N'yadikwa
JF-Expert Member
- Aug 10, 2014
- 8,263
- 12,666
Kuna watu kazini wamegeuza vyeo kuwa mali yao binafsi.
Ukiona mwenzako anastahili kupanda cheo, badala ya kumuunga mkono, unaanza figisu, kumzuia, kumchafua au kutengeneza mazingira ya yeye asipate nafasi.
Lakini kuna jambo moja mnalisahau:
Kumzuia mwenzako kupanda cheo hakumaanishi umemshinda.
Wakati mwingine umempa sababu ya kutafuta njia nyingine za kujenga maisha yake.
Kumbuka, cheo hakidumu milele.
Leo wewe ni Mkuu wa Kitengo, Meneja, Mkurugenzi au kiongozi wa taasisi.
Watu wanakuheshimu, simu zinapokelewa kwa haraka, una ofisi nzuri na mamlaka.
Lakini kesho ukistaafu, hayo yote yanaweza kubaki ofisini.
Hata kama ulikuwa unapokea mshahara mkubwa kiasi gani, mshahara peke yake hauhakikishi uhuru wa kifedha baada ya ajira.
Tatizo kubwa zaidi ni kwamba wakati mwingine cheo kinakubana kujenga mazingira ya kujitegemea.
Unaweza kutumia miaka 20 ukipambana kulinda nafasi yako, kuwazuia wengine wasipande, huku mwenzako ambaye hakupewa nafasi sababu yako akijenga biashara, kilimo, nyumba za kupangisha, uwekezaji na vyanzo vingine vya kipato.
Halafu siku ya kustaafu mnakutana wote nje ya mfumo.
Mwenzako anaweza kuwa hana cheo tena, lakini ana mali na vyanzo vya kipato.
Wewe una cheo kilichostaafu.
Hapo ndipo utagundua kwamba huenda hukuwa unawalinda wenzako dhidi ya maendeleo ulikuwa unawachelewesha, lakini wakati huohuo ukijichelewesha mwenyewe.
Ndiyo maana wakati mwingine utaona mtu aliyekuwa na cheo kikubwa kazini akistaafu na maisha yake yakaanza kuwa magumu, wakati mtu aliyekuwa kwenye nafasi ya kawaida kabisa anaendelea vizuri kiuchumi.
Na hapa kuna jambo lingine la kutafakari:
No wonder wakati mwingine madereva katika public service wanaweza kuwa na hali nzuri ya kiuchumi kuliko baadhi ya maofisa.
Kwa nini?
Kwa sababu si kila mafanikio yanatokana na cheo.
Mtu anaweza kuwa dereva, lakini akawekeza kwenye kilimo, nyumba, biashara, mifugo au miradi mingine kwa miaka mingi. Madereva wanafanikiwa kwa sababu ya fursa ya muda waliyonayo...anakupeleka ukafukuzie perdiem wakati anapoenda kuosha gari anapitia kwenye miradi yake!
Wakati huo huo afisa mwenye cheo kikubwa anaweza kuwa ametumia nguvu zake zote kulinda cheo, kujenga ushawishi na kuhakikisha wengine hawapati nafasi.
Mwisho wa siku wote wanastaafu.
Cheo kinaishia kwenye ofisi. Maisha yanaendelea nje ya ofisi.
Kwa hiyo kama una nafasi ya kumsaidia mwenzako kupanda, msaidie.
Kama amestahili, mpe nafasi.
Usimtengenezee figisu kwa sababu unaogopa siku moja atakuwa juu yako.
Kumbuka: nafasi ya mwenzako haipunguzi thamani yako. Kitu kingine "anaejua anajua tu...huwezi kumshusha"
Na kama una madaraka leo, tumia sehemu ya nguvu hiyo kujenga taasisi, watu na mazingira ambayo hata baada ya wewe kuondoka, wengine wataendelea.
Kwa sababu ukweli mchungu ni huu:
Siku ya kustaafu hakuna anayekuuliza ulikuwa unawazuia watu wangapi kupata vyeo.
Watu wanaangalia umejenga nini, umeacha nini na maisha yako yakoje baada ya cheo.
Watoto wako hawatarithi cheo chako!
Kwa hiyo, stuka!
Usitumie ujana wako wote kulinda kiti ambacho siku moja utalazimika kukiacha.
Jenga watu. Jenga mali. Jenga uwezo wa kujitegemea.
Kubwa kuliko yote acheni roho mbaya huko makazini.
N'yadikwa!