Baadhi ya njia unazoweza kutumia kupata wazo bora la biashara (Business Idea)

Nami naomba nichangie kidogo...

Mi nafikiri alichoandika mdau Chasha ni cha kweli. Tusianze kulalamikia mitaji kama excuse. Cha msingi ni kuwa na nia thabiti, ambayo kwayo inatoa nguvu kubwa sana. Ukiwa na nia, unaweza kutafuta mtaji through kupiga debe, kufanya vibarua and the like.

Nilijaribu kuongea na rafiki zangu pale Kariakoo, ambao wanauza maji, ambao walinieleza kuwa ukiondoa mtaji, wanaweza kutengeneza ziada ya Tsh. 12,000-13,000, na siku ya biashara mbaya wanatengeneza ziada ya Tsh. 4000 at minimal.

Aidha, wale akina mama wanaouza matunda nao wana make ziada ya kiasi kama hicho,ambapo wao wanachukua matunda kule Temeke Stereo kwa Tsh.50-70 kwa embe moja,lakini kariakoo wanauza kwa Tsh. 250-300, na kwa juhudi zao matunda haya yanaisha.

Niliozungumza nao wananieleza tayari wameshanunua plots (walianza biashara hiyo miaka mi3 iliyopita). Hawa waliongozwa na nia iliyowapa nguvu ya kusonga mbele, japo vipo vikwazo walivyokutana navyo, nawanavyokutana navyo, lakini wanasonga mbele.

Hivyo,nafikiri mtaji mkubwa aliokuwa nao mtu ni mind set,na mtaji mwingine ni kuwa na mahusiano mema na jamii, ambayo kwayo unaweza pata mawazo mengi mazuri, na inawezekana ukaaminika na mtu/watu w/akakupesha mtaji.

Nawasilisha mchango wangu

Issue hapa ni guts..ni watu wangapi tunao huo ujasiri wa kuamua maamuzi magamu (kujipanga barabarani) au ndio ile mpaka upigike ndio ukubali hali?
 
Business idea ndio kila kitu kwenye dunia ya sasa unaweza usiwe na pesa lakini unabness idea nzuri ambayo umeweka mikakati jinsi ya kutekeleza idea yako na ukafanikiwa.vile vile idea inweza ikawa si ya kwako lakini ukaweza kuendeleza idea ya mtu mwingine na ukafanikiwa sana kwa mfano wengi wameisikia forever living na jinsi inavyo fanya kazi lakini mimi jinsi nlivoamua kufanya biashara ya foever nimejikuta imebadilisha ulimwengu wa maisha yangu kwa sehemu kubwa sana hivi leo isingekuwa biashara hii sijui ningekuwa wapi.
 
Mitaa mingine noma kwa kamati za ufundi, mfano huku kwetu nilifungua biashara ya duka lakini ilibidi nilifunge. Utakuta kwa wiki pesa zinapotea kimiujiza hasa elfu kumi kumi. Unauza kisha nazitenga elfu kumi peke yake kwa sababu siyo chenji. Lakini nikija kucheki baadaye nakuta hazimo wakati full time nakuwemo mimi mwenyewe dukani! Nilinyoosha mikono kwani sikutaka kuanza kumtafuta mbaya wangu labda ningeua mtu ningemtambua.
 
Back
Top Bottom