#COVID19 Baada ya kampeni ya chanjo za COVID-19 kudoda, Askofu Gwajima kuwa mbuzi wa kafara?

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,976
Kinachoendelea serikalini na bungeni ni kutafuta mbuzi wa kafara baada ya “utapeli” wa serikali kuhusu chanjo za korona kushtukiwa na wananchi wengi nchini.

Fikiria chanjo za watu milioni moja ambazo serikali ilipokea kama “msaada” kutoka Marekani mpaka sasa zaidi ya nusu yake bado ziko kwenye “magodauni” zikisubiri watanzania kujitokeza kwenda kupata hizo chanjo!

Kibaya zaidi hizi chanjo za korona zinahitaji uangalifu wa hali ya juu katika utunzaji ili zisiharibike. Kwa sasa ni mwezi mmoja na wiki mbili tokea serikali ilipopata hizi chanjo!

Chanjo za Johnson and Johnson zinapozalishwa zina expire baada ya miezi 4. Kuna uwezekano wa wananchi huko vijijini kupewa chanjo ambazo zime expire au zimeharibika kutokana na utunzaji mbaya.

Ieleweke kuwa chanjo hizi zinatakiwa kwa muda wote ziwe kwenye jokofu(fridge) lenye joto kati ya 2°C na 8°C (36°F na 46°F). Kwa umeme huu wa mgao au majokofu “spear mkononi” kuna uwezekano mkubwa kwa chanjo kuharibika!

Juzi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam alitoa wito kwa wakazi wa Jiji la Dar Es Salaam na viunga vyake wajitokeze kwenye uwanja wa uhuru kupata chanjo bila kujali makundi yao lakini mwitikio ulikuwa ni hafifu sana hasa ikichukuliwa Jiji la Dar es Salaam lina watu zaidi ya milioni 6 na wengi wana uelewa na ufahamu zaidi.

Huko mikoani ni aibu tupu kwa serikali kwa sababu watu hawaendi kuchanjwa pamoja na kwamba serikali imelipa vyombo vya habari ili vihamasishe watu kwenda kuchanja.

Serikali inatumia nguvu nyingi bila maalifa katika kutimiza malengo ambayo wananchi wengi wameyakataa kimya kimya huku wachache kama Askofu Gwajima wakipaza sauti zao.

Kwa sasa mpaka bunge linaanza kutumia nguvu kuisaidis serikali kuwafumba mdomo baadhi ya wananchi/wabunge wanaotoa sababu za kutochanja.

Yaani serikali haitaki mtu aeleze kwa sauti sababu zinazomfanya asichanje lakini serikali hiyo hiyo inataka waliochanjwa wajipige picha/video na kueleza kwa sauti kwa nini wanachanja.

Kama chanjo ni hiari, kwa nini wizara ya afya inatumia pesa za watanzania wote kuwahamasisha watanzania kuchanja chanjo ambazo mpaka sasa zimeleta mgawanyiko mkubwa huko zinakotoka. Kwa lugha nyingine, serikali inatafuta soko la chanjo kwa kutumia pesa na rasilimali za wananchi.

Neno hiari kwa sasa linageuzwa kuwa LAZIMA eti kwa sababu Rais wa Tanzania amechanja.

Kuna Mbunge mmoja anasema eti maneno ya Askofu Gwajima ya kupinga chanjo yanaweza kusababisha serikali ya Rais Samia kupinduliwa! Eti akamatwe kwa kosa la uhaini! Huyu ni aina ya mbunge anayesababisha bunge zima kuonekana kama limejaa wabunge ambao uwezo wao wa kupambanua na kuchambua mambo ni finyu!

Kinachoendelea nchini kuhusu chanjo kinadhihilisha Watanzania sio wajinga au “sell-out”.
 
Magufuli ameshakufa kijana. Tafuta namna nyingine ya kuishi.

Tanzania kuna chanjo zaidi ya 60..

Kila siku wanawakae na watoto wanapokea chanjo kila iitwapo siku na tena wasipozipata wanalalamika.

TT pekee inatolewa mpaka shots nne na watu wanaipata.

Kampeni ya COVID imekuwa ngumu kwasababu ha athari za akili ya kibwenhmgo Magu alizoacha.

Hata CCM wenyeqe naamini wamejifunza siyo kila mtu anaweza kuwa Rais. Magu was a total disaster.
 
Mkuu maelezo yako mazuri sana.

Mleta uzi ni masalia ya lile chizi la chato.

Mpaka leo hawaamini kama amekufa na hatorudi milele.
 
