Baada ya zoezi la uchaguzi wa Serikali za mitaa kukamilika, natabiri yafuatayo kutokea

Mackanackyyy

JF-Expert Member
Mar 26, 2019
2,338
5,263
1. Haitawezekana kuuza ama kununua kitu chochote kama hauna kadi ya CCM. Mfano Shamba, kwa sababu mauziano ya mali kama hizi zinahitaji kuandikishana kwa Mwenyekiti wa Mtaa, Kitongoji ama Kijiji.

2. Haitawezekana kupata frame ya biashara kwenye maeneo kama viwanja vya mpira, masoko makuu ya miji, ama stand za mabasi, kama inajulikana wewe si mwanaCCM.

3. Haitawezekana kupata barua ya Utambulisho, mfano kukusaidia kufungua Akaunti bank, ikiwa inajulikana wewe si mwanachama wa CCM.

4. Kama una mashauri mahakamani, na inajulikana Wewe si mwanaCCM, Haitawezekana kupata barua ya kukusaidia, mfano kupata dhamana.

5. Tutalazimishwa kwenda kufanya usafi mitaani, au kulima barabara za mitaa, chini ya usimamizi wa polisi, mgambo na jeshi, huku tukipigwa mijeledi mgongoni, makalioni na vichwani.

Absolute Dictatorship. Kifupi, ule wakati wa kulima kwa meno alioahidi ndo huu sasa umewadia, msifikiri hajui anachokifanya kwa kulikimbia Jiji la Dar es Salaam na kwenda kujificha kijijini porini Dodoma. Tujiandae!

NAILILIA NCHI YANGU, NAWALILIA WANANGU😭😭😭😭
 
Barua za utambulisho zinatolewa na maofisa watendaji wa mitaa na kata, isitoshe tangu awali ukienda kwa mtendaji kufuata barua ni lazima uanzie kwa mjumbe wako wa nyumba kumi huyu ni wa ccm.
 
China ni Nchi ya pili kwa uchumi duniani wala Hakuna vyama vya upinzani

Wewe unalilia Nchi yako au unalilia tumbo lako kukosa chakula
 
Hizo akili zako za kukopa huenda unakaa kwa shemeji, tena umemaliza chuo unatafuta kazi ya uhasibu sasa unalipata joto la jiwe utaki kujiajili
 
Kusema ukweli maendeleo si vitu tu kwa binadamu, bali ni uhuru, utu, heshima na kukubali uwepo wa maoni tofauti miongoni mwa watu. Yaani kukubali kutofautiana bila kuhitilafiana, au kupingana kwa hoja bila kupigana kwa ngumi!

Mpe mtu kila kitu, lakini ukimnyima uhuru anakuwa si mtu tena - labda mnyama. Ya Tiananmen square, Hong Kong, Libya, Syria, Iran, nk.; hayataisha!
China ni Nchi ya pili kwa uchumi duniani wala Hakuna vyama vya upinzani

Wewe unalilia Nchi yako au unalilia tumbo lako kukosa chakula
 
Libya walipata nini baada ya gadafi?
Syria wamepata nn?
Iran walipata nini baada ya sadam?

The same applies to hong Kong

Don't be fulled brother,

Tusiwe wafuata mkumbo tusitumike na Mabeberu kuharibu Amani ya Nchi Yetu

Back
Top Bottom