada ya kutakiwa kutoa ufafanuzi.

  Changawa alisema Mchungaji Msigwa anapoteza sifa ya kuendelea kuwa kiongozi wa chama hicho kwa madai kwamba katika uchaguzi huo, hakuwa anawafanyia kampeni wagombea wake wa udiwani, sababu iliyokifanya chama hicho kiambulie kiti kimoja tu kati ya 16 vya mjini hapa, tofauti na majimbo mengine ambako Chadema walishinda ubunge na kupata viti vingi vya udiwani.

  Hata hivyo Mchungaji Msigwa, hakuwa tayari kuyatolea ufafanuzi madai ya kundi hilo la wanachama, zaidi ya kusema kwamba hayana ukweli wowote juu yake na wanaomtuhumu wawasilishe malalamiko yao kwenye vikao halali vya chama.

  Alisisitiza kwamba, hatishiki na tamko la watu wanaomtaka ajiuzulu na kuongeza hatajiuzulu kama wanavyomtaka.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 15, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  Habari hii nimeibandika jamvini kuonyesha jinsi ambavyo Habari Leo ambavyo ni wepesi kupotosha ukweli ....................Kichwa cha habari kinatoa picha ya kuwa wamemshinikiza ajiuzulu ubunge lakini ukiisoma habari yenyewe ni kujiuzulu nafasi ndani ya chama!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Jan 15, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  Hivi angeliwezaje kukihujumu chama na bado yeye na mgombea Uraisi Dr. Slaa kuibuka kidedea katika Mkoa wa Iringi na hususani Iringa mjini? Hawa Habari Leo ni wababishaji sana....na huenda kuna mamluki wa ccm humo ambao ndiyo wanaleta hizo chokochoko................................ila hazina mashiko......................
   
 4. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #4
  Jan 15, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Wameanza chokochoko zao. Kwa nini wasiendelee kumpamba jk na serikali yake? Au wameishiwa maneno? Kwa taarifa yenu, chadema haibabaishwi na propaganda za kipuuzi namna hiyo.
   
 5. Nyamgluu

  Nyamgluu JF-Expert Member

  #5
  Jan 15, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 3,147
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Luxury bar kuna ukumbi wa kufanyia mkutano!!? Hahaha. Vikao vya bar hivyo ndio vyakuleta habari kwenye gazeti? Yani ni sawa na kusema mkutano ulifanyika katika ukumbi wa shikamo pub hapa sinza. LOL!
   
 6. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #6
  Jan 15, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,174
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  Ruta:

  thread zako nyingi huwa naziona kama ni content za magazeti.

  tatizo huwa hausemi ni magazeti gani.

  source ya taarifa yoyote ni muhimu sana.
   
 7. J

  Jukwaani Member

  #7
  Jan 15, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwacheni Mtumishi na msimwandame kwani naona kuna watu wanao pandwa na ccm kama Zito alivyo nunu liwa. Kwani mlimchagua mkiwa hamjui yaliyo tokea? wachenii udaku tunataka mabadiliko.
   
 8. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #8
  Jan 15, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  wametumwa hao
   
 9. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #9
  Jan 15, 2011
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,850
  Likes Received: 2,425
  Trophy Points: 280

  habari leo siku hizi limekuwa linaandika habari biased kidini na kisiasa....

  kuna wakati walikuwa wanakuza mgogoro wa kanisa na waumini kule Rukwa ..baada ya waziri mkuu kukiri waumini walikosea na kuomba radhi kwa niaba ya chama na serikali......wakaacha propaganda hizo..

  Juzi wamekuja na ugomvi wa maiti .....

  Sasa hii ya kichwa cha habari na habari kutofautiana nayo ni kali......bora waweke wazi kama wao ni gazeti la CHAMA au kidini mfano wa Al nnur au tumaini letu...tujuwe ....sio gazeti la serikali!!
   
 10. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #10
  Jan 15, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  Mahali uliponukuu nimeweka wazi ni habari leo sasa source ipi ulitaka au hukosoma?

   
Loading...