Kinachoendelea serikalini na bungeni ni kutafuta mbuzi wa kafara baada ya “utapeli” wa serikali kuhusu chanjo za korona kushtukiwa na wananchi wengi nchini.

Fikiria chanjo za watu milioni moja ambazo serikali ilipokea kama “msaada” kutoka Marekani mpaka sasa zaidi ya nusu yake bado ziko kwenye “magodauni” zikisubiri watanzania kujitokeza kwenda kupata hizo chanjo!

Kibaya zaidi hizi chanjo za korona zinahitaji uangalifu wa hali ya juu katika utunzaji ili zisiharibike. Kwa sasa ni mwezi mmoja na wiki mbili tokea serikali ilipopata hizi chanjo!

Chanjo za Johnson and Johnson zinapozalishwa zina expire baada ya miezi 4. Kuna uwezekano wa wananchi huko vijijini kupewa chanjo ambazo zime expire au zimeharibika kutokana na utunzaji mbaya.

Ieleweke kuwa chanjo hizi zinatakiwa kwa muda wote ziwe kwenye jokofu(fridge) lenye joto kati ya 2°C na 8°C (36°F na 46°F). Kwa umeme huu wa mgao au majokofu “spear mkononi” kuna uwezekano mkubwa kwa chanjo kuharibika!

Juzi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam alitoa wito kwa wakazi wa Jiji la Dar Es Salaam na viunga vyake wajitokeze kwenye uwanja wa uhuru kupata chanjo bila kujali makundi yao lakini mwitikio ulikuwa ni hafifu sana hasa ikichukuliwa Jiji la Dar es Salaam lina watu zaidi ya milioni 6 na wengi wana uelewa na ufahamu zaidi.

Serikali inatumia nguvu nyingi bila maalifa katika kutimiza malengo ambayo wananchi wengi wameyakataa kimya kimya huku wachache kama Askofu Gwajima wakipaza sauti zao.

Kwa sasa mpaka bunge linaanza kutumia nguvu kuisaidis serikali kuwafumba mdomo baadhi ya wananchi/wabunge wanaotoa sababu za kutochanja.

Yaani serikali haitaki mtu aeleze kwa sauti sababu zinazomfanya asichanje lakini serikali hiyo hiyo inataka waliochanjwa wajipige picha/video na kueleza kwa sauti kwa nini wanachanja.

Kama chanjo ni hiari, kwa nini wizara ya afya inatumia pesa za watanzania wote kuwahamasisha watanzania kuchanja chanjo ambazo mpaka sasa zimeleta mgawanyiko mkubwa huko zinakotoka. Kwa lugha nyingine, serikali inatafuta soko la chanjo kwa kutumia pesa na rasilimali za wananchi.

Neno hiari kwa sasa linageuzwa kuwa LAZIMA eti kwa sababu Rais wa Tanzania amechanja.

Kuna Mbunge mmoja anasema eti maneno ya Askofu Gwajima ya kupinga chanjo yanaweza kusababisha serikali ya Rais Samia kupinduliwa! Eti akamatwe kwa kosa la uhaini!

Kinachoendelea nchini kuhusu chanjo kinadhihilisha Watanzania sio wajinga au “sell-out”.
Kwahiyo unaona hiyo ni sifa au ujinga uliotopea? Akili nyingine bwana.
 
Magufuli ameshakufa kijana. Tafuta namna nyingine ya kuishi.

Tanzania kuna chanjo zaidi ya 60..

Kila siku wanawakae na watoto wanapokea chanjo kila iitwapo siku na tena wasipozipata wanalalamika.

TT pekee inatolewa mpaka shots nne na watu wanaipata.

Kampeni ya COVID imekuwa ngumu kwasababu ha athari za akili ya kibwenhmgo Magu alizoacha.

Hata CCM wenyeqe naamini wamejifunza siyo kila mtu anaweza kuwa Rais. Magu was a total disaster.
Kama ilivyo kawaida yenu na wauza chanjo, badala ya kushambulia hoja kwa nguvu za hoja badala yake unashambulia mleta hoja kwa matusi na hoja za nguvu.

Mimi nikitafuta namna nyingine ya kuishi hujui kuwa na wewe itabidi utafute namna nyingine ya kuishi kwa sababu inaonekana maisha yako yanategemea uwepo wa mada zangu hapa Jamiiforums ili uzijibu hata kwa hoja za kijinga kama ulivyofanya ili upate ujira wako!

Eti kwa sababu kuna chanjo zaidi ya 60 kwa hiyo wananchi walazimishwe hata chanjo ambazo zimeleta mgawanyiko mkubwa kwa wataalam kule zinakotoka.

