Mungi
JF Gold Member
- Sep 23, 2010
- 16,975
- 9,580
Kuna kila dalili kwamba Mh. Lema ataomba Rais wetu mpendwa Mheshimiwa Dr. Jakaya Kikwete ampe majina ya wauza unga baada ya kusita kuyataja. Dr. Kikwete muda mrefu sana alisema tayari ana majina ya wauza unga mfukoni, lakini hadi leo hajawahi kuthubutu kuyataja.
Tunavyoona ni kwamba Mheshimiwa Rais hayupo tayari kuaibika kama alivyoaibika rafiki yake kipenzi Zitto Kabwe. Rais hatakuwa tayari kuaibishwa na AG mbele ya bunge pindi AG atakapokuwa anamjibu Mh. Lema. Ninavyofikiri na ndivyo itakavyokuwa ni kwamba AG atakuwa tayari kumjibu Mh. Lema kwamba rais yupo tayari kumkabidhi Kamanda Lema majina ya wauza unga ayataje.
Kama itakuwa hivyo basi, namuomba Mh. Lema atakapopokea list ya wauza unga, aikague list kwanza kuhakikisha jina la yule aliyekamatwa Hong Kong yupo kwenye list.