Baada ya Magufuli, TANESCO wanaanza kata kata ya umeme

zimmerman

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
1,628
3,155
Hayati Magufuli aliwahi kujitabiria kwamba Watanzania watamkumbuka kwa mazuri na si kwa mabaya.

Hii katakata ya umeme hapa Iringa Manispaa ambako tangu Magufuli afariki naona imekuwa kawaida kila siku umeme unakatwa, tena bila taarifa yoyote. Kata kata hii ilipigwa marufuku kipindi cha Magufuli na kauli yake mashuhuri kipindi akiwa hai ilikuwa "yeyote atakayekata umeme atakatika yeye" iliwafanya watendaji wa TANESCO kuwa makini muda wote, na ni kweli umeme ulikuwa stable sana enzi za JPM. Hii yote inadhihirisha umuhimu wa kuwa na kiongozi imara pale juu.

Mama Samia chonde chonde usifanye watanzania tummiss JPM zaidi ya ile kawaida. Uliahidi mwenyewe kwamba mazuri ya Magufuli utayaendeleza lakini tangu umekalia kiti haijasikika sauti yako thabiti juu ya upuuzi puuzi kama huu wa Tanesco kukata umeme mara kwa mara namna hii.
 
Huyo Magufuli angekuwa anafanana na mnavyomuandika basi asingekufa.

Kwa sisi wakazi wa Dar es Salaam miaka yote 5 ya Mwendazake umeme ulikuwa unakatika kwa kiwango hiki hiki cha wakati wa Samia
Ushahidi: Tafuta kauli za Kalemani akiwakaripia wafanyakazi wa TANESCO kwenye Google
 
Huyo JPM angekuwa anafanana na mnavyomuandika basi asingekufa.

Namba 1 huyu hapa. Subiri wengine
 
Ni kweli japo nilimpinga jiwe kwa mambo mengi Sana ,Ila suala la umeme alilidhibiti.Sahivi panya wa tanesco wanatawala.Hata kuja kukufungia umeme wanadai Hamna mita,Jambo ambalo halikuwepo enzi za mwendazake
 
Ndio maana huwa najiuliza hivi Mwendazake hakuandaa Mtu mwenye muelekeo wake?.
 
Huyo JPM angekuwa anafanana na mnavyomuandika basi asingekufa.

Kwa sisi wakazi wa Dar es Salaam miaka yote 5 ya Mwendazake umeme ulikuwa unakatika kwa kiwango hiki hiki cha wakati wa Samia
Ushahidi: Tafuta kauli za Kalemani akiwakaripia wafanyakazi wa TANESCO kwenye Google

Dar ipi hiyo umeme ulikua unakatika

Au ile ya JK na Lowasa 🙄🙄🙄
 
Scenario nyingine hazina mantiki kabisa, unataka kuaminisha umma kua tanesco kipind hiki wanafanya makusudi? Vitu vingine hua viko technically, hata wakati yupo umeme baadhi ya maeneo ulikua unakatika sana mpaka jion ndo unarud. Msi aminishe watu kua mtu mmoja ndie ana uwezo wa kuongoza. Low IQ, think about it!
 
Acha upotoshaji wa kijinga, tatizo la umeme kukatika limeanza mwaka jana wakati wa kampeni, na tumepiga kelele kwenye hilo sana. Kama ni tatizo limeanza enzi za Magufuli na sasa ni muendelezo tu.
 
Sijajua maeneo mengine ila Dar es salaam Mbezi Kimara toka enzi za hayati mpaka dakika hii umeme huwa unakatika mara kwa mara
 
Scenario nyingine hazina mantiki kabisa, unataka kuaminisha umma kua tanesco kipind hiki wanafanya makusudi? Vitu vingine hua viko technically, hata wakati yupo umeme baadhi ya maeneo ulikua unakatika sana mpaka jion ndo unarud. Msi aminishe watu kua mtu mmoja ndie ana uwezo wa kuongoza. Low IQ, think about it!
Hizo technical problems ambazo hazikujitokeza kipindi cha JPM ndio zimeanza kujitokeza mara tu baada ya JPM?
 
Back
Top Bottom