Baada ya UDOM, rungu la Ndalichako latua St. Joseph Arusha

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
joyce-ndalichako_210_120.jpg

WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha St Joseph (SJUIT) Kampasi ya Arusha (kilichofutiwa usajili), waliokuwa chini ya programu ya shahada ya miaka mitano ya ualimu wa sayansi, wametakiwa kusoma ngazi ya cheti au diploma. Kama watataka kusoma ngazi ya juu, watapaswa kuomba upya udahili.

Aidha, Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi imesema wanafunzi waliokuwa wakipata mkopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), mikopo yao pia imesimamishwa.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Simon Msanjila alitoa agizo hilo jana kupitia taaarifa kwa vyombo vya habari. Profesa Msanjila alisema hatua hiyo, inatokana na kubainika kwamba wanafunzi hao hawastahili kusoma shahada na pia hawakustahili kupewa mkopo.

“Tunawafahamisha wanafunzi wa SJUIT waliokuwa kwenye programu ya miaka mitano kwamba watatakiwa kuishia daraja la cheti na stashahada... Kama wanafunzi hao watataka kuendelea na masomo ya juu, watatakiwa kuomba upya,” ilisema taarifa hiyo.

Februari 25, mwaka huu, Wizara kupitia Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) baada ya kujiridhisha kuwa Kampasi ya Arusha ya Chuo Kikuu cha Mt. Joseph Tanzania imepoteza sifa na vigezo vya kuendelea kutoa elimu ya chuo kikuu, ilifuta kibali cha kuanzishwa kwake.

Iliidhinisha uhamisho wa wanafunzi wote, waliokuwa wanasoma katika Kampasi hiyo ya Arusha kwa gharama za Chuo Kikuu cha SJUIT. Aidha, ilifuta udahili wa wanafunzi wapya katika programu ya shahada ya miaka mitano ya ualimu wa sayansi.

Ilielekeza wanafunzi waliokuwa wakiendelea na masomo katika programu hiyo, wahamishiwe katika Kampasi ya Luguruni, Dar es Salaam. TCU ilielekeza kwamba wanafunzi watalazimika kwanza kuhitimu katika ngazi ya Stashada, kama ilivyokuwa imeidhinishwa na Tume hapo awali. Wanafunzi waliohamishiwa kwenye vyuo mbalimbali, waendelee na masomo.

Taarifa hiyo ilisema wakati wa mchakato wa uhamisho, wanafunzi wote walihakikiwa kubaini kama wanakidhi vigezo vya kusoma kwenye ngazi hiyo. Wanafunzi wote waliokuwa wakisoma programu hiyo ya miaka mitano, walihamishiwa kwenye Kampasi ya Luguruni, jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo kutokana na mchakato wa uhakiki, baadhi ya wanafunzi walikutwa hawana sifa za kujiunga na mafunzo hayo ya ualimu. Wale waliobainika kuwa na sifa, walitaarifiwa kuendelea na masomo kwenye kampasi hiyo ya Luguruni.

Wanafunzi katika kundi hili waliobainika kuwa na vigezo, walitaarifiwa kuendelea na masomo katika Kampasi ya Luguruni. Maana ya kuwa na vigezo vya ufaulu tunavyovizungumzia hapa ni kwamba wanafunzi husika wamefaulu katika masomo lengwa yanayowawezesha kusoma Cheti cha Ualimu Daraja “A” ambacho ni kigezo cha kwanza kwa mujibu wa mtaala wa programu hiyo.

Chanzo: Habari Leo
 
Hee hii sasa ni fujo, mtu kajiandaa kusoma miaka mitano ili apate degree halafu ghafla unamwambia atapata Cheti unategemea nini hapo mweeeee
 
Hee hii sasa ni fujo, mtu kajiandaa kusoma miaka mitano ili apate degree halafu ghafla unamwambia atapata Cheti unategemea nini hapo mweeeee
Wanawarudisha nyuma sana hawa madogo aisee.

Ni bora wangeangalia namna ya kusahihisha makosa yao ya kutunga sera mbovu, sio kuwaadhibu namna hii
 
Figisu figisu bado zinaendelea. Kama walishaonekana wana uwezo wa kuendelea na hayo masomo kwa nini wanataka kuwapotezea muda wa kuanza kuapply upya tena? Ni kupotezeana muda tu.

