Julius Kambarage Nyerere muafrika pekee aliyewatetemesha mataifa ya Ulaya na Marekani,aisaida China kuwa mwanachama


britanicca

britanicca

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2015
Messages
8,882
Likes
12,838
Points
280
britanicca

britanicca

JF-Expert Member
Joined May 20, 2015
8,882 12,838 280
Julius Kambarage Nyerere alikuwa kiongozi wa Kitanzania alieiongoza Tanzania, na kabla ya hapo Tanganyika, kuanzia 1960 hadi alipostafu mwaka 1985. Anatambuliwa kuwa ndiye Baba wa Taifa.

Julius Nyerere ni Waziri mkuu wa Kwanza wa Tanganyika na Baadae Rais wa kwanza wa Tanganyika baadae iliyo badilika na kuitwa Tanzania,Jina lake kwa kirusi linaandikwa
Джулиус Ньерере
Wakati wa kupigania Uhuru Nyerere aliongoza mapinduzi mengi barani Africa na ameendelea kukumbukwa kwa ilo, na akaongoza kukataa ubaguzi wa rangi maeneo mbali mbali afrika na duniani kote,

Nyerere katika ujamaa wake na falsafa ya kikomunia au kikomunist aliweza kuwa na ushawishi mkubwa kwa warusi na wachina , uku marekani baada ya kuwashawishi wakoloni kuachia soko la africa waingie wakakutana na mkono wa Джулиус Ньерере
ambaye alikuwa na ushawishi wa hali ya juu sana, Kila walipofikilia kuja africa walimfikiria mwalimu Nyerere atakavyowashawishi wengine kukataa hoja,

Lakini mwaka 1964 Rais wa Marekani aliona ni vema kukutana na mwalimu Джулиус Ньерере
kuzungumzia suala ili la jinsi gani amerika awekeze afrika na kuweza kutimiza maelngo yao, lakini Nyerere aliwakatalia akasema kwamba haitawezekana yeye kuweza kukubali ubepali na ukoloni mamboleo,
Urusi baada ya kusikia hivyo ikatoa nafasi za watanzania kujifunza nchini uko ujamaa na wengine kuwa maspy, nadhani kina luis shika wanaelewa hapa
lengo likiwa kuwashawish zaid Tanzania kuwa upande wa USSR kuliko USA, baada ya mwalimu Nyerere kujua kwamba kumbe yeye ni muhimu akawachezesha ngoma kwamba afungamani na upande wowote,

Miaka kadhaa baadae Wachina likiwa Taifa dogo kiuchumi lakini linaloonekana kukua kwa kasi lilikataliwa kuwa na nafasi ya kudumu ndani ya Baraza la umoja wa mataifa, Rais wa china akajua kwamba marekani ndo kilanja mkuu wa mambo hayo, na marekani kwa Tanzania alikuwa akilegea sana maana alijua soko lake la africa linategemea sana msimamo wa mwalimu Nyerere wa Tanzania, ikabidi urafiki wa china na Tanzania uimarishwe

