Baada ya Sudan kutangaza uhusiano na Israel, Wananchi wapinga

Webabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
7,161
10,877
Kwa majigambo makubwa juzi raisi Donald Trump wa Marekani alitangaza kutoka ikulu ya Marekani juu ya kurudishwa kwa uhusiano baina ya Israel na taifa la Sudan.

Hata hivyo tangazo hilo limepingwa vikali na wananchi kupitia vyama vikuu vya kisiasa.Anayeongoza kupinga uhusiano huo ni Sadik El Mahdi aliyewahi kuwa waziri mkuu wa nchi hiyo ambaye kwa sasa anaongoza chama kikuu cha upinzani nchini humo cha Popular Congress Party.Kuonesha kukasirishwa kwake na tangazo hilo la serikali ya mpita Sadik El Mahdi ameacha kuhudhuria mkutano mkubwa wa viongozi wa dini uliokuwa ufanyike leo.

Katika tamko lake Sadik El Mahdi amesema urudishwaji wa uhusiano huo unapingana na sheria za nchi ya Sudan na ni kama cheche za kuanzisha vita vyengine vya wenyewe kwa wenyewe.Kiongozi mwengine wa chama hicho Kamal Omar amesema serikali ya mpito na ambayo haijachaguliwa na wananchi haina mamlaka ya kurejesha uhusiano na Israel.

Tamko kutoka chama cha FFC nalo limesema msimamo wa watu wa Sudan bado ni kuunga mkono ndugu zao wa Palestina ili warejeshewe haki zao.

Hapo Ijumaa mamia ya wananchi waliandamana kupinga tangazo la Serikali kuhusiana na tangazo la kurejeshwa uhusiano na Israel.

1603566206552.png

‘Ignition of new war:’ Sudan political parties reject Israel deal
 
Hao wasudan waachwe wasote kama wanacheza, nchi yao imekuwa kwenye vikwazo kwa muda mrefu lakini bado hawaoni.

Lini wapalestina wakawa na undugu na wanubi, hao waache uongo.
Mabwana zao wa kiarabu akina UAE, Bahrain, Jordan, Egypt, and soon Saudi Arabia tayari wana mikataba ya amani na Israel mmatumbi anajidai hafidhina kuliko waliokhitilafiana toka enzi. Ajabu sana.
 
Hii habari imekua si nzuri kwa wenzetu waarabu na wale wahafidhina wa humu jf sijui kwa nn? Israel kuwa na aman na nchi za kiarabu ni Jambo jema sana lakn waarabu waliowengi hawataki Aman kabisa na Israel , SS wakristo tunafundishwa kuwa na amani na watu wote wenzetu akina faiza f...wao ni tofauti.
Kwan jf kuna waarab umu?? Kuna washihiri na waarab wa nguruka akina manar
 
Hao wasudan waachwe wasote kama wanacheza, nchi yao imekuwa kwenye vikwazo kwa muda mrefu lakini bado hawaoni.

Lini wapalestina wakawa na undugu na wanubi, hao waache uongo.
Leo baada mafanikio ya kuimega Sudan ndio watu wanasema Sudan ni ya Wanubi lakini huko nyuma tuliambiwa Omar Albashiri ni mwarabu anaongoza serikali inayouwa waafrika.Ajabu kabisa.
Vyovyote iwavyo wasudan wengi wawe weusi au wekundu lakini ni waislamu.Na waislamu ni ndugu sana na wapalestina.Kama haitoshi hiyo hata wangekuwa ni dini tofauti basi matendo ya Israel kwa wapalestina kuwavunjia majumba yao haikubaliki kibinadamu.
 
Yuko mwanamama mzee wa siku nying humu jf subr akuje ana DNA ya kipalestina ila kazaliwa tandale kwa habr hii atakua kanuna sana,! Pole sana Bibi fa....
 
Na matendo ya hamas kurusha makombora Israel na kukimbilia kujificha msikitin nayo hayakubaliki.Kumbuka kuwa hamas ndio chanjo kikubwa Cha machafuko na hao wapalestina wahakemei hivyo vitendo viovu.
 
Hii habari imekua si nzuri kwa wenzetu waarabu na wale wahafidhina wa humu jf sijui kwa nn? Israel kuwa na aman na nchi za kiarabu ni Jambo jema sana lakn waarabu waliowengi hawataki Aman kabisa na Israel , SS wakristo tunafundishwa kuwa na amani na watu wote wenzetu akina faiza f...wao ni tofauti.
Hii habari si nzuri kwa washika dini,,haiendani na unabii,,kwa maana ingine watu walidanganywa,wamepiteza muda bure kuamini mambo ya alinacha,,hakuna Armegodon
 
Hii habari si nzuri kwa washika dini,,haiendani na unabii,,kwa maana ingine watu walidanganywa,wamepiteza muda bure kuamini mambo ya alinacha,,hakuna Armegodon
Armegodon ndo nn ? Bangi mbaya sana.Vita vya Armageddon vitakuja siku za mwisho za dunia, unabii wa biblia ni wa kweli na utatimia.Nakuhurumia sana we unayeupinga unabii.Pole sana.
 
Hii habari imekua si nzuri kwa wenzetu waarabu na wale wahafidhina wa humu jf sijui kwa nn? Israel kuwa na aman na nchi za kiarabu ni Jambo jema sana lakn waarabu waliowengi hawataki Aman kabisa na Israel , SS wakristo tunafundishwa kuwa na amani na watu wote wenzetu akina faiza f...wao ni tofauti.
... hayo.ndio matunda ya kumuulia mbali Jenerali Qasem yule mhafidhina wa Iran ambaye hakupenda kuona Israel inapatana na jirani zake.

Kama kuna kitu cha maana Trump alifanya basi ni kumuua Qasem matunda yameonekana kwa haraka sana. Muda sio mrefu hata Palestina itasanda atabaki Iran peke yake soon very soon.
 
Kuuliwa kwa general kuna connection gani na jamaa kuboresha mahusiano na israel?.
In fact waarabu wa gulf wanaona bora wasaidiane na israel kudeal na iran,maana iran inazidi kuwa region power na upande mwingine waarabu wa gulf wanahofia ottoman empire kurudi,hivyo wanataka kushirikiana na israel kujaribu kuzuia influence ua ottoman empire na persia empire,
Tena infact Endorgan anadai break yake ya mwisho atafungia jerusalem,baada ya kuungusha Aram kingdom(syria),
So israel,arab countries na greece inabidi washirikiane ku countermeasures nguvu ya Turkey kwa upande mmoja(ottoman empire) na iran(persia empire) kwa upande mwingine
 
Armegodon ndo nn ? Bangi mbaya sana.Vita vya Armageddon vitakuja siku za mwisho za dunia, unabii wa biblia ni wa kweli na utatimia.Nakuhurumia sana we unayeupinga unabii.Pole sana.
Hakuna vita ya armegodon ni uongo uliopikwa ukapikika na watu wakaamini,,utasubiri sana tu,vizazi vitakuja na kuondoka hutapata kushuhudia armegedon
 
Leo baada mafanikio ya kuimega Sudan ndio watu wanasema Sudan ni ya Wanubi lakini huko nyuma tuliambiwa Omar Albashiri ni mwarabu anaongoza serikali inayouwa waafrika.Ajabu kabisa.
Vyovyote iwavyo wasudan wengi wawe weusi au wekundu lakini ni waislamu.Na waislamu ni ndugu sana na wapalestina.Kama haitoshi hiyo hata wangekuwa ni dini tofauti basi matendo ya Israel kwa wapalestina kuwavunjia majumba yao haikubaliki kibinadamu.
Palestine kuna wakristo pia kwa taarifa yako.
 
Palestine kuna wakristo pia kwa taarifa yako.
Ni kweli na inajulikana.Lakini inashangaza mara nyingi wakristo nchi mbali mbali huwa wanawaunga mkono wayahudi wawakandamize wapalestina.Utadhani hawajui kuwa Palestina ina wakristo.
 
Back
Top Bottom