Baada ya kupata hasra kilimo cha matikiti, sasa nalima bamia

Baada ya kupata hasra kilimo cha matikiti, sasa nalima bamia

fuvu la paka

Senior Member
Joined
Mar 29, 2015
Posts
133
Reaction score
76
Wakuu Tikiti linenitia hasara ya jumla ya mil 1.4.
Yaani Nigel hudumia sana lakini mwishowe limeniumiza sasa nalima Bamia so naomba kujua Soko la Bamia na ushauri tafadhari

Nimemaliza karibuni
Daaa Nina hasira sana
 
Ni nini kimepelekea upate hasara katika kilimo cha tikiti? Masoko ama?
 
Unataka hasara nyingine wewe, fanya utafiti kwanza au jifunze kuuliza swali, title yako ni kama vile ushafanya maamuzi yako
 
Hii tabia tunayo wabongo wengi sana hatupendi kufanya utafiti tunapenda kuigana tuu ukiona mwengine kafanya hiki na wewe unaenda kufanya kwa kuiga Mfano;kuna mdau nilimpatia taarifa ya mashamba ruvu kwakweli alikua na ujasiri ila hakujipanga kwa kufanya utafiti kuhusu soko la zao alilokwenda kulima matokeo yake kapata hasara tujaribu kufanya vitu vya kipekee bila kuigana Asante sana
 
Hii tabia tunayo wabongo wengi sana hatupendi kufanya utafiti tunapenda kuigana tuu ukiona mwengine kafanya hiki na ww unaenda kufanya kwa kuiga Mfano;kuna mdau nilimpatia taarifa ya mashamba ruvu kwakweli alikua na ujasiriila hakujipanga kwa kufanya utafiti kuhusu soko la zao alilokwenda kulima matokeo yake kapata hasara tujaribu kufanya vitu vya kipekee bila kuigana Asante sana
Mimi nilifungua duka,mtu kaja jirani naye kafungua duka hilo hilo, sasa tunagawana wateja na biashara imekuwa ngumu hasa, watanzania acheni kuigaiga jamani, tunajitengenezea ugumu wa biashara bure, mwisho wa siku kulogana, kwa nini usifungue biashara ya kutegemeana na kusupport nyingine? Mfano huyu anauza supu wewe uza chapati, soda na maji ya kunywa
 
Moja ya kufeli nipale unapoona upungufu wa bidhaa fulani sokoni na kukimbilia kulima au kufuga ni maumivu ukirudi sokoni kumbe wengi mlilima kupata faida kwenye chochote ni kujua tabia ya soko kwa mzunguko wa mwaka mzima
 
Mimi nilifungua duka,mtu kaja jirani naye kafungua duka hilo hilo, sasa tunagawana wateja na biashara imekuwa ngumu hasa, watanzania acheni kuigaiga jamani, tunajitengenezea ugumu wa biashara bure, mwisho wa siku kulogana, kwa nini usifungue biashara ya kutegemeana na kusupport nyingine? Mfano huyu anauza supu wewe uza chapati, soda na maji ya kunywa
kweli kabisa aise Mfano;China kuna viwanda vya kuzalisha equipment tu zitakazotumika katika viwanda vyengine hii inapelekea uzalishaji kutosimama kibiashara tunasema wame outsource kutegemeana kwa kumpa nafasi mtu mwengine mwenye ufanisi kuzalisha kitu ambacho ww haukua na ufanisi wa kutosha tukirudi kwenye mada siyo lazima wote tulime wengine tunaweza kufanya labelling,package au logistics etc
 
Inabidi uangalie pale penye consistent demand, kutokana na hali hasa miji kama Dar es Salaam demand ya pweza nasikia iko juu sana na wafugaji wanaangalia sato na kambale tu. Hebu wekeza kwenye ufugaji wa pweza uone!
 
Hilo ndo swali la msingi,jua kipi kimekuangusha ktk tikiti na ukifanyie kazi ili ukilima tena usipate hasara
 
Kwa kulima bamia sio suluhisho maana haujaelewa unataka kulima nini na kwanini,yaani unafanya bahati nasibu. Hasara ataendelea kuwa rafk yako
 
Hii tabia ya kupata hasara mara moja alafu una kimbia project husika,ni adui mkubwa sana wa mafanikio,umeshajua ulikosea wapi kwenye project yako ya matikiti? Hujawa tayar kusahihisha ulimo kosea? Hakuna tajir hata mmojaaliye kutana na changamoto kisha akazikimbia na akabaki kua tajiri,komaa na tikiti,correct mistakes utafanikiwa mkuu,kwa bahat mbaya fact nyingi za masuala ya kilimo mitandaoni huwa sio relevant,
 
Back
Top Bottom