Baada ya Kutoswa Uwaziri: Shamsi aungana na wazanzibari wanaotaka Mamlaka Kamili ya nchi yao...

Mbona wana uwezo huo wa kuwa kamili !!!
Hata mimi sijui kwanini hawajaamua.

CHAMVIGA hebu washauri wasije katika bunge la katiba, kila kitu kitakuwa kimeishia hapo.
Umewasikia wenyewe wanasema wanaogopa gharama, sasa hapo nani amewang'ang'ania?

Kaka mkuu najua unajua vizuri sana habari za huu uitwao muungano. Tanganyika ndio iliyoomba uwenza na Zanzibar na wala sio Zanzibar kuomba uwenza na sisi. Kwa logic hiyo ndogo tu unapata picha kuwa Tanganyika iliutaka uwenza huu kimkakati na probably Tanganyika ndio inafaidi uwenza huu. Kisha ili kuhakikisha muungano huu haufi ndipo siasa zinachukua nafasi yake. Karibia asilimia 90 ya viongozi wa SMZ wanaokuwa madarakani wanafanyakazi kwa maagizo kutoka Tanganyika. Wachache wanaoamua kusimama na kuonyesha misimamo yao ya kuitaka nchi yao yenye mamlaka kamili ndio hao wanashughulikiwa mapema kabla hawajaota pembe. Yuko wapi Jussa, Mansour na wengineo waliotaka kuchezea sharabu za Simba? I wish watanganyika nasisi tungeandamana nchi nzima kushikiniza hili dubwasha linaloleta malalamiko kila uchwao linakufa.
 
Mwenye Elimu ya msingi hadi Form IV ndio wanatakiwa kuuliza swali hili. Kwa msomi yeyote Jibu liko wazi kama unakishughulisha kichwa chako.

Mimi hata elimu ya msingi sina ndiyo maana nimeuliza na wapo walionijibu kama wewe unaona shida basi pole.
 
Kaka mkuu najua unajua vizuri sana habari za huu uitwao muungano. Tanganyika ndio iliyoomba uwenza na Zanzibar na wala sio Zanzibar kuomba uwenza na sisi. Kwa logic hiyo ndogo tu unapata picha kuwa Tanganyika iliutaka uwenza huu kimkakati na probably Tanganyika ndio inafaidi uwenza huu. Kisha ili kuhakikisha muungano huu haufi ndipo siasa zinachukua nafasi yake. Karibia asilimia 90 ya viongozi wa SMZ wanaokuwa madarakani wanafanyakazi kwa maagizo kutoka Tanganyika. Wachache wanaoamua kusimama na kuonyesha misimamo yao ya kuitaka nchi yao yenye mamlaka kamili ndio hao wanashughulikiwa mapema kabla hawajaota pembe. Yuko wapi Jussa, Mansour na wengineo waliotaka kuchezea sharabu za Simba? I wish watanganyika nasisi tungeandamana nchi nzima kushikiniza hili dubwasha linaloleta malalamiko kila uchwao linakufa.
Hapana hapa ni kutafuta njia ya kukwepa ukweli almaarufu CHAMVIGA.

Kuna fursa zimetokea ambazo ZNZ hawakuzitumia.
1. Hawajawahi kupeleka hoja ya kuvunja muungano BLW
2. Hawajawahi kuleta hoja ya kuvunja muungano Dodoma
3. Hawajawahi kuomba kura ya maoni.

Arguably hiyo inatokana na 'asilimia 98 ya viongozi kufuata maagizo ya Tanganyika'
Fursa ya pili
1. Walitakiwa wasitoe wajumbe wa tume ya Warioba, wakang'ang'ania wajumbe sawa
2. Walitakiwa wasishiriki vikao vya rasimu aache asilimia 98 unayosema ambayo ni watu chini ya 300.
3. Walitakiwa wasilete wajumbe bunge la katiba, wao wanataka idadi sawa.

Hadi hapo unaona dhahiri kuwa hawana nia ya kujiondoa katika 'makucha' ya mkoloni wa bara
Lakini unajichanganya unaposema Tanganyika waandamane kupinga muungano.

Umeghafilikiwa kidogo kwa kusahau kuwa ni wewe uliyesema Tanganyika imewaomba muungano na inawang'ang'ania.

Sasa kama ina wang'ang'ania itaandamaje kupinga haja yao?
Huoni anayeonewa ndiye anapaswa kufany hivyo?

Na pia umechomeka hoja kuwa Tanganyika inafadika na muungano.
Kwa miaka zaidi ya 3 tumejadili nyuzi kwa nyuzi kuhusu muungano na faida zake.

Tumeweza kuwaamsha wznz waliokuwa wanaamini kuwa znz ina nyonywa kwa kuwaonyesha kwa mantiki na tawkimu kuwa Tanganyika hainufaiki na kinyume chake ni ukweli.

