Elections 2015 Baada ya Masheikh wa Bagamoyo, Wachungaji wamzamia Edward Lowassa kumuomba kugombea Urais

attachment.php


Najisikia aibu kuitwa mkristo kama viongozi wenyewe ndio hawa ?.

Soma kibao cha mchugaji wako kimeandikwa SENGE REMA.
 
Waumini Wanatoa Sadaka Zao Kwa Shida Huku Wakijifunga Mkwiji Wao Wanazitumbua Tu Kwa Kujipendekeza. Kumbe Sikukosea Kuacha Kusali Huko Makanisani Na Kuamua Tu Kugeukia Kusali Kwa Miungu Yangu Ya Kizanaki / Kitutsi Na Kiyao Kwani Hainiombi Sadaka Na Inanibariki Kuliko Hata Huko Kwa Hao Wanafiki.
YESU ndiye mchungaji MWEMA yeyote amfuataye hatapotea kamwe.

Kama wewe unawafuata watu na sio NENO la MUNGU hata huko gizani napo kuna uongozi unaoratibiwa na wanadamu kama walio kwenye makanisa.
 
Kwakuwa hofu ya Wasiompenda lowasa ipo katika kuibuliwa kilichojili katika Richmond na kunyang'anywa kwa mali za watoto wao zilizopatikana kwa hila, njama ufisadi na ulaghai basi Wacha Lowasa aje muumbuane!
 
Wanaomuunga mkono Lowasa wanaonesha hili kwa vitenda kwa kuandamana kwenda nyumbani kwake hadharani. Hivi wale wasiomkubali Lowasa nao si waandamane kwenda nyumbani kwake kumpinga hadharani wasikike?
 
y January Makamba Nafasi ya Urais ni nafasi ya hadhi na heshima kubwa. Unapoiomba hupaswi kufanya michezo ya kuigiza. Huu utaratibu wa kuratibu watu, kuwasafirisha, kuwapa posho na ubwabwa waje kukuomba kugombea ni michezo ya kuigiza ambayo ni aibu kubwa.

Kila mgombea ana uwezo wa kutengeneza WATU wa kumuomba kugombea lakini wengine hatufanyi hivi kwasababu tunaheshimu nafasi tunayoiomba na tunaamini kwamba haipaswi kutafutwa kwa ulaghai na maigizo.

Ni aibu sana kutumia shida na njaa za watu kisiasa. Ni aibu sana kukusanya vijana na wazee wa watu na kuwapangia viti na mahema na kuwapa pesa halafu pesa na kuwapiga picha. Ukiona mtu anatafuta nafasi ya uongozi kwa ujanja na ulaghai ujue atatawala kwa ujanja na ulaghai.

Viongozi wanaokubalika na watu hawangaiki kupanga Viti na mahema na kuwapiga picha watu wanaowakubali.

Mgombea anayehaha na kutumia pesa nyingi kuonyesha anakubalika ukweli ni kwamba hajiamini. Kama unakubalika huwezi kuratibu makundi na kuyalipa na kuwapiga picha na kuita waandishi wa habari waje kushuhudia. Hizo ni mbinu za mfa maji.

Naamini Chama changu hakitatishwa na nguvu za maigizo. Tunataka uongozi safi unaomuogopa mungu. Tunataka uongozi wenye uadilifu na fikra mpya za kuisogeza mbele Tanzania. Tunataka viongozi watakaomaliza shida za Watanzania sio wanaozitumia shida hizo kisiasa.

Hata Mzee Makamba, pamoja na umri wake wa miaka 75, leo akiwa na pesa za kumwaga anaweza kutengeneza makundi yakamuombe kugombea Urais.

Ifike mahali katika nchi yetu tuache hii michezo. Tukiendelea na mambo haya, tunatengeneza taifa linaloendeshwa kwa propaganda tu. Watu wanaotaka kuomba nafasi ya Urais wanapaswa kuwa na ujasiri na wanapaswa kujiamini na kusema wanataka nafasi hiyo na wana fikra gani mpya bila kutumia pesa kuonyesha kwamba wanagombea kwasababu wanahitajika na watu. Uongozi thabiti na shupavu hautokani na michezo ya kuigiza.

January Makamba


Acha wivu, we nani kakuambia anaratibu watu? Wivu mwingine hauna maana.
 
Njaa hii itawamaliza. Serikali itunge sheria ya kuanzisha bodi ya wachungaji itakayofanya kazi ya kusajili wachungaji ili kama ni feki wafutwe. Hii itasaidia kuthibiti wachungaji uchwara kama ilivyo bodi ya makandarasi. Tuendako sasa ni kubaya. Kila mwenye kijikanisa uchochoroni atasema ameoteshwa na Mungu juu ya Lowassa kuwa rais
 
Ni huyu msemaji wa Wachungaji wa Pentekosti walioenda dodoma nyumbani kwa el kumrecharge aongeze nguvu za kugombea urais.

Kulikuwa na sababu gani yeye kama kiongozi wa dini kusema mh huyu ni waziri mkuu mstaafu badala ya waziri mkuu mjiuzulu (pm emaritus).?

Kachangiwa sadaka kutoka madhabahuni kwa Bwana aende kusema uongo? Bwana Yesu alishatuasa katika maandiko matakatifu Wachungaji wa mishahara na manabii wa uongo tuwe macho kipindi hiki.
 
Rumors are carried by haters, spread by fools, and accepted by ------.' Good morning Lowasa's ------ haters
 
utendaji wa serikali yetu umekuwa ni maigizo kwa miaka 10, sasa ndo tuje kushangaa maigizo wakati wa kampeni?
Huyo makamba naye upeo wake ni wa kuboreshwa.
 
Rumors are carried by haters, spread by fools, and accepted by ------.' Good morning Lowasa's ------ haters

Mungu aliwapenda akawaumba tofauti na hayawani lakini mmejivua ufahamu na kujivika uhayawani. Kusema mchugaji, kasema uongo hadharani na anapaswa kwenda kutubu ni kuwa na chuki na mtu?
 
Lowasa anafanya propaganda za kitoto. zaidi anawadhalilisha hao wanaojiita wapentekoste na mashehe uchwara.
 
y January Makamba Nafasi ya Urais ni nafasi ya hadhi na heshima kubwa. Unapoiomba hupaswi kufanya michezo ya kuigiza. Huu utaratibu wa kuratibu watu, kuwasafirisha, kuwapa posho na ubwabwa waje kukuomba kugombea ni michezo ya kuigiza ambayo ni aibu kubwa.
January Makamba

January makamba aache kubwabwaja, huu uhuni unaofanywa na Lowassa ndiyo uliofanywa na Kikwete, ukiratibiwa na January Makamba mwenyewe. Anatia kichefuchefu anapokaa chini na kuiponda mbinu inayotumiwa na mwenzake, huku akijua kwamba alifanya hivyo pia kumpitisha Kikwete.
 
Ni huyu msemaji wa Wachungaji wa Pentekosti walioenda dodoma nyumbani kwa el kumrecharge aongeze nguvu za kugombea urais.

Kulikuwa na sababu gani yeye kama kiongozi wa dini kusema mh huyu ni waziri mkuu msaafu badala ya waziri mkuu mjiuzulu (pm emaritus).?

Kachangiwa sadaka kutoka madhabahuni kwa Bwana aende kusema uongo? Bwana Yesu alishatuasa katika maandiko matakatifu Wachungaji wa mishahara na manabii wa uongo tuwe macho kipindi hiki.
Ndo umeamdika nini sasa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom