Baada ya kuacha kazi ngumu ya kuajiriwa, online jobs (Upwork na Fiverr) zilivyobadilisha maisha yangu

Ila Wabongo mko soooooo negative aiseeee, Apps ziko hapo na ame-screenshot, unapata tabu Gani kuingia Play store ukajionea? Na kama unaona unapigwa si unaachana nayo tu? Kwanini tumkatishe tamaa mtu aliyejitolea kutuelimisha?
Wabongo ndivyo walivyo ni wavivu sana wa kufanya uchanganuzi wa mambo na kuupata ukweli.
Wanamcrush mtu bila kufuatilia
 
Bongo kwenye hizi online issues imekua tatizo sana sana.

Binafsi nilishawahi kumuamini mchizi na kweli mpaka leo napata pesa kirahisi kabisa.

Nitakuchek whatsapp mkuu, acha wanaobeza waendelee kubeza.
Hii inasababishwa na wajinga wengi kupigwa za uso na kusambaza chuki kuhusu hizi online platforms.
 
watanzania hatuna elimu hatuna kujiamini alaf kila tunachoona basi tunakibeza ndio maana hata mafuta yakipanda kwa shilingi mia bas utakuta mijitu inalalama mpka inapaki vi ist nyumbani acheni ujinga sio kila jambo lazima ubeze mtandaoni ww fanya uchunguzi wako ukiona halina maana kwako basi achana nalo ila kubeza wakati mtu kwa siku hata hyo buku haiingii mfukoni ni ukosefu wa akili
 
Mimi huwa nafanya vijikazi vidogo vidogo kwenye microworkers, nilisha jaribu up work na fiver nikaona kweli Huko kuna kazi za hela nying ila inakupasa uwe na skills zaidi ya moja ili kuendana na huitaji wa clients, account yangu ya microworkers ina zaidi ya dola 80 na zaidi kidogo, nikikomaa vyema huku nita rudi up work or fiver, pia kuna zile ppc (pay per click) unaweza kupata cent 20 kwa ku click Tangaz au kuchek video, ila hapo hadi ufikishe kiwango kilichowekwa ili uweze ku withdraw ambacho ni 50 usd utakuwa ume choka kabisa, ila kweli hela ndogo ndogo zipo.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Mkuu microworkers umesha withdraw? Walikutumia pin?
 
I don’t know kwa nini watu wamekuja na negative thoughts sana na wakati mtu kaeka NB kabisa hataki ela . Nadhani kuna haja ya mtu kufanya uchunguzi kabla ya kuja kumchafua mtu jukwaani..
Izi apps ziko nyingi kuna upword,fever, freelancer, au hata linkedin. Izi apps mtu unaomba kazi kutokana na ujuzi wako ulio nao, kwa mfano ukienda upwork ukasema maybe let’s say copywriter watakupa test ili kuona ukomavu wako. Baada ya hapo kuna mtu ambae ni client wanatokea nchi nyingi yeye anaeka kazi yake na anaweka dau lake baada ya hapo waombaji ni wengi yeye ndio atamchukua mtu kutokana na rating zake . Kwa mliopanda uber au bolt mnajua vigezo mnavyotumia kuchagua dereva basi na hizi apps ndio ziko the same .
Sijaona haja ya mtu kukimbilia kufikiria kupigwa akati umepewa jina la apps na unaeza kwenda youtube ukaenroll kwenye free course na ukatumia mb ambazo ungeenda kupoteza kwenye app ya mange kimambi.
 
mueleweni,mnavyoweza kumuelewa
nyuzi za hivi zipo nyingi humu
mimi nilianza mwzi wa 5 hadi sasa niearn dola 36
kuna kazi 2 ,moja ya dola 120 na nyingine 420 nazifanya( Ingawa ni ngumu kidogo kuzimaliza lakini napambana nazo)
kabla ya kumshutumu mtu piia google/youtube uhakikishe
au kama upo twiter mcheki jamaa anaitwa mafole baraka.

