Money Stunna
JF-Expert Member
- Aug 9, 2011
- 13,054
- 6,281
Kuna kitu watu hawajui kamwe maoni ya wengi hayawezi kuwa ya wachache kwenye demokrasia ya kweli wengi ndio wanashinda.
Warudishe pesa walizochukua hao
Warudishe pesa walizochukua hao
Wanafiki tu hao, wameshapiga pesa za kutosha now wanajifanya kususa!
hawa jamaa nilishawauri siku nyingi sana waungane! Watanzania wanahitaji ukombozi na uhuru kamili si kupitia utitiri wa vyama lakini kwa kuwaondoa ccm!
Ukawa mbaki vivyo hivyo hadi ccm waondoke! Muulizeni raila odinga mbinu alizotumia kuing'atusha kanu madarakani
Wanafiki tu hao, wameshapiga pesa za kutosha now wanajifanya kususa!
Siku upinzani ukiungana ndipo taanza kuamini ukombozi umefika.
Thursday April 16th 2014
Julius S. Mtatiro
TUMEJIONDOA RASMI KATIKA MCHAKATO WA KATIBA!!
Tumeamua kuwaachia CCM waendelee na mchakato wa katiba
wanayoitaka.
Kwa sababu wameyakataa maoni ya wananchi, na Sasa wameanza vitisho kwenye makanisa, ati wananchi wakipitisha serikali Tatu Wao CCM wataikabidhi nchi iongozwe kijeshi ni vema Sasa tuwaache.
Kwa nia njema kabisa, hatutaki kuwa sehemu ya matusi, kauli nzito kabisa za ubaguzi na kila aina ya upuuzi.
Kama CCM walikuwa na katiba yao wacha waendelee kutengeneza.
Sisi tunarudi kwa wananchi.
Katiba mpya itapatikana tu pale kutakapokuwa na nia njema hasa kutoka kwa vyama kinachoongoza dola.
Mungu ibariki Tanzania!
Ni kweli kabisa ulichosema, wanaopaswa kurudisha hela ni hao wajumbe wa CCM waliobaki.Thanks. Wapuuzi wanasema warudishe hela. Mimi nadhan wakurudisha hela ni waliobaki. Ambao wameenda kinyume na walochoagizwa kukifanya.
"Ndiyo maana, wachache wetu tulipendekeza tuwe na Bunge Maalum la kuchaguliwa na wananchi moja kwa moja. Lakini watawala wetu, pamoja na watawala watarajiwa na wengi wa wanaharakati, katika busara zao na kwa maslahi yao, hawakutilia maanani pendekezo letu. Tumepoteza nafasi ya kipekee ya kihistoria ya kuwa na Bunge Maalum la kuchaguliwa, jambo ambalo limetufikisha hapa tuliko" - Profesa Issa Shivji: Dhana na Maana ya Bunge Maalum la Katiba
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/608682-prof-shivji-ampa-darasa-mzee-warioba-wajumbe-wa-bunge-la-katiba-someni-ili-msiyumbe.html