Msajiri, polisi na mahakama ndio wanazidisha provocation kwa watu.
Sioni dhamira ya kufikia mwafaka wa kitaifa.....Huwezi kuendelelea na maisha yaleyale ya kamatakamata, kesi, fungiafungia halafu utegemee uje ufanye maridhiano na watu walewale.
Halafu mambo mengine mbona ni negligible tu...
Kuna like limwanamke la korogwe juzi limezungumza kauli ya ovyo sana, lakini busara ilitumika, kauli ile ikapuuzwa tu, maisha mengine yakaendelea.
Ndio siasa......lakini busara hizohizo msajiri hazitumii kwa vyama vingine.
Sasa matokeo yake ndio yalee, watu kusherekea tanzia za viongozi, na itafika mahali hatutazikana....
Itafika mahali haitaishia hapo, uhasama utakwenda mbali zaidi.
Kuna wakati watumishi wa TRA walipata ajari ya gari Singida, lakini kilichotokea ni watu raia wake kawaida walifurahia vifo vile.