Baada ya kusota mtaani, nimepata kazi serikalini kama injinia wa maji!

Siyo ckuhz mkuu...jamaa angu mwingine aliajiriwa halmashauri flani kada ya kilimo mwaka jana nae alisota sana...mambo ckuhz chini ya huyu mtetezi wa wanyonge yamebadilika inatakiwa ajiandae kisaikolojia kwa lolote

duh mbona hii ni kali sn basi kweli mambo yamebadilika
 
Habari wana JF!!

Mwaka jana nilileta uzi hapa ili wenyeji wa Dar wanielekeze sehem utumishi wa uma walipo na pia wanielekeze sehemu nzuri ya kufikia!!Refer: Kuuliza sio ujinga: Nina safari ya DSM, naombeni muongozo wenyeji

Wengi walichangia na kunipa mwanga, nawashukuru kwa maoni maana nilifanikiwa kwenda kwenye usaili na Mungu si athmani nimefanikiwa kupata kazi kama mhandisi wa maji yaani water resource engineer!!

Nimerudi tena kwenu wadau mnipe mawazo hasa kwa wale watumishi wa umma au wenye uzoefu wa ajira za serikali!!

1.Hapa nnangoja barua ya kazi, je kuna stahiki zozote nnapewa hasa baada ya kupangiwa kituo?

2. Je ni changamoto gani nitarajie kukutana nazo kama mtumishi wa umma!

3. Vipi kuhusu mifuko ya hifadhi? ni upi bora?

4. Vipi kuhusu makato ambayo naweza kuwa nakatwa kwenye mshahara wangu kama mtumishi wa umma?

5...

Karibuni kwa mawazo wadau!!
UNA KARIBISHA WACHAWI WAKUJUE VIZURI
 
Sisi tumeambiwa turipoti kwa katibu mkuu wa wizara ya maji na umwagiliaji... sijui huko nako pakoje kwenye swala la stahiki!!

kuna mtu kaniambia hapo juu mambo ya cku izi ni sio km zamani so jiandae kisaikolojia chochote kinaweza tokea ukapata mapema au uka zungusha
 
Siyo ckuhz mkuu...jamaa angu mwingine aliajiriwa halmashauri flani kada ya kilimo mwaka jana nae alisota sana...mambo ckuhz chini ya huyu mtetezi wa wanyonge yamebadilika inatakiwa ajiandae kisaikolojia kwa lolote
Duuuh!! alizungushwa siku ngapi mpaka kupewa stahiki zake??
 
hongera mkuu, sisi na elimu zetu bado tunalima kitunguu na tikiti...:eek::eek::eek::eek: kwa miezi minne tunaambulia 500,000.. huku tuna vyeti vyetu vya uhandisi(eng) :rolleyes::rolleyes::rolleyes:
Si kuna sera kilimo kinalipa kwa vijana vipi hapo 500k miezi 4 si ni nadharia kama hivi!
 
Nenda kapate uzoefu na kujenga connection na halmashauri zote za mkoa unaoenda halafu baada ya miaka mitano fungua kampuni yako uchukue tenda.

Achana na habari za kuajiriwa, mshahara huwa hautoshi. Pambana usajiliwe na board ya engeneers upate na certificate kwa maandalizi ya kufungua kampuni. Construction Ina hela sana.

Shukuru Mungu umepata mtu wa kukupa huu ushauri, kazi kwako
 
Hadi leo hajalipwa but mshahara alianza kupata baada ya miezi miwili...but usiogope mkuu unaweza ukafika tu na baada ya mda kidogo upate stahiki zako
Ila si alipewa mshara wa hiyo miezi miwili au ilikuaje mkuu? Na akiwa anangoja mshahara alikua kazin au alirudishwa nyumban??
 
Ila si alipewa mshara wa hiyo miezi miwili au ilikuaje mkuu? Na akiwa anangoja mshahara alikua kazin au alirudishwa nyumban??
Mshahara alipewa wa mwezi mmoja kuanzia hapo mshahara ukaanza kuingia kama kawaida...mshahara mmoja aliuandikia barua ukawa kama madai kuna siku bila shaka atalipwa...alivyofanya mwezi mmoja bila kupata mshahara aliomba ruhusa ya week ka mbili hivi akarudi nyumbani kidogo...but usihofu mkuu changamoto huwa zinatokea mwanzoni tu
 
Moja,usikimbilie kuoa
mbili,kwa kuwa dar ni mgeni ukipata dem usimpeleke kwako we piga juu kwa juu,ukimpeleka home tu,kahamia ukizingatia jiko linawaka nyumbani.
Tatu.epuka kutumia maji yenye rangi ya mende yanalostisha.
Nne.weka akiba sana na jibane kwenye matumizi
tano.epuka kusaidia sana ndugu
yangu ndo hayo
nimecheka kifala
 
Sio kila mkopo una masharti mkuu!!


Hii ni hofu yako na nnakushauri usiwe na hofu!!


Kumbuka sio kila kipanga darasani basi na uraiani atakua kipanga!

Nimepikwa nikapikika miaka minne chuoni na zaidi ya yote nilikua na 'A' kwenye kozi ya engineering practice and ethics!!

Usiwe na hofu kiongozi!!
 
Hivi huko serikalini kuna kitu gani? Mbona kila anaepata kazi huko huona kama vile amefanikisha kitu kikubwa maishani mwake..
 
Back
Top Bottom