brasy coco
JF-Expert Member
- Apr 25, 2012
- 1,489
- 896
Anaitwa Mansoor Yusuf Himidi alikuwa Waziri asiyekuwa na Wizara maalum na mweka hazina wa CCM kabla ya kufukuzwa kazi na Rais wa Zanzibar Dr. Ally Mohammed Shein. Na wadhifa huo kupewa bi Shawana Buheti Hassan, Mansoor anaishi Chukwani alikuwa akiwasidia Wananchi wanaoishi maeneo hayo ya Chukwani Zanzibar kwa kuweka mota inayovuta maji na kusambaza katika nyumba za wananchi, lakini baada ya kutolewa Uwaziri Mansoor kwa khasira au ameamua tu, ameitoa Mota ambayo ilikuwa ikiwasaidia wananchi kupata maji ambayo aliweka yeye kuwasaidia wananchi.
Wananchi wanaoishi katika maeneo hayo wamekuwa na shida ya maji sasa na kwalazimu kwenda umbali mrefu kidogo kufata maji, baadhi ya wanachi wamekuwa wakihoji kuwa ina maana mansour hakusaidia kwa moyo wake bali kwa kuwa alikuwa waziri so baada ya kutolewa ndo atoe mota yake?? Wamesikitika sana hata ivyo kuna Mtu amehaidi kununua mota nyingne ii kurejesha hali nzuri ya huduma ya maji.
Mansour alikuwa akisapoti Mabadiliko ya Muundo wa Muungano na kutaka Zanzibar na Tanganyika wawe na Muungano wa mkataba, ili Zanzibar ipate mamlaka yake na kuiwezesha kuwa na kiti UN pia Mansour alisema kutoa maoni yake si dhambi ila kama atapewa adhabu yeyote yupo tayri na hata ikivuliwa Uanachama CCM hatobadili Msimamo wake, amesema hajawahi hata siku moja kutamka muungano uvunjike ila anataka Muungano wa Mkataba utayoiwezesha zanzibar na Tanganyika kuwa wote wana Viti UN.
Nape alitaka Mansour arudishe Kadi kwa kuwa yupo Against na sera za CCM, Mansour hataki sera ya serikali 2 yenye kuibana Zanzibar na kuifanya ishindwe kujitegemea na kujitawala yenyewe.
Amesema Rais Kikwete alipotoa wazo lake kutaka kuweka serikali ya Umoja wa kitaifa Zanzibar wengne walipinga kwa kuhofia kupinduliwa baada ya wao kuwapindua mwaka 1964( hapa mansour anamanisha kwamba mwaka 1964 walipinduliwa Utawala wa kipemba na kuchukua Nchi waunguja lakini kuna uchambuzi wa kina hapa) lakini baada ya kuisimamisha GNU sasa wanaona matunda yake kwani hata nao CUF walikuwa wakipinga kila jema la SMZ lakini baada ya kupewa nao sasa wanasimamia yale waliyokuwa wakiyapinga na kushangilia, so baada ya kuwepo muungano wa mkataba watu wataona matunda yake japo wengne sasa hawataki kwa manufaa yao binafsi hao viongozi.