Sibonike
JF-Expert Member
- Dec 23, 2010
- 17,297
- 18,053
Kama ilivyo desturi yetu, tunakuwa na moto na kitu kilichopo kwa wakati huo. Ujio wa Obama ulitufanya tukasahau mambo mengi lakini bado yana umuhimu mkubwa. Kabla Obama hajafika tulikuwa tunajadili kauli ya Pinda bungeni kuhusu kuruhusu vyombo vya dola hasa polisi kupiga watu. Maadam Obama sasa kaondoka, turudi kwenye suala hili. kama JK alimstahi na hakuta purukushani wakati Obama anakuja, sasa wakati muafaka kumwambia Pinda aachie ngazi kwa hiari yake mwenyewe. Miaka miwili iliyobaki kumalizia ngwe ya JK, ni vizuri tukapata Waziri Mkuu mwenye ari ya kufanya kazi maana mfipa kwa kauli yake mwenyewe, amechoka. Wapo watu wengi wenye uwezo na utasi wa kufanya kazi