ReganKingdom
Member
- Apr 19, 2017
- 19
- 12
Katika ngazi za uongozi, madaraka(cheo) ni ngazi ya chini sana kwakua mtu unaweza kuwa kiongozi bila madaraka. Lakini huwa ndio ngazi ya kuanzia kwa viongozi wengi.
Madaraka ni nafasi tu ya ki-uteuzi ambayo mtu yeyote huweza kupatiwa na mtu mwenye mamlaka hayo. Lakini uongozi ni kipaji endelevu cha kuongoza watu tofauti tofauti kwa hiari(kibali) yao.
Kiongozi hateuliwi bali hutokea kutokana na muendelezo wa matendo yake mwenyewe ndani ya cheo mahususi ila yenye mchango mzuri kwa watu na ukuaji wao. Ni vizuri kuona nafasi ya madaraka kama mualiko wa mtu kuanza kujijenga kuwa kiongozi ila sio kuwa na mamlaka nguvu za kutawala.
Kiongozi mzuri ni yule ambae hategemei tu mamlaka/sheria yanayotokana na cheo chake kushinikiza jambo au kusikilizwa. Sio tabia ya kiongozi mzuri kutumia cheo kufanya watu wawe wafuasi. Kuna madhara makubwa sana ya mtu akijiita kiongozi kwa kutumia madaraka.
yafuatayo ni baadhi ya madhara:
-kiongozi anaetegemea cheo na madaraka yake kuongoza hupata wafuasi wasio waaminifu,wanafuata kwakua tu inabidi kutokana na nguvu za kiutawala za muhusika.
-viongozi wa namna hii hukosa nguvu za ushawishi kwani watu huwa na mipaka ya kushawishika sawa na mipaka ya kimamlaka aliyopewa huyu mtu.
Viongozi wa namna hii wanakua maboss na sio viongozi,kwakua ufanisi wao unategemea Zaidi taratibu,sheria na sera ili kuongoza watu jambo ambalo huzuia ubunifu na kujitolea kwa watu unaowaongoza.
Viongozi wanaotegemea mamlaka pia hupata shida sana kufanya kazi na vijana, watu wenye elimu kubwa na watu wa kujitolea (volunteers)
-pia huwa wanakosa marafiki, kwani hupenda kukumbusha watu kuwa yupo juu yao, na watu wapo kumsikiliza yeye tu na sio kinyume na hivyo. Pia hutishika sana na vipaji au ubunifu unaochipukia kwani wanaamini ni tishio kwa cheo chake.
Viongozi wa namna hii huwekeza nguvu zote kulinda cheo huku wakidharau nguvu ya kukubalika na watu lakini kama ilivyo vyeo havidumu milele hasi kwa mtu wa namna hii muda huwa mfupi Zaidi na hawapati nafasi ya kukua.
Yapo madhara mengi. Ni muda Viongozi kutambua kuwa cheo ni uwanja wa kujifunza kuwa kiongozi wa watu.
Na kiongozi wa watu ni yule ambae hutafuta ruhusa ya kuongoza watu kwa watu wenyewe baada tu ya kupata cheo kwa kuweka maslahi ya watu mbele ya yale ya kwake mwenyewe.
Huhamasisha ubunifu na ushirikiano, husikiliza Zaidi ya kutaka kusikilizwa,hukuza uzalishaji na kuwa kocha wa wengine.
Kuongoza wengine na Zaidi ya yote kumchukulia kila mtu kama mwanadamu mwenye mchango.