Baada ya ku-trend Kimataifa, kamanda wa kubadili upepo hatimaye upepo umembadilikia!

Trust None

JF-Expert Member
Feb 12, 2018
1,260
4,415
Kukiwa na tukio linaloteka nyoyo na hisia za watu basi huyu jamaa huja na "kituko" kama utani vile kwa lengo la ku-'divert ideas' za watu na kuwasahaulisha kabisa kile walichokuwa wakijadili.

Sasa upepo umembadilikia.... Fuatilia...

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amezitaka mamlaka husika kuchukua hatua za kisheria kwa anayehusika na uhalifu wa kimtandao wa kutumia jina lake kwenye ukurasa wa Twitter.

Makonda ametumia ukurasa wake wa Instagram kukanusha kuhusika na taarifa inayosambazwa katika mtandao huo juu ya wanaolaghai wanawake na kudai kuwa hana akaunti kwenye mtandao wa Twitter wala Facebook isipokuwa Instagram kwa jina la Baba Keagan.

“Naomba kuutaarifu umma kwa mara nyingine tena. Mimi Paul Makonda Mkuu wa Mkoa sina A/c TWITTER hata FACEBOOK. Mtu anaetumia jina langu ana malengo mabaya tena Kwa faida iliyojaa uovu.”

“Naziomba mamlaka zinazohusika kuchukua hatua kwani kunasiku atatoa kauli itakayoleta taharuki katika jamii. A/c pekee ni nayo tumia ni ya Instagrame tena Kwa jina la baba_keagan.”

Screenshot_20190814-195720.png


Lengo ni lilelile kuwatoa watu kwenye reli.
 
Inaonekana hajui vipaumbele vya kazi zake hebu nimtajie baadhi yake tu
1. Ulinzi na usalama wa mkoa, akomeshe vitendo vya kutekwa watu n.k.
2. Makusanyo ya mapato katika mkoa wake
3. Kuhakikisha watoto wote wanapata elimu bora - nyumba za walimu, madarasa, madawati, vitabu, n.k.
4. Maji safi na salama,
5. Umeme
6. Takataka katika jiji la Dar
7. N.k. ndoa za watu awaachie wengine hilo siyo la muhimu kwake
 
Back
Top Bottom