CHINA YAOMBA MSAADA KWA TANZANIA

Rais wa China alishika safari na kuja mjini mzizima(Dar es salaam) kukutana na mwalimu nyerere na kufanya mazungumzo kadhaa ambayo Nyerere aliyakubali ila kwa masharti kadhaa,
Mwaka 1965 mwezi wa pili Nyerere alitembelea beijing na hakutaka kuongelea suala la reli ya TAZARA japo alijua kuwa ni muhimu kama wanavyolizungumza na Kaunda kila wakati,na sababu iliyopelekea Nyerere kusita kuliongelea ni kwasababu China pia ilikuwa ni nchi masikini kwa wakati ule. Lakini Pamoja na kwamba China ilikuwa masikini waliona kitu ambacho Dr.Nyerere angewasaidia na kuwakwamua kwa mbeleni na rais Liu Shaoqi akafanya mazungumzo ya nisaidie nikusaidie baina yake na mgeni wake toka Tanzania yaan Mwalimu, na yeye akasema kumsaidia kujenga reli ya Tazara Naye mwenyekiti wa chama Mao Zedong akamwambia Nyerere, “You have difficulties as do we, but our difficulties are different. To help you build the railway, we are willing to forsake building railways for ourselves.also we need your help in another way” akimaanisha unamatatizo kama sisi tulivyo na matatizo japo yanatofautiana, hivyo basi tunakuhakikishia kama makubaliano yataenda sawa tutatimiza ili,
china ikahakikishia Tanzania kwamba endapo watakubali kuwasaidia katika kushawishi kujiunga na Bazraza la usalama la Umoja wa Mataifa wao pia watakamilisha ujenzi huo kabla ya mwezi oktoba 1966.
nje ya ilo mwalimu Nyerere aliona kama kazi ngumu mno kuwaingilia magabacholi wa marekani , ila akajitahidi na akawaomba china pia wafanye haya
1.China ijenge miundombinu ndani ya Taifa changa la Tanzania kama vile reli na barabara
2.Iwape Tanzania mbinu za kiufundi hata kuwasaidia kusomesha watoto au wanafunzi ndani na nje ya Tanzania
3.Iwekeze zaidi katika viwanda na kujenga viwanda vipya
4.Uwepo ushirikianoa katika mafunzo juu ya ukomunist na ujamaa baina ya vyama tawala,

Matunda yake yalikuwa kama ifuatavyo
1.Vilijengwa viwanda kadhaa kama ufariki Textile na vingine
2.China haikopeshi Tanzania hata siku moja kwa riba kubwa
3.Reli ya TAZARA kwa upande wa Tanzania imejengwa kama zawadi kutoka china kutokana na juhudi za mwalimu Nyerere,
4.Kikaimarishwa chuo cha mafunzo ya siasa Kivukoni kwa sasa kinaitwa Mwalimu Nyerere Memorial academy
5. Nafasi za kusomea china kwa watanzania zikaruhusiwa zaidi.
6.Baadhi ya sehemu za china watanzania wanenda bila visa, Kama Macau, Hongkong.
7.Miradi mingine ya barabara ilijengwa.


SAFARI YA NYERERE ULAYA NA NCHINI MAREKANI NA MAZUNGUMZO JUU YA CHINA

Kama mwanzoni inavyoeleza china alisaka sana uhusiano wa kidiplomasia na umoja wa mataifa , pia Nyerere alikuwa aingiliki na saa nyingine wanadhani alivyomwana falsafa akikaa chini atayakataa waliyokubaliana kule China na saa nyingine kuhisi China wanaweza wasitimize lengo,
lakin waziri wa biashara kutoka zanzibar bwana Abdulrahman Mohamed Babu na mawaziri wengine waliongeza ushawishi mkubwa sana ili China isisitishe mpango huo na pia kuendelea kumsihi mwalimu Nyerere akubaliane nao kwa haraka kutekeleza mpango huu, Mwaka 1965 Katika mkutano wa mawaziri wakuu wa Jumuiya ya madola maarufu kama Commonwealth prime minister's conference, waziri mkuu wa uingereza wa muda huo Bwana Harold Wilson alichanganyikiwa baada ya kuona uhusiano wa Tanzania na China umekuwa mkubwa mpaka baadhi ya mawaziri wa baraza la Nyerere wako "directly in the Chinese pay."
Pia uhusiano huu ulimchanganya waziri mkuu wa Canada Lester Pearson na kuuliza kama Nyerere ataendeleza ukaribu na wachina au wakomeshe misaada toka Canada Nyerere alisema msimamo wake uko pale pale na baadae akalalamika kwa hotuba iliyotikisa mkutano wa Umoja wa mataifa akishutumu Nchi za magharibi kuwanyanyasa China na Kuwanyima haki ya kuwa katika baraza la usalama la umoja wa mataifa.

NYERERE AWEKA MGOMO NA KUSIMAMA NDANI YA MKUTANO KAMA WANAYOFANYA UKAWA
Baada ya kuona anayoyadai yana msingi na hawaoneshi hata chembe ya kumkubalia mwalimu Na akaendela na kutishia kujitoa kwenye jumuiya ya madola maana walionekana kumkazia china asijenge ile reli maana kuna uhusiano uligundulika kwamba ndo wanapinga ujenzi wa reli, na akasema kama wanapinga ujenzi wa reli kufanywa na China mbona hawaweki njia mbadala ya kujenga reli hiyo?
pia Nyerere alikasirika na kutamka maneno haya kwa kingereza na kusimama uku mataifa mengine wafuasi wakiwemo , Zambia, Ghana, Uganda,Kenya, Siela leone,Rwanda,Costa Rica, Peru, China, Russia,Sweden, na Mataifa mengine mengi, Nyerere alisema maneno haya akiwa amesimama kwenye mkutano huo ambao aliomba kuhutubia umoja huo akakataa kabisa kukaaa na wenzake wakasimama,
"... all the money in this world is either Red or Blue. I do not have my own Green money, so where can I get some from? I am not taking a cold war position. All I want is money to build it."
— Julius Nyerere, PRO, DO183/730, to CRO, No. 1089, 3 July 1965.

akimaanisha hela yote duniani ni ama nyekundua au bluu, sina hela yangu ya kijani, sasa nipate wapi hela ? hapa siungania au sifanyi hivi kwasababu ya vita baridi yenu na USSR ninachotaka ni hela ya kujenga reli ndo maana nikamuomba china.

MKUTANO WA HAIRISHWA BAADA YA NYERERE KUCHOCHEA MGOMO NA KUSHAWISHI MATAIFA TAKRIBAN 40

Baada ya Nyerere kusimama mda mrefu bila kutaka kukaa uku akiwahamasisha wengine ilibidi mkutano uhairishwe mpaka siku nyingine ambayo ilizaa matunda, na ulikuwepo mkutano wa watu mataifa manne kabla ya mkutano mkuu
1.USA
2.CHINA
3.TANZANIA
4.UINGEREZA
mkutano au kikao hicho kililenga kujua nini uhusiano wa China na Tanzania na kwanini hasa , na walioendesha mkutano huo walikuwa wamarekani na waingereza,
Nyerere alisema maneno yale yale na kuyarudia mara kadhaa , na baadaye waziri wa uingereza akaomba kuongea kwa kina na Nyerere wakiwa wawili, ndipo Nyerere akaweka mapendekezo yake kwamba Marekani ama amuachie China ajiunge Umoja wa mataifa na kuwa na kura ya Veto ama atafte wa kufanya nao biashara wengine si africa wala mashariki ya mbali,

OMBI LA NYERERE LAKUBALIWA KWA MASHARTI
Ombi ilo lilikubaliwa kwa masharti yafuatayo
1.China atapewa nafasi ila Nyerere asiendeleze vikao na wanachama wajumuiya ya madola kutoka Africa au wakikutana basi wasiwe wao awepo mtu atakayejua wanazungumza nini,
2.China ajenge reli ile lakin hela akope kwenye chanzo watakachompangia wao na kwa riba wanayotaka wao,
3.China asiwe na mahusiano ya Moja kwa moja na USSR bila kuhusisha wamarekani
4.Nyerere akubaliane na falsafa ya ukoloni mamboleo na mabepali,

NYERERE AKUBALI MASHARTI KWA UJANJA NA KUTOYATEKELEZA -AIBUKA IDI AMINI PANDIKIZI LA MABEPALI

1.Hakuna asiyejua kwamba Nyerere aliendeleza vikoa vyake na watu aliokatazwa na pili urafiki wake na USSR ndo akauimarisha vema

2.ukaanza mpango wa urani/Uranium One Inc.,mmoja kati ya miradi mikubwa duniani ambao ni wazalishaji wazuri pia ,mradi huu unamilikiwa na ROSATOM State Atomic Energy Corporation, unaofanya uzalishaji katika mradi wa mto Mkuju(Mkuju River Project), uko kusini mwa Tanzania,takribani km 470 km kusini magharibi mwa jiji la Dar es Salaam.

3. Kiwanda cha ndege cha urusi Russian aircraft manufacturer, Irkut Corporation, kikasaini makubaliano ya kuwapatia Air Tanzania Company Limited (ATCL) vifaa na zana za ndege za MS-21.

makubaliano hayo yalitekelezwa na mengine yakatekelezwa na viongozi waliofuata,

Baada ya kuona Nyerere amekuwa mkaidi na ameendelea kuujenga umoja wa Afrika mashariki wakaamua kumuundia zengwe , kwanza kuuharibu umoja huo kwa kuweka pandikizi Iddi Amini na kuvuruga,
Pili kuanzisha uchokozi ambao amini aliuanza mwaka 1971 Nyerere akakaa kimya akaenda kufuata silaha Urusi baada ya waingereza kumkatalia, na mwaka 1978 Vita iliyorudisha maendeleo ya Tanzania na kuharibu uchumi na kuondoa concectration ya Nyerere katika Nchi baadhi na kuyakabili matatizo yake, ilo lilikuwa fanikio kubwa mno na la kushangiliwa na wazungu,

hapa patakusaidia
Top secret CIA files expose US covert operations in Tanzania

KUFA KWA USSR 1992 NA KUZOROTA MAENDELEO YA AFRIKA

Baada ya ujamaa kushindwa na kusambaratika kwa USSR kutokana na Pandikizi la Marekani Gobachev kulipelekea uchimi wa nchi zisizojua kunyonya wengine nazo kuyumba,
Mtaifa mengi ya Africa yalionekana kupenda vya bule na hawakuweka mpango mbadala wa kujikwamua kwa nguvu zao, walitegemea nchi hizo za Urusi kuwasaidia , jambo ambalo limewacost sana

MADHARA YAKE KWA TANZANIA

Mapambano ya kupigania China kuingia kwny Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa yalimyima Dkt Salim Ahmed Salim nafasi ya kuchaguliwa kuwa Katbu Mkuu wa UN Miaka ya 1980s

Tanzania ilikwama kwa baadhi ya mambo kama ujamaa na kukwama juu ya sera zake zenye mlengo wa kikomunist

Figisu za kumnyima Mwalimu Nyerere heshima kwa dunia na kumpa mandela kama mkombozi wa Afrika jambo ambalo linapotoshwa

ulale mahali pema peponi Nyerere.


1469522376_wpc6887ab4.pngMakala hii imeandaliwa na Bitanicca,
Unaruhusiwa kukopi ila acknowledgement ni jambo muhimu,UKIKOPI SEMA UMEITOA WAPI


Britanicca.

cc Pascal Mayalla Shark meningitis barafu
 
Kasinja jr

Kasinja jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2017
Messages
866
Likes
1,427
Points
180
Kasinja jr

Kasinja jr

JF-Expert Member
Joined Aug 4, 2017
866 1,427 180
mhh watu mnayatoa wapi hayo. ila alikuwa kichwa, umesema alisimama kama UKAWA, sawa lakini yeye sisimamia mambo ya msingi na hakuwahi kuziba mdomo kwa Toilet paper kama UKawa, wala hakukubali mafisadi,
 
N

nchonga aliyebaki

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2017
Messages
511
Likes
551
Points
180
N

nchonga aliyebaki

JF-Expert Member
Joined Mar 21, 2017
511 551 180
mgomo wa mzee huyu ulikuwa hatari zaid na akigoma anagomea mambo ya maana si kama wanaogoma siku hizi,
ukitaka kujua mgomo wake muulize mzee mmoja anaitwa abdunuru suleimani, au muulize mzee malechela mgomo wa nyerere ulimtoa kugombea CCM
 
N

nchonga aliyebaki

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2017
Messages
511
Likes
551
Points
180
N

nchonga aliyebaki

JF-Expert Member
Joined Mar 21, 2017
511 551 180
mhh watu mnayatoa wapi hayo. ila alikuwa kichwa, umesema alisimama kama UKAWA, sawa lakini yeye sisimamia mambo ya msingi na hakuwahi kuziba mdomo kwa Toilet paper kama UKawa, wala hakukubali mafisadi,
UKAWA wahuni tu
 
kabwinyola

kabwinyola

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2016
Messages
528
Likes
524
Points
180
kabwinyola

kabwinyola

JF-Expert Member
Joined Aug 5, 2016
528 524 180
hilo jina lilivyoandikwa kirusi hatari ukiambiwa ulitamke mgawane hela za dk shika hakuna wa kuzipata
 
britanicca

britanicca

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2015
Messages
8,882
Likes
12,838
Points
280
britanicca

britanicca

JF-Expert Member
Joined May 20, 2015
8,882 12,838 280
mgomo wa mzee huyu ulikuwa hatari zaid na akigoma anagomea mambo ya maana si kama wanaogoma siku hizi,
ukitaka kujua mgomo wake muulize mzee mmoja anaitwa abdunuru suleimani, au muulize mzee malechela mgomo wa nyerere ulimtoa kugombea CCM
tuambie ili
 
Sky Eclat

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Messages
29,541
Likes
83,100
Points
280
Sky Eclat

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined Oct 17, 2012
29,541 83,100 280
Asante mkuu Britanicca ila tu hujaweka sawa sababu za China kukataliwa kujiunga na baraza la usalama la UN ni ikiukwaji wa haki za binadamu.

Niliwahi kusoma makala moja jinsi wazungu walivyo heshima uwezo wa Nyerere kujenga hoja na kuweza kuwashawishi watu waikubali hoja hiyo.

Uwezo mwingine mkubwa aliokuwa nao Nyerere ni uwelewa mkubwa wa lugha ya Kiingereza pamoja na misamiati yake aliweza kuwa na control katika mijadala ya kidiplomasia.
 
britanicca

britanicca

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2015
Messages
8,882
Likes
12,838
Points
280
britanicca

britanicca

JF-Expert Member
Joined May 20, 2015
8,882 12,838 280
Asante mkuu Britanicca ila tu hujaweka sawa sababu za China kukataliwa kujiunga na baraza la usalama la UN ni ikiukwaji wa haki za binadamu.

Niliwahi kusoma makaka moja jinsi wazungu walivyo heshima uwezo wa Nyerere kujenga hoja na kuweka kuwashawishi watu waikibali hoja hiyo.

Uwezo mwingine mkubwa aliokuwa nao Nyerere ni uwelewa mkubwa wa lugha ya Kiingereza pamoja na misamiati yake aliweza kuwa na control katika mijadala ya kidiplomasia.
sababu kuu za kutotaka china ajiunge na baraza la umoja wa mataifa ni kwamba waliona mbali kwamba CHINA atakuja kuwa na nguvu alafu anaonekana kufuata mlengo wa RUSIA hii iliwatesa sana ,maana nguvu aliyokuwa nayo USSR alafu umuonegezee mwingine kama china ni matatizo, na trend ilionesha CHINA atakuja kuwa na veto power miongoni mwa nchi zenye nguvu.
 
J

JokaKuu

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2006
Messages
14,368
Likes
8,746
Points
280
J

JokaKuu

Platinum Member
Joined Jul 31, 2006
14,368 8,746 280
Asante mkuu Britanicca ila tu hujaweka sawa sababu za China kukataliwa kujiunga na baraza la usalama la UN ni ikiukwaji wa haki za binadamu.

Niliwahi kusoma makala moja jinsi wazungu walivyo heshima uwezo wa Nyerere kujenga hoja na kuweza kuwashawishi watu waikubali hoja hiyo.

Uwezo mwingine mkubwa aliokuwa nao Nyerere ni uwelewa mkubwa wa lugha ya Kiingereza pamoja na misamiati yake aliweza kuwa na control katika mijadala ya kidiplomasia.
..zama hizi tumepwaya sana ktk medani ya diplomasia na mashirikiano ya kimataifa.
 
britanicca

britanicca

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2015
Messages
8,882
Likes
12,838
Points
280
britanicca

britanicca

JF-Expert Member
Joined May 20, 2015
8,882 12,838 280
..zama hizi tumepwaya sana ktk medani ya diplomasia na mashirikiano ya kimataifa.
kabisa kuanzia kuondoka kwa Nyerere tumepwaya sana hasa kwa mheshimiwa Magufuli ndo tumepwaya kabisa
 

Forum statistics

Threads 1,237,407
Members 475,533
Posts 29,287,333