Baada ya "Vuta Nikuvute" sasa mwili wa Mzee Ndesamburo kuagwa Uwanja wa Majengo badala ya Mashujaa

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,411
Serikali ya mkoa ikiongozwa na kaimu mkuu wa mkoa Mrisho Gambo imezuia matumizi ya uwanja wa mashujaa moshi kwa ajili ya shughuli za kuuaga mwili wa mzee Ndesamburo. Sababu walizotoa.
Mahakama na shule viko jirani.

Hata hivyo uwanja huo umekuwa ukitumika kwa ajili ya mikutano ya injili na Mchungaji Mwakasege kuanzia jumatatu hadi jumapili, Wakati hizo taasisi zikiwepo.

Ila kosa ni Chadema Kutaka kuagia mwili wa marehem Ndessamburo Katika Uwanjani huo Serikani Ijitathimini sasa...

===

UPDATES:

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika yafuatayo kuhusiana na sakata hili.

''Nimeongea na Mh Bananga aliyeko uwanja wa mashujaa , vyombo vya usalama vinazuia kuaga mwili wa Ndesamburo kuagwa hapo. Hii ni mbaya sana''


Screenshot from 2017-06-03 14-38-29.png


View attachment 518605 View attachment 518604

=======
UPDATES:

Serikali ya Hamashauri ya Manispaa ya Moshi imeruhusu matumizi ya Uwanja wa Majengo kwaajili ya Shughuli za kuuaga mwili wa Mzee Philemon Ndesamburo badala ya Uwanja wa Mashujaa kama ulivyotangazwa hapo awali.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya Serikali Uwanja wa Majengo ndio utafaa zaidi kuliko Uwanja wa Mashujaa.

WhatsApp Image 2017-06-03 at 15.37.20.jpeg
 
Embu nukuu maneno yake yote vizuri au weka kabisa barua iliyopokelewa kutoka ofisini kwake tujisomee na kuona tarehe au pia aliyasemea wapi.

Serikali ya mkoa ikiongozwa na kaimu mkuu wa mkoa Mrisho Gambo imezuia matumizi ya uwanja wa mashujaa moshi kwa ajili ya shughuli za kuuaga mwili wa mzee Ndesamburo. Sababu walizotoa.
Mahakama na shule viko jirani.
Hata hivyo uwanja huo umekuwa ukitumika kwa ajili ya mikutano ya injili na Mchungaji Mwakasege kuanzia jtatu hadi jpili hizo taasisi zikiwepo.
 
Kuna kosa lipi la mahakama na shule kuwepo jirani na eneo la kumuaga marehemu? Huu uonevu dhidi ya Chadema sasa umevuka mipaka hata kuingia kwenye kuaga waliofariki.

Halafu kuna watu humu wanataka kumfananisha huyu mwenye roho mbaya sana na Sokoine na Mwalimu!
 
Hivi, aliyekataza matumizi ya uwanja huo si yule yule aliyeelekeza pesa tuliochanga za rambirambi za Lucky Vincent zikarabati hospitali? Mbona hataki watu walioumizwa na msiba wapewe rambirambi au waage marehemu wao? Hajui kwamba kila mtu (na hata yeye) lazima anakutana na msiba, na kwamba hata yeye siku moja atakufa?
 
Back
Top Bottom