KWELI Baadhi ya Dawa za kutibu Malaria zinaweza kusababisha mzio mwilini, ikiwemo Kuchubuka Uume na Midomo

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Mdau wa JamiiForums analalamika kuwa alitumia dawa za kutibu Ugonjwa wa Malaria zinazoitwa EKELFIN ambazo baadaye zilimsababishia kupatwa na mchubuko sehemu za siri na midomoni.

IMG_9090.jpeg

Anashangaa kwanini Serikali haitoi taarifa kwa watumiaji juu ya madhara ya dawa hizi kwa binadamu.

Ni kweli kuwa dawa hizi zinaweza kusababisha athari tajwa?
 
Tunachokijua
Malaria ni ugonjwa unaosababishwa na vimelea vya Plasmodium ambayo husambazwa na mbu jike aina ya anopheles.

Dalili za awali za ugonjwa huu huanza kuonekana takriban siku 10-15 tangu mhusika ang’atwe na mbu mwenye vimelea na huhusisha kuongezeka kwa joto la mwili, uchovu, kukosa hamu ya kula, maumivu ya kichwa, kuharisha na kutapika pamoja na kuongezeka kwa mapigo ya moyo.

Matibabu yake
Msingi wa matibabu ya ugonjwa huu umekuwa unabadilika ili kuongeza ufanisi kwenye kudhibiti vimelea vyake, pamoja na kupunguza maudhi ya dawa yanayoweza kujitokeza kwa mgonjwa.

Mwongozo wa matibabu unaopaswa kutumiwa na watoa huduma wote wa afya Tanzania Bara uliotolewa na Serikali kupitia Wizara ya afya mwaka 2021 yaani “STANDARD TREATMENT GUIDELINES AND NATIONAL ESSENTIAL MEDICINES LIST FOR TANZANIA MAINLAND” unaelekeza matumizi ya Artemether-Lumefantrine (ALU) kama dawa chaguo la kwanza kwenye kutibu ugonjwa wa Malaria ambapo Dihydroartemisinin-Piperaquine inaweza kutumika kama mbadala.

Ikiwa matumizi ya sindano yatahitajika, Artesunate au Artemether zinaweza kutumika.

Madai ya Baadhi ya Dawa Kusababisha Mzio
Madai yanayojadiliwa hapa yanahusisha dawa inayoitwa Ekelfin, jina la kibiashara linalotumiwa na kampuni ya ELYS CHEMICAL INDUSTRIES LTD. Dawa hii huwa na mjumuiko wa Sulfadoxine na pyrimethamine, baadhi hupenda kuita SP.

JamiiForums imebaini kuwa, Kwa asili yake, Sulfadoxine ni kemikali yenye asili ya sulfa ambayo kwa baadhi ya watu husababisha allergy (mzio) kubwa au ndogo.

Inaweza kusababisha vidonda midomoni na kwenye maeneo yenye ngozi laini mwilini hasa midomo na sehemu za siri, kupauka, mabaka na kutokwa na malengelenge kwenye ngozi, kupungua kwa mkojo, kusikia milio kwenye masikio pamoja na umanjano hivyo madai ya mdau yapo sahihi.

Mfano wa majina mengine ya kibiashara ya dawa hii ni Malafin, sulphadar na Fansidar. Zote ni dawa zinazoweza kuleta madhara yanayofanana kwa mhusika.

Ili kuzuia madhara haya, wataalamu huuliza kwanza kama mgonjwa aliwahi kupata mzio wa aina yoyote ya dawa pamoja na historia yake ya awali.

Aidha, Artemether-Lumefantrine (ALU) ni dawa inayofaa zaidi kwa mtu mwenye mzio wa aina hii.
Mm naona hizo dawa zipo sahihi ila utofauti ni kwamba hizo dawa inatakiwa asiwepewe mtu ambaye anamagonjwa mengine.
kama kisukari nk
Na huwa wanqandikaga kwenye kile kikaratasi ambacho kinakuwaga kwenye dawa ila watu wanakuwaga wabishi

Ila na tatizo la wabongo wengi wanapenda kukalili magonjwa mtu akisikia kichwa kinamuuna kidogo tu utasikia hii ni malaria anachukua chap dawa za malaria bila hata kwenda kwa doctor.
Madhara yake ndio hayo.
 
Mdau mmoja wa JamiiForums.com analalamika kuwa alitumia dawa za kutibu Ugonjwa wa Malaria zinazoitwa EKELFIN ambazo baadaye zilimsababishia kupatwa na mchubuko sehemu za siri na midomoni.

View attachment 2427102

Anashangaa kwanini Serikali haitoi taarifa kwa watumiaji juu ya madhara ya dawa hizi kwa binadamu.

Ni kweli kuwa dawa hizi zinaweza kusababisha athari tajwa?
Hii ni kweli mimi nikitumia dawa hizi huwa natokewa na mchubuko sehemu za siri kwenye kichwa cha uume mwishoni niliamua kuachana nazo kwa kuwa nina mzio na dawa nyingi mno hali inayopelekea kutumia mitishamba zaidi.
 
Kuhusu metakelfin/ekelfin kuwa na athari hizo ni kweli kabisa. 2012 nilitumia hizo dawa na kutokewa na mchubuko kwenye kichwa cha uume. Huo mchubuko ni kama ule ambao umepata kidonda af kinaweka gamba gumu wakati kinakauka. Nilijiuliza je ni ugonjwa wa zinaa?

Basi baada ya siku kadhaa hali ile iliondoka na hofu ya ugonjwa wa zinaa ikaondoka sababu kulikuwa hamna maumivu yoyote katika uume.

Baada ya kama miezi minne nikapata malaria tena. Nikaandikiwa kutumia metakelfin/ekelfin. Nilivotumia dozi kuamka kesho yake asubuhi nakuta tena hali ile ya mara ya kwanza kwenye uume. Basi nikarudi hospital na kumwambia daktari kuhusu hali ile.
Dakatari alinianbia metakelfin/ekelfin ina sulphur ambayo wakati mwingine inaleta athari hasi kwa mtumiaji(sijui kama ufafanuzi huu ni sahihi).

Kuanzia hapo nikaacha kabisa kutumia ekelfin/metakelfin. Kabla ya matukio hayo nilishatumia hiyo dawa kwa zaid ya miaka 5 na kulikuwa hamna athari hizo mwanzo.
 
Mmi huwa Sichagui dawa. Mwili wangu unachukua dawa yyte ile hta iwe ya kenya sipatagi madhara yoyote japo nitachelewa kupona tofauti na za kwetu huwa nawai kupona hasa malaria
 
Mdau mmoja wa JamiiForums.com analalamika kuwa alitumia dawa za kutibu Ugonjwa wa Malaria zinazoitwa EKELFIN ambazo baadaye zilimsababishia kupatwa na mchubuko sehemu za siri na midomoni.


Anashangaa kwanini Serikali haitoi taarifa kwa watumiaji juu ya madhara ya dawa hizi kwa binadamu.

Ni kweli kuwa dawa hizi zinaweza kusababisha athari tajwa?
Ungetoa hata kapicha hivi tukaone, maana huku kwetu tukifika duka la dawa tunasema tu namba dawa za malaria hata hatujui effects. Lakini hapa najifunza jambo
 
Mdau mmoja wa JamiiForums.com analalamika kuwa alitumia dawa za kutibu Ugonjwa wa Malaria zinazoitwa EKELFIN ambazo baadaye zilimsababishia kupatwa na mchubuko sehemu za siri na midomoni.


Anashangaa kwanini Serikali haitoi taarifa kwa watumiaji juu ya madhara ya dawa hizi kwa binadamu.

Ni kweli kuwa dawa hizi zinaweza kusababisha athari tajwa?
Hivi bado malaria yapo? Huku nyanda za juu kaskazini mashariki tulishasahau hiyo kitu.
 
Hii imekaa vipi kitaalamu? Hali hii inaendelea kushamili tokea siku ambayo mbu walipoamua kunigeuza mboga kwenye makazi mapya
 
24 Reactions
Reply
Back
Top Bottom