Wembe uliosahaulika tumboni kwa miaka 11 waondolewa

BANDOKITITA

JF-Expert Member
Oct 4, 2022
303
541
Ama kweli Duniani kuna mambo. Wembe uliosahaulika tumboni kwa miaka 11 watolewa.

Madaktari nchini Kenya wamemfanyia upasuaji Bi. Felister Namfua (36) na kutoa wembe wa upasuaji uliosahaulika ndani ya tumbo kwa muda wa miaka 11.

Bi Felister amekua akiishi na maumivu makali ya tumbo kwa miaka 11 akiamini kuwa ana vidonda vya tumbo (ulcers) na amekuwa akipata matibabu ya ugonjwa huo.

Tatizo hilo lilianza wiki kadhaa baada ya kujifungua mtoto wake wa kwanza katika hospitali ya Kitale Magharibi mwa Kenya.

Kadri miaka ilivyozidi kwende, aliendelea kupata maumivu makali, ndipo madaktari walipata shauku kuwa ugonjwa alionao ni mkubwa kuliko vidonda vya tumbo.

Mume wa Felister Stephen Mungai ameomba vyombo vya usalama nchini humo kuchunguza madaktari wamliofanyia upasuaji mke wake huku akidai fidia kutokana na matatizo waliomsababishia.
 
miss pablo

JF-Expert Member
Jul 9, 2018
5,106
10,184
Heh, mbona kama ndugu yangu. Namfua? Ina maana amehamia Kenya ama? Pole sana kwake
 
pwilo

JF-Expert Member
May 27, 2015
8,099
9,043
Yaani ingekuwa ulaya hapo mtu analipwa hela nyingi sana na anaaga kabisa umasikini ila huku hapo ni funika kombe mwana haramu apite

Sent from my SM-N950F using JamiiForums mobile app
 
2025DG

JF-Expert Member
Jan 30, 2023
221
529
Madaktari nchini Kenya wamemfanyia upasuaji Bi. Felister Namfua (36) na kutoa wembe wa upasuaji uliosahaulika ndani ya tumbo kwa muda wa miaka 11.

Bi Felister amekua akiishi na maumivu makali ya tumbo kwa miaka 11 akiamini kuwa ana vidonda vya tumbo (ulcers) na amekuwa akipata matibabu ya ugonjwa huo.

Tatizo hilo lilianza wiki kadhaa baada ya kujifungua mtoto wake wa kwanza katika hospitali ya Kitale Magharibi mwa Kenya.

Kadri miaka ilivyozidi kwende, aliendelea kupata maumivu makali, ndipo madaktari walipata shauku kuwa ugonjwa alionao ni mkubwa kuliko vidonda vya tumbo.

Mume wa Felister Stephen Mungai ameomba vyombo vya usalama nchini humo kuchunguza madaktari wamliofanyia upasuaji mke wake huku akidai fidia kutokana na matatizo waliomsababishia.
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom