EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,483
- 15,308
Wakati sakata la Miss Tanzania 2014 likiendelea, hebu tujikumbushie baadhi ya kashfa za Miss World zilizowahi kutokea. Tokea Mashindano haya yaanzishwe mwaka 1951, baadhi ya washiriki walishakumbwa na kashfa mbalimbali kama ulevi, kuwa na watoto (single mothers) na wengine kugunduliwa baadae kuwa walikuwa wanafanya u-model kisirisiri kwa kupiga picha huku wakiwa uchi. Post zinazofuata nitaonyeresha baadhi ya kashfa za Miss World pageant. Kama unajua nyingine waweza kuongezea. Habari na picha kwa msaada wa http://www.mirror.co.uk/news/uk-news/miss-world-top-10-scandals-1266379
Miss World wa kwanza kabisa alikuwa Kiki Hakansson kutoka Sweden. Akiwa Miss World wa kwanza na wa mwisho kupewa taji huku alikiwa amevaa vazi la kuogelea.
Mwanzilishi wa Miss World Eric Morley alinukuliwa akisema kuwa washiriki wa Miss World walitakiwa kuwa na umri wa miaka 17 hadi 25, mrefu, uzito wa kilo 50 hadi 57, kiuno cha inch 22 hadi 24, hips za inch 35 hadi 36 na siyo zaidi au pungufu ya hapo.
Aliongeza kuwa washiriki ni lazima wawe na sura nzuri, meno mazuri, nywele za kutosha na miguu mizuri mbele na nyuma na kuchunguzwa kwa makini kama wana wana alama alama kwenye magoti.
Mwaka 1965, Miss United Kingdom Lesley Langey alishinda Miss World lakini baadae ushindi wake ulitawaliwa na kashfa ya picha zake alizopiga akiwa uchi.
Hakuvuliwa Miss World lakini u-miss wake ulikuwa hauna tena maana aka meaningless.
Mwaka 1966 wanafunzi nane wa Chuo Kikuu cha Cambridge walijaribu kumteka Miss World alipotembelea chuoni hapo. Miss World wa mwaka huo alikuwa Johana Carter kutoka Afrika ya Kusini.
Mpango wa kumteka ulishindikana baada ya Miss World huyo kupiga mayowe huku mlinzi wake akipambana vikali na genge hilo la wanafunzi kwa kutumia mwavuli wake.
Wanafunzi hao walitaka kumteka Miss World kama njia ya kudai fedha za kuendesha charity ya wanafunzi iliyokuwa inafanyika wiki hiyo chuoni hapo.
Mwaka 1970 wanawake waliandamana kupinga mashindano ya Miss World yaliyokuwa yanafanyika Marekani na kuongozwa na mchekeshaji Bob Hope.
Waandamaji hao walitupa mabomu kwenye stage na kutegeshea mengine chini ya gari la BBC lililokuwa nje ya ukumbi ili kuzuia mashindano hayo yasionyoshwe kwenye TV.
Hata hivyo, hakuna aliyejeruhiwa na mashindano hayo yalionyeshwa kama kawaida.