Baada ya kutelekeza mimba, ililelewa na mwingine mtoto akapewa yeye (r.i.p) na jina lake

Huwa nawachukia wanaume wenzangu washenzi kama wewe mkuu!!!!Hvi unakataaje mimba?unaanzaje!!!mimi hata kama ziwe Buku sizikatai!!Muwe mnaacha usenge mazee!!!
 
Sasa mkuu kwa ushauri huu unaniweka njia panda ya ni bet for future?
Mkuu, kuna hadithi inasema, mkulima wa shamba alipanda mbegu ya pekee kabisaa duniani, ikamea na kuzaa matunda ambayo hakuna mtu mwingine yeyote aliyekuwa nayo. Kila msimu mtu akitaka zao la mti ule ni lazima apate kwa mkulima yule.

Ikatokea, ndege wakala tunda la mti, wakajisaidia kwenye shamba la mtu mwingine, ukaota mti, ukazaa matunda.

Swali likawa, mti ule ni wa nani? Mwenye shamba, au mwenye mbegu? Ikaamuliwa kuwa mwenye shamba ndio mwenye mti. Shamba ni yule mwanamke, kama jamaa asingetangulia mbele ya haki, pengine usingetafutwa lakini zaidi, wewe ukiwa timamu ulikataa, na huyu mpaka umauti unamkuta aliamua kuwa yule ni matokeo ya shamba lake, hivyo ni jukumu lake, kwa HESHIMA ya huyo jasiri, narudi tena, kaa mbali na huyo mama na mtoto, muache mtoto aje akutafute mwenyewe kwa wakati utakaokuwa umepangwa.
 
Hapo zamani nilikuwa na mchumba ambae hadi kuachana kwetu tayari alikuwa na mimba changa. Nlijua ila baada ya kuvurugwa kwa kutengana kule nilimkatalia kwa kumwambia sina mwanamke mwenye mimba kama wewe.

Yule binti akapata mtu mwingine ambae alidumu naye hadi kajifungua. Sijui walikubaliana nini ila mtoto aliandika jina lake kama baba mzazi.

Baada ya miezi kadhaa R.I.P. kijana kafariki na baada ya muda mwanamke kaolewa na mwanaume mwingine.

Leo tarehe 22/01/2020 mwanamke aliniita na akawa amenambia kuwa mtoto huyu japo unamtenga na haumhudumii ila ni wako. Alienda mbali na kunambia kuwa Ndugu wa marehemu walimjia kumwambia kuwa marehemu aliwaambia mtoto ni wake.

Yeye aliwakatilia kwa kuwaambia kuwa mtoto huyu ana baba ila sio mtoto kwenu. Ndugu wa marehemu wamegoma na wanaendelea kumtambua kama mtoto wa mtoto wao.

Naomba msaada kama inawezekana Kumpata mtoto kisheria na kubadili jina la baba ili liwe langu.
Pole kwa yaliyokukuta japo ni ya kujitakia (hukupaswa kukataa ile mimba). Ninachokushauri kufanya ni kama ifuatavyo:
Ninaamini kwenu una wazazi kama hawapo tafuta mtu/watu wazima uwaeleze kinagaubaga kilichotokea na unachotaka kufanya sasa.

Kisha wao wataenda kuongea na wazazi wa mwanamke halafu tena waongee na wazazi wa baba mlezi aliyefariki kisha watakuletea majibu na hapo ndiyo ujue jinsi ya kufanya. (Nina imani utapata mwanao)
 
Ahsante kwa mchango mzuri ndugu

Sawa na Ahsante kwa ushauri wako
Mkuu, kuna hadithi inasema, mkulima wa shamba alipanda mbegu ya pekee kabisaa duniani, ikamea na kuzaa matunda ambayo hakuna mtu mwingine yeyote aliyekuwa nayo. Kila msimu mtu akitaka zao la mti ule ni lazima apate kwa mkulima yule.

Ikatokea, ndege wakala tunda la mti, wakajisaidia kwenye shamba la mtu mwingine, ukaota mti, ukazaa matunda.

Swali likawa, mti ule ni wa nani? Mwenye shamba, au mwenye mbegu? Ikaamuliwa kuwa mwenye shamba ndio mwenye mti. Shamba ni yule mwanamke, kama jamaa asingetangulia mbele ya haki, pengine usingetafutwa lakini zaidi, wewe ukiwa timamu ulikataa, na huyu mpaka umauti unamkuta aliamua kuwa yule ni matokeo ya shamba lake, hivyo ni jukumu lake, kwa HESHIMA ya huyo jasiri, narudi tena, kaa mbali na huyo mama na mtoto, muache mtoto aje akutafute mwenyewe kwa wakati utakaokuwa umepangwa.
 
Wewe ilikuwa ni Sperm Donor tu (Donor Kantre), hiyo haimaanishi kuwa nchi ni yako (mtoto).
 
Back
Top Bottom