Naja naja
JF-Expert Member
- Sep 13, 2016
- 747
- 1,452
Baada ya kusota sana mtaani hatimaye nuru imeonekana.
Kwa kifupi nilisoma ngazi ya degree lakini sikuweza kuhitimu kutokana na masuala ya kifedha.
Misukosuko iliniandama baada ya mzazi kuumwa sana hivyo uchumi uliyumba sana hivyo nilipostpone .
Baadaye nika resume masomo hivyo hivyo kibishi lakini kwa bahati mbaya mzazi akafariki na nikajaribu kuongea na uongozi wa chuo waangalie namna ya kunisaidia lakini ikashindikana na nikakosa namna kabisa ya kuendelea hivyo nikaamua kuacha masomo na kuja mtaani kupambana.
Nilipambana vya kutosha huku na kule sana sana viwandani haswa viwanda vya Murzah two na four.
Hatimaye nimebahatika kupata mfadhiri na tumewekeana makubaliano maalum ya kurudisha fedha baada ya kumaliza masomo.
Hivyo nimebahatika kuanza taratibu za usajili chuo kingine.
Lakini alichosema atanisaidia vitu basic ambavyo ni ada na hela ya kula nikiwa chuoni.
Hii ni faraja kubwa sana kwangu .
Pia iwe mfano kwa wengine waliokata tamaa waombe kwa Mungu atawainua siku moja.