baada ya kumchumbia ameanza kuniogopa

baada ya kumchumbia ameanza kuniogopa

kamati

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2013
Posts
240
Reaction score
109
Ndugu zangu nimekuja kwenu kutaka ushauri mimi ni kijana mwenye umri wa 26 years nimetokea kumpenda binti mmoja kiukweli kwa mtazamo wa macho yangu naona dunia nzima hakuna kama yeye.Basi mtoto wa kiume nikajitosa kuchana mistari kiukweli binti akaniambia niende kwao basi nikamwambia mzee wangu kwani sisi tamaduni zetu mzazi ndie anantole mahali basi tangu hapo binti ananiogopa sana yaani nikutana nae anazuka ameangusha kitu anainama hawezi kuniangalia usokwa uso sasa jamani nisaidieni hivi hiyo na nyinyi imewahi kuwatokea?na inasababishwa na nini?
 
...baadhi ya makabila hizo ndo mila zao, so sio hatari ni ishara ya kumheshimu mume mtarajiwa...
 
Ni kawaida kwa msichana kuwa na aibu mbele ya mwanaume anayemtaka kimapenzi! Na hasa kama ni bikra!
 
pole, kadiri yangu naona hamja jiweka karibu mkazoeana, mna mda gani toka hiyo mistari hadi kuwajulisha wazazi? mme do? kama bado ndo maana yuko vile ukichungulia tu baaasi. pia anaweza akawa anazuga tu, inamaa huo uzuri umeuona wewe tu wanaume wengine hawajaona?
 
yaani huyu sili mzigo nasubiri ndoa mwezi wa 12
 
Duh! Sidhani kama haya izo zitaleta maana kimantik!
May b ndio UCHIZI WAKE! Coz nilisikia kila mtu ni chizi, tunatofautiana viwango na matumizi tu!
 
Kula vitu hivo aibu zote zitaishaaa! (Did i just say that? Tell me i did not!)

Lara 1, sijui siku hizi ukoje...?? I don't want to believe you did.... This can't come out of Lara 1 I know JF-cally
 
ni heshima kwa husband to be umh



heshima! yawezekana anamuogopa jamaa, heshima haiko hivyo. Lakini mimi nahisi katafuta kitoto anakizidi miaka kadhaa kinaona aibu mtu sawa na uncle wake kukifuata!
 
Ulitaka akutolee macho kama fundi saa kadondosha funguo!!!!!!
 
yaani huyu sili mzigo nasubiri ndoa mwezi wa 12

Ni uamuzi mzuri nami nakushauri usile mzigo mpaka baada ya ndoa jambo hilo litakujengea heshima zaidi kwake na kuonyesha kuwa wewe si mtu wa papara kitu ambacho naamini ndivyo ulivyo.Mwezi wa 12 sio mbali ndugu haina haja ya haraka ya tendo hilo madhali mshaamua kuoana. Pia msisahau kupima. Kila la kheri na matayarisho ya harusi.
 
Hili ni kosa kubwa sana unafanya....kuassume kuwa mkioanamtakuwa ok. Baada ya miaka kadhaa ya ndoa, communication skills ni muhimu sana. Ndo maana wanasema marry the one who makes you laugh! Mie ningesepa hapo...sipendi mapozi!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom