Baada ya Zitto sasa ni Kikwete

Baada ya Zitto sasa ni Kikwete

Ukimwona samaki anaogelea kwenye beseni au kalai, ujue kawekwa humo, haiwezekani kuwa alizaliwa humo.
 
Kama rais wa nchi anaogopa kuwataja wauza unga unafkiri itakua rahisi kwa ZZK kuwataja walio ficha mabilion ya pesa nje ya nchi
 
R u serious? Coz kama amezui yasijulikane kwa miaka 7 nin kitamfanya ayatoe
 
Naunga mkono hoja!

Kikwete amkabidhi Mh Lema hayo majina ASAP! watanzania wana haki ya kufahamu ukweli. Wauza unga wanawaharibu sana vijana wetu.
Kwa hiyo ile single ya kapuya imeishaje?????????????????????????
 
Jana mbunge wa Arusha mjini mhe. Godless Lema alimtaka mbunge wa Kigoma Kazikazini mhe. Zitto Zuberi Kabwe kuwa ampatie majina ya watu walioficha mabilion nchi uswiss wakati Lema akisubilia majina kutoka kwa Zitto, gafla AG Werema aliibuka kusiko julikana na kuweka wazi kuwa zitto kwa kiapo hana majina wala account za walioficha mabilion huko uswiss.

Sasa basi ni wakati mwafaka kwa Mbunge Godbless Lema kuomba majina ya wauza unga ambao Kikwete alishawahi kusema anayo lakini leo mwaka wa saba hatujawahi kutajiwa licha ya Lukuvi nae kuthibitisha kuwa siku majina yakitajwa hakuna mbunge atakae baki salama.

Kwa kauli hiyo bungeni tumejaza wauza sembe na watimiaji wa sembe yaani madawa ya kulevya na Kikwete anawajua.

Ni wakati mwafaka sasa tutajiwe majina hayo au Werema atoe kauli kama ya jana kuwa kwa kiapo Kikwete hana majina ya wauza unga.



Asanteni naomba michango yenu.


Teh teh hii nimeipenda na nimeisambaza kwa raia wasiofika JF
 
Acha ujinga wako wewe hapa tunachotaka kutajiwa majina siyo status za watu ,manake inavyoonekana nae kama hana vile.
hivi unaweza kumfananisha rais kikwete na mtu kama lema? mkuu Crashwise ata kama unafilisika kifikra si kwa kiwango hiki,kutuletea thread za kitoto. Zitto alikuwa anahojiwa na kamati iliyochaguliwa na bunge kwa kiapo, sasa mnataka from no where rais nae afanye hivyo kwa misingi gani? tuweke itikadi pembeni tujadili mada
 
Hivi majina yakijulikana nini huwa kinafuata?. Mwakyembe alitaja wahusika wa Richmond, Slaa alitaja wahusika kwenye List of Shame..... hata hao wenye Fedha chafu Uswis wakitajwa inakuaje?

au adhabu ya Fisadi Bongo ni kutajwa hadharani?

angalau tuwajue ili wakati tunaomba tuwaweke kwenye maombi wapooze kama jaji aliyechakachua hukumu ya lema au kama lowasa..
 
Mwambieni daktari slaa awape amefunuliwa tayari si ndo mnamwita nabii wenu.
 
Mwambieni daktari slaa awape amefunuliwa tayari si ndo mnamwita nabii wenu.

Tatizo ya wapuuzi wengi kila kukicha wanamuota Dr. Slaa hata sehemu ambapo hahusiki utasikia dr slaa....mbona mnakuwa na akili za kushikiwa...
 
Naunga mkono hoja lakini ingekuwa njema zaidi kama akitoa hoja binafsi bungeni; au katika hili haiwezekani? Kwamba Mbunge anatoa hoja binafsi ya kutaka yeye apewe hayo majina ya wauza unga ili ayataje bungeni.
 
MNataka kumfanya Lema mbuzi wa kafara nyinyi apewe majina ili iweje,kamana Lema husithubutu tunakupenda kamanda hacha Zitto apewe majina ayataje yeye si ndio anapenda ujiko kuonekana ana uchungu na Taifa
 
I support the motion,hizi siasa za kutafuta umaarufu hazifai
 
Back
Top Bottom