Nahodha kasema hapo juu, gharama za kiti UN, gharama za Ulinzi na usalama na gharama za sarafu ni kubwa sana na akawataka wznz waangalie mambo hayo.

Jusa alisema anataka muungano kwasababu za kisiasa na kiuchumi.
Mansour Himid na Nasor Moyo wote wamesema hata mama Fatma naye kashadidia. S
asa hawa wanaonyonywa wanataka muungano wa nini tena?

Labda una la nyongeza kuhusu Tanganyika kufaidika na muungano, hebu tukusikilize una hoja zipi?

Mkuu Nguruvi3 unajitahidi kupindisha mantiki ya maelezo yangu sijui kwanini. Kwanza mimi nimesema watanganyika tuandamane na sio Tanganyika. Tanganyika inaongozwa na watu ambao haohao ndio hasa wanajua lengo na malengo ya huu muungano ni wazi kwakuwa wanajua faida yake ndio maana wana ung'ang'ani. Nina imani kuwa hata raia wengi wa Tanganyika hawaupendi na hawajui maslahi ya muungano kwao. Ndio maana nikasema ni bora hata tungeungana kuukataa huu muungano ambao faida yake wanafahamu wachache na wengi ni mabubu hata ukiwauliza ni nini hasa watanganyika tunafaidika. Kisha hiyo unayoitata fursa ya kwanza hata ya pili unategemea nini kwakiongozi anayetekeleza maagizo au anayeendeshwa kwa remote control? Apeleke mapendelezo ya kuvunja muungano BLW kisha atamjibu nini aliyemuweka. Asitoe wajumbe katika tume ya katiba kisha amjibu nini bosi wake? Asilimia kubwa ya wananchi wa Zanzibar hawaupendi na hawautaki muungano na sio viongozi wa Znz.
 
Last edited by a moderator:

Tanganyika na Watanganyika sijui unawezaje kuwatenga.
Anyways, hilo suala la wznz hawapendi muungano si kweli. Wasingependa muungano nusu yao wasingeishi bara.
Wasingependa muungano wangeitisha kura ya maoni kuwashinikiza viongozi wao.
Wasingependa muungano wasingemchagua mtu wa CCM ambaye makamu wake ni mzanzibar na yupo kwasababu ya uzanzibar tu na wala si sifa au kitu kingine.
Wasingependa muungano wasingeyasema waliyoyasema katika kongomano la bwawani mwaka 2012 oktoba 6.

Wanaowaongoza wznz wengi unaosema wasiopenda muungano ni akina Maalim, Jusa, Himid, Moyo, Bakar
Wao wametamaka wazi wanataka muungano, sasa hao wengi ni wapi?

Kelele za watu 4 kwenye basi zinaweza kufanya basi zima lionekane zogo kumbe ni wlevi 4 tu.
Kama hawapendi muungano kuna fursa nyingine inakuja, nayo ni kura ya maoni, wasusie kabisa wasiende vituoni.
 
Wazanzibar wengi hawajui wanarubuniwa na viongozi wao kama walioanza kuchangia hapo juu,kuvunja muungano hawatakiwi kutumia nguvu kabisa ni rahisi sana,kama wanataka wawakilishi wao bungeni wasije kabisa,wazanzibar wanaofanya kazi bara waondoke,Bilali naye arudi wote warudi hadi wafanya biashara wao warudi wao kweli kama wanaipenda nchi yao kweli sasa, huu ni unafiki mkubwa kujitamba eti wanaita nchi yao kwani hata hivyo kuna aliyeondolewa zanzibari na kupelekwa kuishi asikotaka, hawa viongozi wanarudi kutafuta nguvu ya umma wanaposhindwa kuwajibika kwenye kazi walizopewa,kama ni kutemwa uwaziri wabongo au wabara wangapi wametemwa nafasi hizo na kutulia kwa kushindwa kuwajibika ipasavyo!!that's life !! afanye mengine.these people have no permanent friend they have always permanent self interests ,he supposed to be quite.
 
Mkuu nimepata kigugumizi, kwenye wekundu hapo hao wawili mbona kama bado wapo kwenye siasa!! Ujumbe wa Tume ya Katiba siyo sehemu ya siasa? Unamsemeaje Sumaye?

Sumaye nhuiongea kama raia wa kawaida tu, siyo mwanasiasa tena kwa vile hana cheo chochote cha kisiasa ukiachilia vile wanavyobaki navyo kama matokeo ya kustaafu wadhifa wa uwaziri mkuu; kama anacho basi naye siyo mstaafu. Salim na Waryoba ni raia wa kawaida kabisa, hawana vyeo vyovyote vya kisiasa ila vile vinavyotokana na nyadhifa zao za zamani. Ujumbe wa tume yoyote ile siyo madaraka ya kisasa; in fact tungeweza kuwa na wajumbe kwenye tume ya katiba ambao siyo watanzania. Kenya walikuwa na wajumbe wengi sana kwenye tume yao ya katiba ambao hawakuwa wakenya.
 
Back
Top Bottom