Baada ya kufanyiwa upasuaji wa Tezi Dume, imerudi tena

Baada ya kufanyiwa upasuaji wa Tezi Dume, imerudi tena

tuko pamoja hiyo tiba inasaidia na wenye kansa pia.tunatoa elimu kutokana na mazingira uliyopo.kumbuka pia majani ya mchunga ni tiba halali kabisa ya tezi dume inayoanza.
Yanatumika vipi, fafanua kiongozi
 
Nashindwa kuelewa baada ya kusumbuliwa na tezi dume nikafanyiwa upasuaji mambo yakawa Safi.

Baada ya muda takribani mwaka imerudi tena nini chanzo au upasuaji ulifanywa kwa juu juu tu.

Msaada madokta
Tafuta tiba asili tu. Bahati mbaya nikaumwa hiyo siwezi kufanya upasuaji. Nimeshuhudia mambo ya ajabu kwa wengi niliowajua waliofanyiwa upasuaji. Huo utaalam kwa hapa kibongo bongo bado
 
Kama huna jibu potezea. Hivi kuna hospitali ndogo wanaofanya upasuajiwa tezi dume? Huo upasuaji kafanyiwa hospitali kubwa. Hapa kauliza uashauri na mwongozo na hapa kuna wataalamu dunia nzima wanaweza wakampa mwongozo sahihi. Hivi ulishawahi kwenda hizo hospitali unazoziita kubwa? Wengi wanaohudumia wagonjwa ni Wanafunzi wa inteinship . Wale wabobezi wanazunguka duniani kutoa semina na warcsha. Ila sasa kwenye malipo na dawa utaambiwa mfumo nenda pale nenda pala. Hii kesi ya tezi dume kujirudia nimesikia nyingi inahitaji mjadala wa kina kwa wataalamu wa afaya/ urology
Wewe ni kilaza tena useless asshole, yaani mtu na professional yake aje kumsaidia mgonjwa kwa kupost JF..? Wewe ni idiot
 
Ww endelea na kuzunguka kwnye mahospitali wakati dawa unayo uwanjani kwako.tunakupa bure ushauri ukitaka unachukua.weng tu wamepona kwa majani mchunga na wengne kwa style yao.c lazima tiba ifanane MUNGU AMETOA TIBA KILA SEHEMU KWA AINA YA MITI ILIYOPO HAPO
Wewe Unasumbua bure na hizo Tiba zako. Unajua sababu za Tezi dume kuvimba?

Kuna sababu nyingi moja ikiwa ni maambukizi, uvimbe kama cysts au Kansa na kila tatizo lina Tiba yake.

Jinsi ya kujua kama mtu tezi dume limevimba unachukuliwq damu kuangalia
PROSTATIC SPECIFIC ANTIGEN (PSA); kama ni zaidi ya 4, hapo jua kuna tatizo.

Tatizo la Tezi dume linaangaliwa hivi:-

PSMA-PET Scan kikijumuishwa na MRI ya tezi dume. Kipimo hiki kina uwezo mkubwa wa "kumulika" na kuonyesha sehemu ndogo kabisa ya seli za tezi dume zilizojificha na zinazosababisha PSA ipande, hata kama ziko microscopic.

Ukishajua ndipo inachukuliwa biopsy katika sehemu hiyo yenye uvimbe ili kubaini tatizo linalosababisha tezi dume kuvimba.

Watch out, siyo kuwa wanachukua kinyama kimoja, wanachukua vingi ki Takwimu baada ya kuwa na strata ya hako ka uvimbe. Ili vinyana vipepekwe kwa pathologist abaini tatizo.

Kama una swali, uliza maana mimi ni mhanga wa hii kitu na mpenzi wa Tiba mbadala.
 
…i. Nimeshuhudia mambo ya ajabu kwa wengi niliowajua waliofanyiwa upasuaji. Huo utaalam kwa hapa kibongo bongo bado
upo 100% sahihi kwa hapa TZ, ingawa vifaa vipo. Watu wanatibu blindly tu. Daktari anaona PSA inapanda, anasema bado haijafika 10! What!!!!! PSA haiwezi kupanda bila sababu
 
Kikwete alienda kufanyiwa nje.

Watu wakatania kwamba ameogopa kuchunguliwa Tanzania na kupimwa kwa kidole.

Turns out yaweza kua alijua huku bado tunajikongoja kwenye surgery.

Rudi hospital tezi dume hugeuka kua kansa. Achana na JF rudi hospital
 
tuko pamoja hiyo tiba inasaidia na wenye kansa pia.tunatoa elimu kutokana na mazingira uliyopo.kumbuka pia majani ya mchunga ni tiba halali kabisa ya tezi dume inayoanza.
Ndugu yangu, kwanza elewa kuwa Kansa kwa sasa si tatizo kubwa. Management ya Kansa ndilo jibu ya Kansa.

Utatibu Kansa bila kujua Gleason Score? Au kujua Kansa ipo wapi? Je, Unajua miili ya binadamu siyo homogenous ni heterogenous?

Unajua kadri unavyochelewa kuua hizo cell ndipo zinasambaa?
 
Wewe ni kilaza tena useless asshole, yaani mtu na professional yake aje kumsaidia mgonjwa kwa kupost JF..? Wewe ni idiot
wapo watu walipsaidiwa mambo makubwa na mazito zaidi ya unsvyofikiri wewe dada unayeishi mjini kwa kupiga miti
 
Ugonjwa wa tezi dume kuvimba Papillon 1906 ni ugonjwa wa Gharama ila kwa mwanaume ukifika 50, ni wachache wanaukwepa.

Kwa ushauri wangu dawa ya Gharama ndogo ingawa ina madhara makubwa ni kuiondoa tu. Gharama za kuiondoa ni pamoja na uhanithi kama urologist hana vifaa vya kumuongoza ili asidhuru nerves za kusimamisha. Ili baadaye uendelee kuzila K kwa dry ejaculation.
 
Kikwete alienda kufanyiwa nje.

Watu wakatania kwamba ameogopa kuchunguliwa Tanzania na kupimwa kwa kidole.

Turns out yaweza kua alijua huku bado tunajikongoja kwenye surgery.

Rudi hospital tezi dume hugeuka kua kansa. Achana na JF rudi hospital
Hospital kwa hapa Tz hawawezi kufanya hicho kitu jamaa yangu. Niamini. Simtishi ila anaweza kufanyiwa halafu anaweza akadumu siku kadhaa,halafu ikawa ndio nitolee. Kwanza hata alivyofanyiwa hiyo nyingine mpaka sasa yuko hai ni Jambo la kushukuru
 
Ugonjwa wa tezi dume kuvimba Papillon 1906 ni ugonjwa wa Gharama ila kwa mwanaume ukifika 50, ni wachache wanaukwepa.

Kwa ushauri wangu dawa ya Gharama ndogo ingawa ina madhara makubwa ni kuiondoa tu. Gharama za kuiondoa ni pamoja na uhanithi kama urologist hana vifaa vya kumuongoza ili asidhuru nerves za kusimamisha. Ili baadaye uendelee kuzila K kwa dry ejaculation.
Ndio maana marehemu mkwe wangu alikataa kabisa operation

Sasa dry ejaculation,je unapata raha kama ile ya awali?
 
upo 100% sahihi kwa hapa TZ, ingawa vifaa vipo. Watu wanatibu blindly tu. Daktari anaona PSA inapanda, anasema bado haijafika 10! What!!!!! PSA haiwezi kupanda bila sababu
Waliletwa vijana kuja kufanyia mazoezi hicho kitu huku wilayani. Watu wengi walijitokeza kurekebishwa hiyo. Waliondoka watu sana. Kila akifanyiwa anakuwa vizuri si zaidi ya wiki 2,baada ya hapo anazidiwa nitolee.

Baba mkwe wangu amefanyiwa hospital kubwa tu ya rufaa. Japo alikuwa mtu mzima lakini baada ya hapo hakuwahi kutulia. Apumzike kwa amani.
 
Nashindwa kuelewa baada ya kusumbuliwa na tezi dume nikafanyiwa upasuaji mambo yakawa Safi.

Baada ya muda takribani mwaka imerudi tena nini chanzo au upasuaji ulifanywa kwa juu juu tu.

Msaada madokta
Nje ya mada hivi ukifanyiwa op ya tezi dume unaweza kupiga mzigo.
 
Waliletwa vijana kuja kufanyia mazoezi hicho kitu huku wilayani. Watu wengi walijitokeza kurekebishwa hiyo. Waliondoka watu sana. Kila akifanyiwa anakuwa vizuri si zaidi ya wiki 2,baada ya hapo anazidiwa nitolee.

Baba mkwe wangu amefanyiwa hospital kubwa tu ya rufaa. Japo alikuwa mtu mzima lakini baada ya hapo hakuwahi kutulia. Apumzike kwa amani.
Watu wengi wanaondoka kutokana na uzembe wa madaktari. Nasema hapa Tanzania, Daktari anajifanya Mungu Mtu!!!! Hii ndilo tatizo. Hujui ni nani anajua na nani anajifunza. Haya masuala yanahitaji umakini sana. Na madaktari ambao wapo Muhimbili dakika hii, wakati Aga Khan wanamsubiri na pia anatakiwa Rabinisia, hawezi kuwa makini.
 
ERTUGRUL BEY kwa kuongeza, siyo lazima kwa sasa kufanyiwa upasuaji.

Njia za kutibu hii kitu ipo katika makundi mawili 1. Radical Prostatectomy (upasuaji) na 2. Radical Radiotherapy (Kutokupasua).

Upasuaji nao upo katika makundi matatu
i. Open ya kawaida,
ii. Laparoscopic, na
iii. Robotics. Hii ndiyo kiboko yake ingawa ni gharama

Radical Radiotherapy ipo katika njia kuu 6 kwa ubora wake:
i. External Beam,
ii. IMRT,
iii. IGRT,
iv. Cyber Knife,
v. Brachytherapy, na
vi. Proton.

Hivyo kikubwa ni kwanza kujua mwili wako hususan mtu akifika miaka 50 kwa kuangalia PSA ambayo kawaida huwa ni 0-4. Ikizidi hapo, ingawa watu wanadai uzee nao huchangia, to be on the safe side, tafuta kwa nini PSA inapanda na most likely ni vicell vya Cancer vinaanza kukunyemelea.

Onyo: Mimi si daktari wa kutibu binadamu ila ni mhanga wa hii kitu, hivyo sizungumzi kutokana na theories za kusoma vitabuni au kuona wagonjwa bali nimeyapitia
 
Hospital kwa hapa Tz hawawezi kufanya hicho kitu jamaa yangu. Niamini. Simtishi ila anaweza kufanyiwa halafu anaweza akadumu siku kadhaa,halafu ikawa ndio nitolee. Kwanza hata alivyofanyiwa hiyo nyingine mpaka sasa yuko hai ni Jambo la kushukuru
Ila kuna vituo vimespecialise kwenye tezi dume. Nafikiri pana msaada sana sehemu hizo
 
Back
Top Bottom