Baada Ya Kupotea Zaidi Ya Miaka Milioni 65 Ameibuka Tena

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,610
1,809

Samaki mkubwa wa kihistoria duniani ambaye alikuwa amepotea zaidi ya miaka milioni 65 ameibuka juzi katika Kisiwa cha Nyuli, Pwani ya Tanga na kuvuliwa na wavuvi wa eneo la Sahare Jijini hapa.

Samaki huyo aina ya Silikanti amekuwa akipasua vichwa vya wanasayansi ya viumbe wa majini duniani kutokana na umbile lake kuwa na viwiko vya miguu na mikono, pingili na mafuta mengi tofauti na samaki wengine.

Mshauri wa Uvuvi katika Sekretarieti ya Mkoa wa Tanga, Hassan Juma alitoa taarifa hiyo juzi wakati wa kikao cha waandishi wa habari cha kutambulisha shughuli za mradi wa uhifadhi wa mazingira ya baharini na pwani (MACEMP) kwa Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga.

Alisema samaki huyo alivuliwa usiku wa kuamkia juzi Jumatatu katika miamba ya kisiwa cha Nyuli na wavuvi wanaoendesha shuhguli zao kwenye pwani ya Sahari Jijini Tanga na baadaye idara ya uvuvi kupewa taarifa juu kuonekana kwake.

``Ilikuwa kazi kubwa kupata taarifa zake kwani kutokana na elimu tuliyoitoa mwaka jana juu ya samaki huyo na kutangaza kuwa ni nyara ya Serikali, waliomvua waliogopa kutuarifu wakidhani kuwa tutawakamata na kuwashitaki,`` alisema Hassan.

Mshauri huyo alisema siyo kweli kwamba Serikali itawafunga watakaobainika kumvua Silikanti ila wanapaswa kutoa taarifa na kumuwasilisha kwenye ofisi za dara ya uvuvi ili ufanyike mchakato wa kupeleka habari zake kwa wataalamu wa kisayansi katika nchi mbalimbali duniani kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

``Silikanti amekuwa akipasua vichwa vya wanasayansi ya viumbe wa baharini duniani kwa kuwa kuibuka kwake ni changamoto ya kisayansi kwani alishapotea tangu miaka 65 milioni iliyopita sasa wanachunguza kujua sababu za kuibuka tena,`` alisema Hassan.

Mtaalamu huyo alisema kumbukumbu zinaonyesha kwa mara ya kwanza kuibukia upya kwa samaki huyo tangu apote miaka milioni 65 iliyopita ni mwaka 1950 ambapo alivuliwa katika visiwa vya Commoro, mwaka 1982 akaonekana Malindi Mombasa na mwaka jana aliibukia kisiwa cha Nungwi Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa ya mtaalamu huyo ni kuwa elimu juu ya samaki huyo ilitolewa kwa wavuvi katika vijiji vilivyopo kwenye mwambao wa Mkoa wa Tanga, Septemba mwaka jana na kwamba matokeo ya utafiti wake uliofanyikia nchini Japan yameshawasilishwa ambapo Serikali inajiandaa kuutoa.



Source: Ibrahim Haule, Nipashe
 
kitu kilichopotea hakionekani, sidhani tatizo liko kwenye samaki! Hivi miaka hiyo milioni 65 wanasayansi gani walikuwa wanamtafuta? Kama kitu hukioni haina maana kimepotea na kwa vile samaki hawa wapo, ina maana wameendelea kuwepo kwa miaka milioni yote hiyo! Uumbaji ulimalizika na Mungu alishapumzika.
 
Hili bandiko linafaa lipelekwe kwenye jukwaa la Elimu ili liweze kujadiliwa kisayansi zaidi..
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom