Ni safari ndefu sana lakini mwisho imefanikiwa.
Nilianza kumfukuzia mwaka 1999 nikiwa darasa la nne, yeye akiwa darasa la tano. Kiukweli nilikuwa nampenda na yeye pia alikuwa ananipenda sana. Siku nisipomuona nilikuwa siwezi kulala kabisa usiku.
Hali ilikuwa mbaya zaidi alipomaliza shule mwaka 2001 na kuniacha darasa la sita. Kwa kweli nilitamani kuacha shule ili niende nikakae naye huko mtaani.
Nilijua fika hawezi kuchelewa kuolewa maana mtoto alikuwa mzuri sana. Na kumbuka tulikuwa wapenzi lakini hatukuwahi kufanya mapenzi licha ya kuchezeana tu. Kitendo hiki kiliniuma sana kuishia tu kushika mapaja ya mtoto mzuri.
Ni kweli matokeo yalipotoka tu akaolewa na mpaka muda huo sikuwahi kuwasiliana tena mpaka mwaka huu 2017!
Mi nilimaliza hiyo shule na kufaulu kuendelea na masomo hadi chuo na sasa nina mishe zangu hapa town.
Siku moja nikiwa kwenye kazi nikaona
call ya namba ngeni, kuuliza akajitambulisha ni Eliza my love wa enzi zile p/school.
Kwa kweli nilihisi moyo kupasuka kwa furaha. Nilimuita town amefika leo nikala tunda na kesho anarudi kwa mume wake huko mkoani. Najiona shujaa.
Sent using
Jamii Forums mobile app