Baadhi ya kashfa za Miss World pageant

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,483
15,308
Wakati sakata la Miss Tanzania 2014 likiendelea, hebu tujikumbushie baadhi ya kashfa za Miss World zilizowahi kutokea. Tokea Mashindano haya yaanzishwe mwaka 1951, baadhi ya washiriki walishakumbwa na kashfa mbalimbali kama ulevi, kuwa na watoto (single mothers) na wengine kugunduliwa baadae kuwa walikuwa wanafanya u-model kisirisiri kwa kupiga picha huku wakiwa uchi. Post zinazofuata nitaonyeresha baadhi ya kashfa za Miss World pageant. Kama unajua nyingine waweza kuongezea. Habari na picha kwa msaada wa http://www.mirror.co.uk/news/uk-news/miss-world-top-10-scandals-1266379

Miss%20World%201957%20Marita%20Lindahl.jpg


Miss World wa kwanza kabisa alikuwa Kiki Hakansson kutoka Sweden. Akiwa Miss World wa kwanza na wa mwisho kupewa taji huku alikiwa amevaa vazi la kuogelea.

Mwanzilishi wa Miss World Eric Morley alinukuliwa akisema kuwa washiriki wa Miss World walitakiwa kuwa na umri wa miaka 17 hadi 25, mrefu, uzito wa kilo 50 hadi 57, kiuno cha inch 22 hadi 24, hips za inch 35 hadi 36 na siyo zaidi au pungufu ya hapo.

Aliongeza kuwa washiriki ni lazima wawe na sura nzuri, meno mazuri, nywele za kutosha na miguu mizuri mbele na nyuma na kuchunguzwa kwa makini kama wana wana alama alama kwenye magoti.

Lesley%20Langley


Mwaka 1965, Miss United Kingdom Lesley Langey alishinda Miss World lakini baadae ushindi wake ulitawaliwa na kashfa ya picha zake alizopiga akiwa uchi.

Hakuvuliwa Miss World lakini u-miss wake ulikuwa hauna tena maana aka meaningless.

17th%20November%201966


Mwaka 1966 wanafunzi nane wa Chuo Kikuu cha Cambridge walijaribu kumteka Miss World alipotembelea chuoni hapo. Miss World wa mwaka huo alikuwa Johana Carter kutoka Afrika ya Kusini.

Mpango wa kumteka ulishindikana baada ya Miss World huyo kupiga mayowe huku mlinzi wake akipambana vikali na genge hilo la wanafunzi kwa kutumia mwavuli wake.

Wanafunzi hao walitaka kumteka Miss World kama njia ya kudai fedha za kuendesha charity ya wanafunzi iliyokuwa inafanyika wiki hiyo chuoni hapo.
b00tkpc1_640_360.jpg



Mwaka 1970 wanawake waliandamana kupinga mashindano ya Miss World yaliyokuwa yanafanyika Marekani na kuongozwa na mchekeshaji Bob Hope.

Waandamaji hao walitupa mabomu kwenye stage na kutegeshea mengine chini ya gari la BBC lililokuwa nje ya ukumbi ili kuzuia mashindano hayo yasionyoshwe kwenye TV.

Hata hivyo, hakuna aliyejeruhiwa na mashindano hayo yalionyeshwa kama kawaida.​



 
Mary%20Stavin,


Mary Ann Catrin Stavin alishinda Miss World mwaka 1971, hata hivyo alishindwa hata kutembea kwenye stage kutokana na kulewa baada ya kunywa chupa moja ya whisky kwenye ukumbi wa Royal Albert Marekani yalikokuwa yanafanyika mashindano hayo.
 
Marjorie%20Wallace


Mwaka 1973 Miss United States Marjorie Wallace alishinda Miss World lakini alifurahia kwa miezi minne tuu baada ya kunyang'anywa u-Miss World huo kisa kutoka na wanaume wengi ma-celebrities kitu ambacho kilimfanya kutekeleza mission yake ya kuwa Miss World.
 
Kumbe kashfa ni jambo la kawaida kwa hawa watu...kwahyo mwana wa mtemvu hatakuwa wa kwanza kumbe
 
1974:%20%20Helen%20Morgan,%20Miss%20United%20Kingdom%20is%20crowned%20Miss%20World%201974.


Mwaka 1974 Miss Wales, Helen Elizabeth Morgan, alishinda Miss World.

Hata hivyo alinyang'anywa taji hilo siku nne baadae baada ya kugundulika alikuwa na mtoto (single mother) wa mwaka mmoja na nusu, kitu ambacho sheria za Miss World zinakataza mpaka sasa.

Alimwacha mwanae nyumbani na bibi yake wakati yeye akishirikiri Miss World.
 
2nd%20December%201980:%20%20Kimberley%20Santos,%20Miss%20Guam,%20elected%20Miss%20World%201980%20holds%20her%20crown%20high%20above%20her%20head


Mwaka 1980, Gabriella Brum kutoka Ujerumani alishinda Miss World lakini alidumu na taji kwa siku moja tuu baada ya boyfriend wake kudai kuwa alikuwa hamuuingi mkono demu wake kuwania taji hilo.

Baadae ilikuja kugundulika kuwa alikuwa amepiga picha za uchi kwenye magazeti.

Nafasi yake ilichukuliwa na Miss Guyam Kimberley Santos aliyeko kwenye picha hapo juu.
 
Mary%20Stavin,


Mary Ann Catrin Stavin alishinda Miss World mwaka 1971, hata hivyo alishindwa hata kutembea kwenye stage kutokana na kulewa baada ya kunywa chupa moja ya whisky kwenye ukumbi wa Royal Albert Marekani yalikokuwa yanafanyika mashindano hayo.

Ha ha ha ha ha..i like it! Imenikumbusha mrembo mmoja kwenye harusi ya kaka yake akachukua kipaza sauti na kuanza kuwatambulisha familia yake..ilipofika zamu yake kujitambulisha akasahau jina lake..hahah Mc alipomfuata akamuuliza kwa kunong'ona huku sauti ikisikika kwenye Microphone .."Eti mi naitwa nani" ha ha,...bongo bhana!
 
Ulla%20Weigerstorfer


Mwaka 1987 Miss Austria Ulla Weigestorfer (katikati) alinyang'anywa taji la Miss World baada ya kugundulika kuwa alikuwa amepiga picha za uchi.

Boyfriend wake ndiye aliyechapisha picha hizo ili watu wazione.
 
Miss%20World%20Diana%20Hayden%20(C)


Mwaka 1997, Diana Hayden (katikati) kutoka India alikuwa mzuri na alifanya vizuri sana kwenye maswali aliyoulizwa na hivyo kushinda Miss World.

Hata hivyo, ilimbidi aachie taji hilo baadae baada ya kugundulika kuwa alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na jaji moja aliyekuwa kwenye panel ya kutoa maamuzi.
 
Ha ha ha ha ha..i like it! Imenikumbusha mrembo mmoja kwenye harusi ya kaka yake akachukua kipaza sauti na kuanza kuwatambulisha familia yake..ilipofika zamu yake kujitambulisha akasahau jina lake..hahah Mc alipomfuata akamuuliza kwa kunong'ona huku sauti ikisikika kwenye Microphone .."Eti mi naitwa nani" ha ha,...bongo bhana!
nawe vp umelewa tayari mbona unaleta utani
 
Nigeria


Mwaka 2002 kulizuka tafrani nchini Nigeria na kusababisha vifo vya watu 215 na wengine 500 kujeruhiwa.

Ilidaiwa kuwa tafrani hiyo ilitokana na makala ya mwandishi wa Kinigeria aliyeandika kuwa kama Mtume Mohammad angemchagua mshiriki mmoja kama mke, jambo ambalo lilisababisha taharuki kubwa kati ya Waislamu na Wakristu.
 
Outside%20the%202011%20Miss%20World%20final%20from%20Earls%20Court%20in%20London,%20as%20protesters%20demonstrate%20outside%20Earls%20Court.


Mwaka 2011 karibu wanawake 200 waliandamana London siku ya maadhimisho ya miaka 60 ya Miss World.

Baadhi ya waandamaji walioshiriki maandamano ya mwaka 1970 walikuwepo pia kwenye maandamano hayo.
 
Outside%20the%202011%20Miss%20World%20final%20from%20Earls%20Court%20in%20London,%20as%20protesters%20demonstrate%20outside%20Earls%20Court.


Mwaka 2011 karibu wanawake 200 waliandamana London siku ya maadhimisho ya miaka 60 ya Miss World.

Baadhi ya waandamaji walioshiriki maandamano ya mwaka 1970 walikuwepo pia kwenye maandamano hayo.

Sababu ya maandamano ilikuwa ni nini mkuu EMT
 
Last edited by a moderator:
Mwaka 2014 Sitti mtemvu alichaguliwa kuwa Miss Tanzania. Ajabu Passport yake na cheti chake cha kuzaliwa vinapishana miaka ya kuzaliwa wakati ukiomba passport lazima uambatanishe na cheti cha kuzaliwa!
 
kwa sasa bongo ni Sitti Mtenvu haya yalokwisha pita yaachwe kwanza, na yeye avue taji ndio tujue ni muendelezo wa hawa dada zake
 
Back
Top Bottom