Hujui kama chanjo zingine mpaka kupewa binadamu zilipitia mfumo unaotambuliwa kimataifa ambao pia sio mfumo unaotumika sasa wa “emergence administered” ambao dhumuni lake kuu ni uchumi kwanza?
 
Yule "Hero" wako
kichwa ngumu ndie chanzo cha yote, apumzike anapostahili, alifundisha wengi ujinga mwishowe ukamrudia mwenyewe.

Kama “hero” wangu alifundisha ujinga, kwa nini wasio wajinga wameshindwa kuondoa ujinga kwa waliofundishwa ujinga?

Yaani wewe usiye mjinga unashindwa kuondoa ujinga kwa aliye na ujinga! Hapa nani ni mjinga zaidi!

Unaweza usijue mantiki ya ulichokiandika lakini kwa kukusaidia umezidi kukoleza hoja yangu kuwa Rais Magufuli aliaminiwa na watu wengi na kwa sababu hiyo alikuwa na political legitimacy sio nchini pekee bali duniani.

Halafu lazima uelewe na kujua kuwa askari mzuri ni yule anayekufa vitani akiwapigania wengi! Pres Magufuli died a hero and not in vain.
 
Magufuli ameshakufa kijana. Tafuta namna nyingine ya kuishi.

Tanzania kuna chanjo zaidi ya 60.

Kila siku wanawakae na watoto wanapokea chanjo kila iitwapo siku na tena wasipozipata wanalalamika.

TT pekee inatolewa mpaka shots nne na watu wanaipata.

Kampeni ya COVID imekuwa ngumu kwasababu ha athari za akili ya kibwenhmgo Magu alizoacha.

Hata CCM wenyeqe naamini wamejifunza siyo kila mtu anaweza kuwa Rais. Magu was a total disaster.
Kichwa chako kinatakiwa kipelekwe gereji.
 
Kama “hero” wangu alifundisha ujinga, kwa nini wasio wajinga wameshindwa kuondoa ujinga kwa waliofundishwa ujinga?

Yaani wewe usiye mjinga unashindwa kuondoa ujinga kwa aliye na ujinga! Hapa nani ni mjinga zaidi!
Mjinga zaidi ni yule aliyekuwa na mamlaka makubwa badala ya kuyatumia positively akaenda kuwaambia watu mapapai yetu yana Corona, nawe kibaraka wake ukashangilia; kwa ujinga wenu ulimwengu wote ukatucheka.

Haiwezekani ule ujinga wenu mliosambaza kwa miaka kadhaa uje kufutika kwa miezi michache, it will take time.

Magufuli aliaminiwa na wengi kwa sababu alikataa mawazo tofauti na yake, alitaka asikilizwe yeye pekee kwa kila ujinga ataoongea, ndio maana wengi wamepotezwa wakati wa utawala wake, askari anayekufa vitani kwa kupigania ujinga mpe salaam.
 
Kwenye chanjo serikali imechemka big time.

Juzi wizara ya afya imesema kwa mwezi mmoja ama siku 32 watu 304,000 ndio walikua wamechanja, kwa maana kua ndani ya mwezi mmoja chanjo ni 33% tu zimetumika.

Kwa hesabu ya haraka chanjo milioni za msaada zitahitaji miezi 3 kumalizika wakati hizo chanjo haijulikani zilizalishwa lini hadi kufika Tanzania na hadi kumalizika zitakua na miezi mingapi, watu watapewa expired shots.

Iwapo mpango wa covax ni kutusaidia chanjo milioni 12, maana yake tutahitaji miezi 36 kuzimaliza hizo chanjo za covax, miaka 3 na ushee. Na wataalam wanashauri ili kujihakikishia ulinzi angalau uchanje 70% ya raia wako, kwa Tanzania ni kama milioni 40, hiyo tutahitaji miaka 10 kumaliza kuchanja 70% ya raia wote.

Hesabu za chanjo zinagoma, tumeingia mkenge wa kukubali kukopeshwa trilioni 2 za kununua madawa ya chanjo lakini iko wazi huu ni usanii.
 
Ukiwa kiongozi ukazungukwa na wanafiki wengi. Ni ngumu kufanikiwa.

Mama ana wasaidizi ambaohata huna uhakika kama wanafanyakazi kwa dhati, au bora liende.

Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
Uaminifu? Oh kumbe unamaanisha uaminifa ahhaaa haya ndo yalimpata jpm wetu , zamu kwa zamu aliishi na maadui bila kujua.

Zamu kwa zamu
 
Back
Top Bottom