Watanzania tuna value sana uwezo wa kukariri kwa mtu na kupata elimu ya kwenye makaratasi, sijui tumelogwa...
 
Makosa hayakuwa ya hawa watoto

Makosa yalikuwa ya watunga sera, ni bora wangesitisha kuchukua maingizo mpaya wakawaacha hawa waliokuwa tayari washaanza kuendelea na elimu yao.
 
Waache kupotezea watu muda kwa sababu mwanafunzi huyo huyo ambaye anauwezo wa kusoma degree sioni logic ya kumwambia rudi nyumbani then uapply upya tena..

Ni kuwatengenezea mazingira magumu tu yasiyo na msingi kabisa. Au wanataka kutengeneza mazingira ya kupata pesa inayotelewa ya application fees. Sioni logic yoyote hapa...

Wizara iache kutengeneza mazingira ya bureaucracy kwenye kazi. Siasa wanazosema kwenye elimu ndo kama hzi sasa.

Hvi unapotengeneza mazingira magumu kwa watu kujisomea na bado unapambana kuondoa adui ujinga unategemea nini.

Me naona kama vile hii awamu hawana nia ya kweli kuondoa ujinga kwa watanzania..

Maana kama zaidi ya 7000 juzi wamefukuzwa leo wengine wenye uwezo wanaambiwa pamoja na kuwa na uwezo wa degree sii ruhusa kuendelea.. utaishia hapo hapo... Hapa pana uwalakini mkubwa sana hata mjinga atakuambia pana shida hapa...
 
Lazima elimu yetu iheshimike kwakweli hakuna habari ya mizaha kwenye elimu wakuu.
Wakati JK anaivunjia heshima elimu kwa kutunga hizo sera "mbovu" wewe ulikuwa unakata viuno hapa unamsifia. Sasa Magufuli amewachenchia huko hapa hapa unakata viuno kuwa elimu iheshimike. Nyie vijana wa CCM ni kama mapopo, haijulikani nyie ni ndege au wanyama maana mnakatika viuno tu bila kujali hii ni bolingo au reggae.

Tunataka Magufuli aweke mfumo na sio kukurupuka, hapa kuna hatari Magufuli akiondoka mwingine atakayekuja akawarudisha hawa vijana kwenye degree. Ndio maana tunataka Standard Operating Procedures SOP ili hata mwaka 2050 mtoto asome elimu ile ile. Haiwezekani kila mtawala anayeingia madarakani anakuja na utaratibu wake bila kujali kama ni mzuri au mbaya. Kipi ni kipi?
 
Mkuu, naungana na wewe katika issue ya kila Mtawala kuja na mambo anayoyajua yeye. Its very sad indeed. Wote tunakumbuka Waziri fulani wa Elimu (sote twamfaham) alivyofuta michepuo ya Ufundi na kufuta michezo mashuleni. Basi tu ni ili mradi kila mtu anakuja na anachoona yeye kinamfaa. Hatuna National Policy, bali ni Utashi tu Wa Kiongozi aliyepo kwa wakati husika. Mungu saidia akiwa na maono na fikra pevu tunasema Ahsante Mungu, kama akimislead ujue Taifa linaingia kwenye majaribu.

National Policy!!!
 
Na hili litaiuwa elimu yetu na kuizika kabisa. Kila mtu anakuja na maono yake, no collective and sustainable policy, hapa tumefeli coz akija kilaza basi kila kitu kinaharibika.

Unaondoaje michezo mashuleni?
 
Jesca yuko Udom pale anaendelea kudunda.

Na anaishi ikulu ndogo ya Chamwino, analetwa asubuhi na VX tinted la serikali chuoni, na akitoka chuo anafuatwa na VX tinted.
Na ulinzi juu,kweli kodi ya mlala hoi inatumika ipasavyo.
 
Afu
Wanawarudisha nyuma sana hawa madogo aisee.

Ni bora wangeangalia namna ya kusahihisha makosa yao ya kutunga sera mbovu, sio kuwaadhibu namna hii
Afu siku wakija kuharibu huko mbeleni naamini wewe ndio utakuja kuwa mmja wa watu watakao inyooshea serikali mkono....Ebu tujifunze kuwa watu wenye maono ya mbali si kila jambo linalofanywa na serikali ni kwa ajili ya kumkomoa mwananchi wake bali ni kwa faida yetu sote
 
Back
Top Bottom