Baada ya Nakaaya, CCM wanamtega Lema wa Chadema Arusha? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baada ya Nakaaya, CCM wanamtega Lema wa Chadema Arusha?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by BRIA, Sep 16, 2010.

 1. B

  BRIA Senior Member

  #1
  Sep 16, 2010
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 199
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 60
  Katika hali isiyotarajiwa na inayotia shaka Mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chadema Ndugu Godbless Lema amekutwa Bar akiwa amekaa na viongozi wa andamizi wa Chama Cha Mapinduzi katika Bar ya Family Pub mjini Arusha kuanzia saa tatu usiku na kuendelea huku wakiwa wenye furaha.Ikiwa haiujulikani ni kwa vipi jambo hili limetokea wakati Mgombea wa CCM Jakaya Kikwete akiwa mjini Arusha kwa ziara rasmi ya kampeni.
  1. Maswali ya kujiuliza ni kwa vipi mwenyekiti wa CCM Ndugu Jublate Kileo awepo Bar na Mgombea wa Chadema wakati ambao mwenyekiti wa Taifa wa Chama hicho akiwa bado mjini hapa?ina maana hawana mazungumzo ya mikakati ya kulitwaa jimbo au ndo mkakati ni kumchakachua GODLESS LEMA
  2. Je kwanini wawepo mda huo mahali hapo au ndo kuthibitisha kuwa Jublate hamuungi mkono Dr Batilda Buriani kwani alikuwa kundi la Felix Mrema?
  3. Ndo kusema sasa CCM wanataka kumchakachua Godless Lema arudishe kadi na kujitoa kugombea Ubunge hapa Arusha mjini?ni muda tu utakaosema.Nategemea sana wahusika wote watatoa ufafanuzi wa kina au kama walikuwa wana mazungumzo ya kawaida nani ajuaye
   
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  Sep 16, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  That's horror!
   
 3. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #3
  Sep 16, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Siasa sio ugomvi mkuu.... inabidi mkutano mara moja moja kwenye baaa. Ila kuwa makini jamaa wasikuue kama wanaccm wa mwanza
   
 4. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #4
  Sep 16, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mkuu, mwaka huu wameshasema kuwa ushindi ni lazima. Kwa hiyo stashangaa kusikia nini kitafuata.

  Hata hivyo wakae wakijua mwiso wa siku ushindi wana wananchi wenyewe na siyo dola lenye kulazimisha mambo. Marin Hassan ni shuhuda wa jambo hili.
   
 5. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #5
  Sep 16, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Tatizo chadema mna mawazo mengi ya kilofa...
   
 6. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #6
  Sep 16, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  come on Kibs ...are u kidding me?
   
 7. K

  Keil JF-Expert Member

  #7
  Sep 17, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  ... ambayo yanafanana na wale vigogo wa CCM wa Wilaya ya Nyamagana ambao wanatuhumiana kuzungukana "kushikana miguu" kwenye swala la rufaa ya Wenje. Au wana CCM wa Mkoa wa Kigoma ambao wanapeana barua za uhamisho saa sita usiku utadhani wanga/wachawi!

  Wakati wa Uchaguzi kila mtu ana-watch back ya mwenzake ili kuepuka backstabbing. CHADEMA wakitiliana mashaka inakuwa mawazo ya kilofa, CCM wakituhumiana ni mawazo na msimamo makini .... kaazi kweli kweli.
   
 8. P

  PapoKwaPapo JF-Expert Member

  #8
  Sep 17, 2010
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  waache waende tu...kwani nishaona sisiem haiwezi n'goka madarakani, tunahitaji dikteta mmoja hapa ndio tutakuwa na adabu
   
 9. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #9
  Sep 17, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Acha matusi ya kiCCM wewe ni vuvuzela tu! lol
   
 10. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #10
  Sep 17, 2010
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,848
  Likes Received: 2,423
  Trophy Points: 280

  starehe haina siasa...ndio maana Jakaya ...pamoja na upinzani na mbowe majukwaani ....walikuwa wakikutana pamoja kwenye starehe.....na huko nyuma ...Jakaya alikuwa ni mmoja wa wahudhuriaji wazuri kwenye Club ya billicanas.....

  Ni muhimu ikaeleweka kuwa siasa haiwezi kutuzuia kukaa baa pamoja naa kuzungushiana raundi za bia kama ilivyo utamaduni wetu watanzanania .....mkifuatilia mtagundua kuwa kuna wagombea wengi tu wa CCM wanakunywa na wapinzani ie CHADEMA....na hata wale wavutaji wa sigara wanaendelea kugongeana ....na wale wakware wanaendelea kutongozana ...maisha yanaendelea.......

  Sioni ajabu kwenye hili.....ningeshangaa kama walikuwa wananywea pombe chumbani.....maana ingemaanisha walikuwa wana ongea siri.....lakini BAR is a public place....na watu wa Arusha kukesha bar ni kawaida yao.....
   
 11. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #11
  Sep 17, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Ni kweli lia inawezekana timing ya hicho walichokifanya (ambacho inawezekana ni kawaida kunywa pamoja) ikawa ndo mgogoro unaosababisha huu mjadala. Pia ukizingatia kwamba kwa sasa watu wanawindana!
   
 12. K

  Keil JF-Expert Member

  #12
  Sep 17, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Dark City nakubaliana na wewe ... CCM sasa hivi wako desperate, hasa kwenye mikoa ambayo wanaona wazi kwamba wana hati hati ya kushinda. Wanaweza kufanya chochote kile ili kupunguza nguvu ya upinzani.

  CCM wao wenyewe wametuhumiana kule kwa Mrema, kwamba Mzee Kimaro anamsaidia Mrema (Lyatonga) ili ashinde. Hiki kipindi cha uchaguzi ni ku-doubt kila unapoona kuna nyendo zisizo za kawaida.

  Bado CCM hao hao si ajabu wakaja na doubt nyingine kwamba inawezekana huyo mwenyekiti wao wa CCM mkoa (Kileo) kwa kuwa mtu wake hakupita kwenye kura za maoni may be anataka kumhujumu Buriani.

  Hivi kweli Mwenyekiti wa CCM Taifa na pia mgombea Urais yuko mkoani kwako na ameingia Arusha mjini saa 12 jioni, unaweza kuwa na nafasi ya kuongea na mgombea wa chama kingine badala ya kumpa briefing Mwenyekiti na Mgombea Urais mwenendo mzima wa Kampeni mkoani kwako? Hapa kuna kiwingu cha kutosha kuleta maswali.
   
 13. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #13
  Sep 17, 2010
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,423
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Inauma lakini usikate tamaa! Jemadari siku zote mbele kwa mbele! Ila nafikiri kwa faida ya taifa letu, na kwa ajili ya kulinda amani tuliyorithishwa na Mwl, na kwa kuwa tunapendana wote licha ya itikadi au ushabiki wa vyama(maana sijui itikadi ya chama hata kimoja siku hizi), tuliowapa kazi ya kuhakikisha mambo haya ya kipuuzi hayatendeki, wanapaswa waamke waliko lala. Sioni kwa nini Takukuru wasimhoji Nakaaya, simply mbona umehama, umepewa chochote atasema hapana, anaachiwa, na wengine wafahamu kwamba wapo! TAKUKURU wanahoji watu wengi sana hata bila sabau ya msingi, kwa hili la siasa ambalo ni hatari na linaweza likaleta machafuzi wanakaa kimyaaaaaaaaaaaaaaaMungu aepushe mbali.
   
 14. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #14
  Sep 17, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,067
  Likes Received: 1,805
  Trophy Points: 280
  Mushampoteza huyu!... :becky:
   
 15. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #15
  Sep 17, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Vituko vya Zenj tumeviona mzee !!
   
 16. K

  Keil JF-Expert Member

  #16
  Sep 17, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Wagombea ubunge wa CUF ndio makini? Yule mgombea wa Lindi ambaye hakurudisha fomu mpaka Prof. Lipumba akaomba msaada ya TAKUKURU ili wamhoji, yeye alikuwa makini sana?

  Umamluki uko kila chama, hata CCM kwenyewe kuna Mamluki. Hoja hapa ni msimamo wa mhusika na malengo ya mhusika. Wengine wanaingia kwenye chama kwa ajili ya malengo fulani na asipofanikiwa then anaamua kuondoka.

  Tambwe Hizza alitesa sana mitaa ya Temeke akiwa na CUF na alikuwa tishio kwa CCM, Makamba akamhamisha na kumpa kazi pamoja na yule Mzenji [nimesahau jina lake] ndo wamepewa kitengo cha propaganda. Siku Makamba akiondoka kwenye Ukatibu Mkuu, jua kwamba Tambwe na huyo Mzenji wanaweza kuwa njia moja kuhama CCM, maana wako Lumumba kwa huruma ya Makamba. Tambwe kajaribu kugombea chaguzi za ndani amekosa.

  Kuna Mama mmoja kutoka Kanda ya Ziwa alikuwa ni Mbunge wa Viti Maalum [CUF] wa bunge hili linalomaliza muda wake sasa, siku Bunge lilipovunjwa alikwenda kurudisha kadi ya CUF kwa JK na kuchukua ya CCM. Teddy Kasela-Bantu alikuwa mbunge wa CUF viti maalum na tena alikuwa kiongozi huko kwao Tabora. Bunge la 2000 - 2005 lilipovunjwa na yeye akatimkia CCM na kwenda kugombea kwao Bukene. Hujiulizi ilikuwaje akashinda kwanza kwenye kura za maoni na baadaye uchaguzi mkuu, ni kwamba akiwa Mbunge na Kiongozi wa CUF alikuwa aki-double kama kada wa CCM na kuweka mambo yake sawa huko alikokuwa anataka kugombea. Naila Jidawi aliingia kwenye mgogoro mkubwa sana CUF mpaka wakamfukuza na kupelekana mahakamani, serikali ya CCM ikamtetea na akaendelea kupata mafungu yake kama kawaida na mahakama bado ikasema ni mbunge halali wa CUF ingawa chama kilikuwa kimemkana.

  Tufike mahali tukubali tu kwamba katika hivi vyama iwe ni CCM, CUF, CHADEMA, TLP, NCCR au chama chochote kile, waganga njaa wako wengi. Akikosa maslahi/anachotafuta atahamia chama kingine.

  Dr. Limbu aliporudi Tanzania alikuta moto wa mageuzi unawaka. Mwaka 1995 baadhi ya wana CCM jimbo la Magu walimuomba agombee akagoma, akasema upepo unavuma kuelekea NCCR. Jamaa alijitosa kupitia NCCR akaambulia vumbi. Baada ya uchaguzi bahati mbaya Mbunge wa Magu akafariki, Dr. Limbu alirudi CCM kwa kasi kubwa, akateuliwa apeperushe bendera ya CCM kwenye uchaguzi mdogo. Aliangushwa Bwana Mapesa (John Cheyo). Mwaka 2000 alipojaribu tena ndio akapita. Hao ndio wana siasa wetu.

  Umamluki, uganga njaa, uhovyo na mengineyo hayako CHADEMA pekee, kila chama kina watu wa namna hiyo, inategemeana na jinsi unavyowa-define.

  Rais wa Malawi aliweka rekodi ya kujivua uanachama wa Chama kilichompeleka Ikulu na akaanzisha chama chake kipya na mpaka leo hii bado anapeta na hicho chama kipya. Kwenye siasa kuna mambo mengi sana.
   
 17. m

  mozze Senior Member

  #17
  Sep 17, 2010
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 185
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa nini hatufikirii huyu LEMA alikuwa anapata siri za CCM ili azidi kuwazima? Sio kila mtu hana msimamo. Nakaaya alikuwa na madaraka gani? Alikuwa na Influence gani? Si amejiunga Chadema ingali ni Imara? kwa yeye ndiye aliyeanzisha Chadema?
  Tusikuze mambo, Nakaaya ni mwanachama kama wengine, mwache aende kwani kura wanapiga wananchi!
   
 18. B

  BRIA Senior Member

  #18
  Sep 17, 2010
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 199
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 60
  Hukusoma original post vizuri bro ngoja nikuwekee tena Soma uelewe?
  Katika hali isiyotarajiwa na inayotia shaka Mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chadema Ndugu Godbless Lema amekutwa Bar akiwa amekaa na viongozi wa andamizi wa Chama Cha Mapinduzi katika Bar ya Family Pub mjini Arusha kuanzia saa tatu usiku na kuendelea huku wakiwa wenye furaha.Ikiwa haiujulikani ni kwa vipi jambo hili limetokea wakati Mgombea wa CCM Jakaya Kikwete akiwa mjini Arusha kwa ziara rasmi ya kampeni.
  1. Maswali ya kujiuliza ni kwa vipi mwenyekiti wa CCM Ndugu Jublate Kileo awepo Bar na Mgombea wa Chadema wakati ambao mwenyekiti wa Taifa wa Chama hicho akiwa bado mjini hapa?
  2. Je kwanini wawepo mda huo mahali hapo au ndo kuthibitisha kuwa Jublate hamuungi mkono Dr Batilda Buriani kwani alikuwa kundi la Felix Mrema?
  3. ndo kusema sasa CCM wanataka kumchakachua Godless Lema arudishe kadi na kujitoa kugombea Ubunge hapa Arusha mjini?ni muda tu utakaosema au ndo walikuwa kwenye mazungumzo ya kawaida tu..
   
 19. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #19
  Sep 17, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160


  wengi wetu tunaoshabikia chadema, nia yetu ni kutafuta uhuru wa kweli wa kujumuika, kutoa maoni, haki ya kweli ya kujiunga (freedom of association, speech and the right to organise) kwani vitu hivi ni ingriedients muhimu sana kwa ujenzi wa maisha bora kwa kila mtu. Hivyo wapiganaji mbali mbali tunatumia forum ya chadema ambapo kuna like minded people kwa kuwa tunategemea kupata mafanikio ya marekebisho ya katiba haraka iwezekanavyo.

  Hata mkoloni mwingereza aliruhusu kuwepo kwa
  uhuru wa kweli wa kujumuika, kutoa maoni, haki ya kweli ya kujiunga (freedom of association, speech and the right to organise) kwa waafrika ndio maana kukawepo vyama vya wafanyakazi na vyama vya ushiriki vyenye nguvu kama vile tfl, kncu, kcu, n.k.

  Kutokana na kuwepo kwa
  uhuru wa kweli wa kujumuika, kutoa maoni, haki ya kweli ya kujiunga (freedom of association, speech and the right to organise) mwalimu nyerere alivitumia vyama hivyo kudai uhuru wa tanganyika hadi ukapatikana mwaka 1961.

  Lakini kwa bahati mbaya sana kutokana na kuogopa challenge mwalimu nyerere, na radiclas ndani ya tanu wakafuta uhuru wa kweli wa kujumuika, kutoa maoni, haki ya kweli ya kujiunga, kwa kufanya yafutayo:-
  1)mwaka 1964 wakakufuta tanganyika federation of labour (tfl) iliyokuwa mstari wa mbele kudai uhuru hadi kupatikana na badala yake wakaunda nuta, ambayo mwenyekiti wake alikuwa akiteuliwa na rais.
  2) mwaka 1965 wakafuta mfumo wa vyama vingi vya siasa na kuanzisha ukiritimba wa siasa za chama kimoja-tanu pekee
  3)mwaka 1976 wakafuta vyama vya ushirika vya wakulima na kuunda bodi za mazao. Hatimaye 1981 wakarejesha vyama vya ushirika vya kiserikali hadi leo hii.

  Kwa vitendo vyao mwalimu nyerere , tanu na ccm walimuondoa mkoloni mzungu na wao kugeuka wakoloni waafrika. Ndio maana tanzania ya leo inahitaji ukombozi wa pili ambao utahusisha kuwakmboa watanzania kifikra.

  Hivyo katika misingi ya uhuru wa kweli wa kujumuika, kutoa maoni, haki ya kweli ya kujiunga na bila kuingilia haki zake kama binadamu ndg godless lema yuko huru kukutana na mtu yoyote, wakati wowote na mahali popote.

  Tukumbuke hatukupigania kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa ili kujenga uadui au uhasama baina yetu wenyewe. Aidha ikumbukwe kuwa wagombea wa vyama mbali mbali ni wakazi wa eneo, jimbo husika na pengine kabla ya mwaka wa uchaguzi mkuu walikuwa na mahusiano ya kindugu, kikazi, kibiashara n.k

  kwa mtizamo wa bria, na wengine wenye mawazo kama yako, upo uwezekanao wa chadema kurithishwa silka, tabia na hulka za kiccm za kubana uhuru wa kweli waananchi kujumuika, kutoa maoni, haki ya kweli ya kujiunga (freedom of association, speech and the right to organise).

  Nimelazimka kutoa ufafanuzi huu ili kuweka records sawa ili mgombe wetu ndg godless lema ahukumiwe kwa vitendo vyake katika mchakato wa uchaguzi mkuu wa 2010 kama mwakilishi wa chadema na si vinginevyo hususan anapokuwa akitumia uhuru wake binafsi. Sipingi kuwa upo uwezekano wa hofu aliyo nayo bria kutokea lakini kuanza kujadili mabo hayo mapema kisa hiki ni kumvunjia heshima mgombea wetu.
   
 20. B

  BRIA Senior Member

  #20
  Sep 17, 2010
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 199
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 60
  Watu wanahoji timing na kundi lilikuwa limemzunguka kaka?ndo mana nimetoa hili kama angalizo soma text vizuri?Mwanajeshi anapokuwa vitani kuna tofauti ya Uhuru ambao anakuwa nao tofauti na kipindi anapokuwa Uraiani?Unafanya nini Bar na kundi la wafanyabiashara na wanachama wa CCM meza moja mda huu wa kazi?na mimi angalizo langu ni kwa CHADEMA NA CCM kwa pamoja..Nimezungumzia watu wawili mwenyekiti wa CCM na wa MGOMBEA..Namwamini sana Lema...ila ajirekebishe
   
Loading...