Baada ya kunusurika kifo, Irene Uwoya aokoka!

Baada ya kunusurika kifo, Irene Uwoya aokoka!

Aiseee sasa ana kanisa hahahaha😂😂😂😂😂
 
Ameonna kamaliza madanga town na keshazeeka hana soko sasa kaamua kuwa tapeli wa dini. Kuna watu watakuwa kuni zetu.
 
Ameonna kamaliza madanga town na keshazeeka hana soko sasa kaamua kuwa tapeli wa dini. Kuna watu watakuwa kuni zetu.
Mbona hilo ni suala la hiyari jamani? Hakuna atakayelazimishwa kwenda kanisani anakohudumu.
 
Kwa hiyo kuokoka hua ni kama show ya kuwaonyesha wanadamu? Unatunza ushuhuda gani wakati anaye hukumu ni Mungu? Au mungu atahitaji ushuhuda wa binadamu kama vile yeye hajui? Kwani huwezi kumkataa shetani ikiwa wewe na Mungu wako tu ndio mkawa mnajua?
 
Mshindi namba 5 wa Miss Tanzania 2006, muigizaji na mjasiriamali Irene Pangras Uwoya, 35 amempokea Yesu kuwa bwana na mwokozi wa maisha yake!

Muigizaji huyo aliyezaliwa na kulelewa katika Ukatoliki, alifikia uamuzi huo baada ya kukumbwa na maswahibu yaliyotishia uhai wake.

Mjane huyo wa marehemu Ndikumana, ambaye walifunga ndoa takatifu ya Kikristo mwaka 2008 hadi walipotengana 2013, kisha kuolewa na Dogo Janja kwa ndoa ya Kiislam Oktoba 2017 kabla ya kutengana mwaka mmoja baadaye, anaonekana kweli kudhamiria katika imani yake hiyo mpya baada ya kuonekana akiwa amebadili mwenendo hadi wa mavazi yake!

CHANZO NI UZINDUZI WA FILAMU …!
Kama unafuatilia vyema tasnia ya filamu chini, utakuwa umesikia kuhusiana na ujio wa filamu mpya kutoka kwa muigizaji huyo, Olema ambayo ilizinduliwa Septemba 8 mwaka huu jijini Arusha.

Uzinduzi huo ulioambatana na mkusanyiko mkubwa wa nyota wakubwa kutokea tasnia hiyo na wengineo jijini hapo, ulifana kwelikweli!
Pesa ilitumika, pesa ikaonekana katika uzinduzi huo!

Irene aliyeonekana kuwekeza nguvu na pesa nyingi katika filamu hiyo, alikuwa na mipango mingi, ikiwemo uzinduzi katika majiji makubwa nchini.

Hata hivyo, mipango sio matumizi… Mipango hiyo ilivurugika alipotua jijini Mwanza kwa ajili ya maandalizi ya uzinduzi wa filamu hiyo jijini hapo, hali yake ya kiafya ilibadilika ghafla!

Hali ilikuwa mbaya sana, uamuzi wa haraka ukachukuliwa kumuwahisha Dar Es Salaam kwa ajili ya uangalizi zaidi wa kimatibabu.
Irene aliugua sana, hali iliyopekea kupungua kimwili.

USHIRIKINA WATAJWA…
Kama mjuavyo palipo na wengi pana mengi, kila mmoja ana lake juu ya kilichomkuta Uwoya katikati ya uzinduzi wa filamu yake hiyo aliyowekeza hela nyingi.

Irene aliyepokea sifa kedekede kutoka kwa wadau wa filamu nchini baada ya kuonesha njia ya mabadiliko na mapinduzi baada ya tasnia hiyo kudorora, inasemekana wenzie hawakupendezwa na hilo, wakafanya ya kufanya!

Tazama pichani, hapa ni kabla ya kuuguaView attachment 2855638


Baada ya kuugua… Huu ndio muonekano wake mpya.View attachment 2855639

KUOKOKA SIO KAZI…
Kumrudia Mungu ni jambo jema, na yafaa kupongezwa katika hilo. Lakini haizuii sisi kujiuliza kutokana na aina ya maisha yake iliyozoeleka…
Atadumu katika Ulokole? Vipi zile bata na machawa wake ndio zimekwisha? Aristoste na wenzie watafute cha kufanya mjini boss kaokoka?

Irene ameonesha mabadiliko katika matanuzi kwani hata birthday yake mwaka huu ambayo husheherekea kila mwaka ifikapo Dec. 18 haikuwa kama ilivyozoeleka wakati mwingine akikodi eneo zima la starehe na kufanya kufuru ya hela!
Tumuombee!


Kupitia chanzo changu cha kuaminika,

Nifah
Kahaba hili
 
Back
Top Bottom