Baadhi ya njia unazoweza kutumia kupata wazo bora la biashara (Business Idea)

Nilicho gundua Casha ni Aibu na wala sio ukosefu wa mawazo ya biashara.

Mi naamini watu wengi wana mawazo mazuri ya kuanzisha biashara bila hata mtaji wa shilingi moja ila shida kubwa ni Aibu kumfikiria mtu atanionaje

Ebu soma historia hii

kuna kijana mmoja alitoka katika familia duni sana kimaisha alikuwa anaishi na bibi yake alikuwa hana mama wala baba wazazi wake walitangulia mbele ya haki akiwa mdogo kwa hiyo alilelewa na bibi yake kwa tabu na masha alisoma mpaka kidato cha nne.

alipomaliza shule alihangaika asijue la kufanya mpaka siku moja alipokaa chini na kufikiri kwa undani zaidi nitafanya nini katika maisha yangu magumu kiasi hiki, wakati akitafakari akatokea mama moja akamuomba akamtupie taka kwani taka zake zilikua zimejaa kwenye viroba alivyohifadhia taka.

Kijana alikua hana kiburi bila ya kujivunga akanyanyuka na kwenda kutupa taka aliporudi yule mama akampa 1000 akatokea na mama mwingine akamwambia na mimi naomba ukanimwagie na zakwangu akaenda na yule mama akamlipa pia 1000 kwa jioni ile akawa tayari ana 2000 iliyo muwezesha kupata mlo wa jioni.

Siku ya pili aliamka asubuhi na kuanza kupita kila nyumba na kuanza kuulizia kama wanahitaji huduma ya kumwagiwa taka cha kushangaza kwa siku nzima alifanikiwa kupata sh.20000 alifurahi sana ingawa majirani walimuongelea ,walimdharau, na wengine walimbadilisha jina kabisa na kumuita mwaga taka hakujali alichojali ni nini anapata na maisha yake anayaendesha vipi,hakujali alijipa moyo na kusema hata wakiniita mwaga taka hawanisaidii shida zangu nazijua mwenyewe.

Aliendelea na kazi yake ya kupita nyumba hadi nyumba kukusanya taka mpaka akafanikiwa kutengeneza mkoko teni wa kuzolea taka hakuishia hapo akatengeneza mikokoteni mingine zaidi na kuanza kuajiri vijana wenzie ili wamsaidie akaendelea mpaka akafikia kiwango cha kufungua ofisi mtaani kwao ,akanunua magari ya kuzolea taka sasa ni tajiri mkubwa watu hawamwiti tena mzoa taka bali ni bosi mzee mkubwa mkuu ndio majina yake kwa sasa
ana magari ya kisasa kabisa ya kuzolea taka na kuzisaga na kuwa mbolea anauza mbolea na kukusanya taka vyote vinamuingizia hela.

Nachojaribu kusema ni kwamba watu wengi huzuia malengo yao kwa Aibu ya kumuogopa fulani, utamkuta msichana kamaliza shule ana ujuzi mzuri wa kutengeneza chapati au maandazi na mtaani kwao hakuna vitu hivyo anaogopa kutengeneza kisa aibu.

Kwahiyo biashara sio mtaji ni uwezo wa kufikiri tu na kuweka Aibu pembeni.
 
Kweli kabisa mtaji ni shida. Lakini shida ni kitu kizuri kama kitatufanya tuichukie shida na tufikiri namna ya kuitatua. Uaminifu ni mtaji, vikundi vya watu waaminifu vinasaidia sana katika upatikanaji wa mitaji. Sio lazima kwenda benki, inawezekana kutengeneza mfuko wa kikundi na kukopeshana kwa masharti ya kujipangia. Uaminifu na uwajibikaji ni muhimu. Tunaweza kufika mbali sana. Pia tujue hatutakiwi kuishia kwenye kuwaza, tuchukue hatua.

" HUWEZI KUFIKA NG'AMBO YA MTO KWA KUYATAZAMA MAJI"
 
Mimi naweka tu mkazo kwamba mtaji ni wazo na sio pesa nikijitolea mfano mm mwenyewe natama sana kufanya biashara nakumbuka kipindi cha nyuma kabla cjaanza kuzishika pesa nilikuwa nasema nikipata laki moja naanza biashara lakini cha ajabu saivi nashika hadi million tatu mkononi na sina biashara yoyote naishia kusema tatizo ni mtaji nabaki kunywa pombe tu na kubadilisha nyumba za kupanga kila siku kutoka za bei ya chini kwenda juu na kununua furniture kali akati hazinisaidii ila ni kutaka muonekano kwenye jamii...lakini najua ningekuwa na wazo zuri la biashara myb mpaka leo ningeshakuwa millionea....kwaiyo tujipange jamani hizi show off hazina faida...
 
Ni keli watu wanazania Biashara ni Mitaji mikubwa, Unaweza kabidhiwa Bilon Moja na ukashindwa vibaya sana katika biashara, Biashara sio kuwa na Pesa bali nistrategies,

Ni kweli kabisa hata wale mama Lishe wa miji mikubwa kama Dar na kwingineko wana kuwa wanapata faida za kutosha tatizo kubwa ni kukosa mikakati na Vision za kuweza kuvuka kutoka hapo walipo na kuja kumiliki Migahawa mikubwa, Inawezekana kabisa mama lishe kuja kumiliki migahawa mikubwa kabisa, Ila wanakosa focus that is why unawakuta katia levo moja kwa miaka zaidi ya 20, ambapo ilitakiwa wawe wamegraduate from Small to Medium business
Ni kweli kabisa
 
Kweli kbxa kaka, watu wengi wana aibu kwamba wataonekanaje kwa jamii iliyo wazunguka...pia kuna hili swala la kukatixhana tamaa pia n tatizo kubwa ktk miongoni mwetu.
 
Back
Top Bottom