Safi kabisa ila sisi watanzania apps za muhimu watu wanaleta matusi ila zile za kina mange kimambi wanakimbilia hadi kulipia kabisa
 
I don’t know kwa nini watu wamekuja na negative thoughts sana na wakati mtu kaeka NB kabisa hataki ela . Nadhani kuna haja ya mtu kufanya uchunguzi kabla ya kuja kumchafua mtu jukwaani..
Izi apps ziko nyingi kuna upword,fever, freelancer, au hata linkedin. Izi apps mtu unaomba kazi kutokana na ujuzi wako ulio nao, kwa mfano ukienda upwork ukasema maybe let’s say copywriter watakupa test ili kuona ukomavu wako. Baada ya hapo kuna mtu ambae ni client wanatokea nchi nyingi yeye anaeka kazi yake na anaweka dau lake baada ya hapo waombaji ni wengi yeye ndio atamchukua mtu kutokana na rating zake . Kwa mliopanda uber au bolt mnajua vigezo mnavyotumia kuchagua dereva basi na hizi apps ndio ziko the same .
Sijaona haja ya mtu kukimbilia kufikiria kupigwa akati umepewa jina la apps na unaeza kwenda youtube ukaenroll kwenye free course na ukatumia mb ambazo ungeenda kupoteza kwenye app ya mange kimambi.
Elimu ya tanzania imezalisha kizazi flani hivi hakijui kujiongeza wala Kufanya tafiti binafsi kuhusu jambo flani.

Ni elimu ambayo imezalisha vijana ambao Wao Wako nyumA Sana kuhusu masuala yanayoendelea duniani. Hadi unajiuliza Hadi 2020 msomi WA TANZANIA tena chuo kilicho mjini kama UDSM hajui Upwork wala Fivver katika ulimwengu huu WA changamoto za Ajira.


Anyway maisha ni kuchagua Acha niishie hapa. Wale vijana mnaotaka kujifunza tumieni simu zenu vizuri kila kitu kipo mikonon mwenu hamta pigana na Ajira za TAMISEMI. Kuweni watafuti na wadadisi basi tafuteni hata marafiki Kenya au South au Nigeria mbadirishane mawazo mtaona mlivyo weupe kichwani.

Niishie hapa
 
Jf kuna wasomi wajingaa mtu hawezi ata kuingia Google ukajirizisha platform za kufanya kazi zipo nyingi sana. Muhimu kutambua hakuna pesa rahisi tunapambana mno kuzipata ata 5$ haipatikan kirahsi but fursa zipi ata mimi nilianza na 0$.
Screenshot_20220226-153512_Freelancer%20-%20Upwork.jpg
Screenshot_20210728-154246_Freelancer%20-%20Upwork.jpg
Screenshot_20210525-180500.jpg
 
Upwork na fiver ni site ambazo watu wenye account wanapost kazi kutafuta ma freelancer wa kuzifanya wenye ujuzi husika hakuna wizi wala utapeli hizi ni site zinazotambulika kisheria,na kufungua account ni kipengele hasa upande wa upwork,ninayo account ya upwork lakini kupata kazi ndio mziki nahisi inabidi u upgrade account yako ili uweze kupata kazi kirahisi ila kazi ni nyingi sana...kuna kijana anaitwa Baraka mafole nilikuwa namfatilia sana twitter alisaidia pakubwa kuweza kufungua account upwork,ili kupata kazi inabidi uwe na ujuzi wa kutosha wa kazi unayotaka kufanya maana mnashindana na wahindi,wanaijeria,wapakistan,wazungu n.k

Upwork ni sehemu kimbilio kwa watu wasio na ajira ila sharti uwe na ujuzi kama ulipe orodheshwa hapo juu na mtoa mada...sema wabongo wengi hutumia njia hii kuingiza pesa kwa kufundisha watu au kuwatapeli baada ya wao kujua..kifupi tuna roho mbaya.
 
Back
Top Bottom