Baada ya mahojiano na Diamond, Times FM wawekwa kikaangoni na kamati ya maudhui ya TCRA

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
52,209
42,068
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kamati yake ya maudhui inafuatilia mahojiano ya mwanamuziki Nasseb Abdul maarufu Diamond aliyoyafanya katika kituo cha Redio cha Times jijini Dar es Salaam.

Mkuu Idara ya Utangazaji ya mamlaka hiyo, Andrew Kisaka amesema wamechukua uamuzi huo kwa kuwa mahojiano hayo yamefanyika katika kituo wanachokisimamia.
=======

Baada ya Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe kusema kwamba amesikitishwa na kauli za Diamond alizozitoa kupitia kipindi The Playlist cha Times Fm dhidi ya Naibu Waziri wake, Juliana Shonza, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kamati yake ya maudhui inafuatilia mahojiano ya mwanamuziki huyo aliyoyafanya katika kituo hicho.

Akiongea na mtandao wa gazeti la Mwananchi leo, Ofisa Mkuu Idara ya Utangazaji ya mamlaka hiyo, Andrew Kisaka amesema wamechukua uamuzi huo kwa kuwa mahojiano hayo yamefanyika katika kituo wanachokisimamia.

Katika mahojiano hayo, Diamond alimjibu Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza kutokana na Serikali kuzifungia nyimbo 15 mwezi uliopita, zikiwemo mbili za mwanamuziki huyo.

Kisaka amefafanua kuwa kiutaratibu wao wanaangalia zaidi chombo ambacho wamekipa leseni na kwamba, masuala mengine yatashughulikiwa na mamlaka nyingine.

Amesema suala hilo kwa sasa linafanyiwa kazi na kamati ya maudhui na kuahidi kulitolea ufafanuzi siku za hivi karibuni akiwataka wananchi kuwa na subira.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo DKt. Harrison Mwakyembe amesema si busara kwa Diamond kushindana na serikali endapo ana ushauri wowote ni vema akauwasilisha kwa njia sahihi na si kumshambulia Naibu Waziri kwa dharua na kejeli.

Chanzo; Bongo 5
 
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kamati yake ya maudhui inafuatilia mahojiano ya mwanamuziki Nasseb Abdul maarufu Diamond aliyoyafanya katika kituo cha Redio cha Times jijini Dar es Salaam.

Mkuu Idara ya Utangazaji ya mamlaka hiyo, Andrew Kisaka amesema wamechukua uamuzi huo kwa kuwa mahojiano hayo yamefanyika katika kituo wanachokisimamia.
Wanahangaika tu
Wajue hata shoza japo anasema ni serikali naye ni mtu na kila mtu ni sehemu ya serikali.

Haya mambo wajifunze mtu anavyokwenda mrama hali ya kua kabeba dhamana ya kiserikali.
 
Tumsubiri TCRA naye,sijui ataifungiaTimesfm au WasafiTv na Redio ,pamoja kupanic kwa Diamond (jamaa anapoint ila tatizo uwasilishaji wake ,lkn yupo sahii 100%) lakini wajitafakari kwanza BASATA ,TCRA na WIZARA hii tasnia ya burudani inaenda kimungumungu (wasanii walivyo kama wale mbuzi wakafara) na maamuzi yao yanawaumiza wasanii baada ya kuwasaidia.
 
Hii Chuki inayoanzishwa sio salama kwa nchi na Afya ya jamii kwa TCRA inataka kusimamia mazungumzo ya Live pia kama Watafuatilia YouTube wao inawahusu huko wameshindwa kudhibiti upoteaji wa mapato ya Wasanii wameingilia huu ugomvi walishindwa kuzungumza lolote kesi ya Ay,Fa na Tigo leo eti kuchunguza mazungumzo hayo What is next ?.
 
kuna nchi design ya china,cuba venezuela n.k ni aina ya nchi zenye sheria na taratibu nyingi kwelikweli kiasi kwamba unaeza kujikuta hauna uhuru wa kutosha tusielekee huko jamani
 
Oooh ghafla visenti sina nimerudi tandale,
Nimeshindwa kulipa bima nimeuza madale,

radio nyimbo wamezima TV ndiyo hataree,
Umeneja umebaki jina hanitaki hata tataleee

Ooh wale mashabiki zangu walionisifu kwa maneno matamu, leo ndiyo maadui zangu ni mitusi tu kwa Jamii forum,

Kimwana si dada yangu eti naye hanifahamu,
Hata WCB nikiwapigia wananifokea hata salamu.


Yametimiaaaaaaa..... !!
 
Oooh ghafla visenti sina nimerudi tandale,
Nimeshindwa kulipa bima nimeuza madale,

radio nyimbo wamezima TV ndiyo hataree,
Umeneja umebaki jina hanitaki hata tataleee

Ooh wale mashabiki zangu walionisifu kwa maneno matamu, leo ndiyo maadui zangu ni mitusi tu kwa Jamii forum,

Kimwana si dada yangu eti naye hanifahamu,
Hata WCB nikiwapigia wananifokea hata salamu.


Yametimiaaaaaaa..... !!
u wish
 
Nilichogundua Diamond ni kijana mwenye nguvu na ushawishi sana hapa TZ.

Interview aliyofanya imezidisha umaarufu kwa Times fm, mtangazaji Lil Ommy, Juliana Shonza na Basata. Hasa hasa hiyo radio na mtangazaji wake kuna watu naamini walikuwa hawaijui kabisa au kuisikia hiyo radio pamoja na mtangazaji huyo ila wiki hii wanazungumziwa kutokana na Diamond.
 
We dogo alinifurahisha sana wenzie wanatekwa ye akatoa kibao cha BORA NIKAE KIMYA sasa yamemkuta anaenda kubwabwaja tena radioni mbona hajatumia zile busara za kukaa kimya kumbe mpka watu waguswe maslai yao ndo hawakumbuki kukaa kimya!!
 
Raha ya nchi yetu unapo fanya jambo lolote kutafuta mkate kabla ujafanikiwa hakuna hata mtu yoyote hata kuwa mda na wewe na Serikali yako lakini ikisha vuka kila mtu anafanya kukujua na kuwa juu yako.
 
Back
Top Bottom