Baada ya Kalenga, sasa CCM kurejesha jimbo la Iringa mjini

Baada ya Kalenga, sasa CCM kurejesha jimbo la Iringa mjini

kwa hiyo majimbo yote ya mijini ni ya cdm?

watu duni tu ndiyo wanaweza kuchagua ccm ! Kumbuka mijini hakuna watu wa hivyo , nani wa kumnunua kwa wali kitumbo na maharage ? Kuna tetesi kwamba ccm itaipoteza DSM yote 2015 !
 
kimewauma alivyo onyesha wafanyabiashara wa meno ya tembo n akina nan nchi hii.....wakat ikulu imeatamia majina bila kuyafanyia chochote.....dhaifuuuuuu chakavuuuuu
 
watu duni tu ndiyo wanaweza kuchagua ccm ! Kumbuka mijini hakuna watu wa hivyo , nani wa kumnunua kwa wali kitumbo na maharage ? Kuna tetesi kwamba ccm itaipoteza DSM yote 2015 !

aisee that is very possible....sisi tunaokaa huku mtaan ndo tunajua kinachoendelea.....mind set za wakaz weng zimebadilika sana...juz kariakoo mvua zmenyesha maji machafu yakatapakaa jamaa wakasema hii ni kaz ya uongoz imara wa ccm.....
hehehehehehe!!!!
 
wakati wao wanawaza Iringa mjini,sisi wasukuma wa kanda ya ziwa hasa mkoa wa Mwanza tumejipanga kuyachukua majimbo yote mikononi mwa hawa wakoloni weusi,pia,tutakomesha uhuni wa magamba uliofanywa na magamba kwa kushirikiana na mamluki wao Matata kwa kuchagua madiwani wote kutoka CDM!
 
BAADA ya kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Kalenga, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimesema kinajiimarisha zaidi kirejeshe mikononi mwake, Jimbo la Iringa mjini mikononi mwake. Jimbo la Iringa Mjini linaloongozwa na Mchungaji Peter Msigwa aliyechaguliwa mwaka 2010 kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Awali, katika kura za maoni mwaka 2010, Frederick Mwakalebela aliyekuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ndiye alishinda, lakini akaenguliwa katika kinyang’anyiro cha ubunge na badala yake akasimamishwa aliyekuwa mshindi wa pili, Monica Mbega. Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga alisema;

“Hatuwezi kubweteka na ushindi wa Kalenga, ushindi huo tutautumia kujiimarisha ili mwaka 2015 majimbo yote ya uchaguzi yachukuliwe na CCM.”
Mtenga alisema CCM inayo kazi ya kufanya katika Jimbo la Iringa Mjini na kuwepo kwa dalili za wananchi, kumchoka mbunge wa sasa. “Tunatakiwa kujiimarisha zaidi,”

Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu ambaye ni mwanzilishi wa mbio za bendera za chama hicho, alisema; “Kazi iliyoko mbele yetu ni kulifikia kundi kubwa la vijana.”

Alisema wana uhakika vijana wengi watajiunga na chama hicho, kabla ya uchaguzi mkuu ujao.

“Mbio zijazo za bendera ya CCM tutazitumia kukutana na vijana, zitalenga kuwashawishi vijana kujiunga na CCM; Tunataka wajue historia ya CCM na taifa lao ili nao washiriki kujenga uchumi wa nchi,” alisema.
Akizungumzia maendeleo ya vijana katika taifa hili, Msambatavangu alisema yataletwa kwa kufanya kazi na si kwa porojo za wanasiasa.

“Hakuna mwanasiasa anayeweza kugawa mitaji kwa vijana wote, akanunua mavazi kwa vijana wote, akatoa posho ya kila mwezi kwa vijana wote; njia pekee ya kujiletea maendeleo ni kutumia fursa zilizopo kufanya kazi,” alisema.

Alisema umaarufu wa vijana, utasifiwa kwa jinsi watakavyoonekana wakibadili maisha yao kwa kufanya kazi halali na si kwa kufanya maandamano ya kuvuruga amani na utulivu wa nchi.


Usiongee tu au kuandika pasipo kujua ccm wameshindaje Kalenga. Ccm wametumia tshs 600,000,000,000 na ushahidi upo alivyotoa hizo pesa yani ziliidhinishwa na Mwigulu. Ccm wametumia polisi. Kumbuka kipindi cha uchaguzi kila jimbo linajitegemea sidhani kama ccm wataweza kugawa pesa katika majimbo yote 300. Usichekelee Ushindi wa Kalenga kuwa mtashinda jimbo la Iringa kumbuka tutakuwa na tume huru la uchaguzi kama mungu atasaidia ipatikane, na daftari la wapiga kura litaboreshwa. Katika nchi ya Tanzania ccm bila kuhonga katika chaguzi hakuna kitu na hilo wanalijua.
 
watu duni tu ndiyo wanaweza kuchagua ccm ! Kumbuka mijini hakuna watu wa hivyo , nani wa kumnunua kwa wali kitumbo na maharage ? Kuna tetesi kwamba ccm itaipoteza DSM yote 2015 !

Sio tetesi ni ukweli watapoteza majimbo yoote dar hawana jipya hao magamba
 
Uwezekano wa jimbo la Iringa mjini kurudi chama cha mashetani ni mkubwa. Wanyalu ni mashabiki mno wa hili chama la wauza unga; hata kama haliwasaidii lolote.
 
watu duni tu ndiyo wanaweza kuchagua ccm ! Kumbuka mijini hakuna watu wa hivyo , nani wa kumnunua kwa wali kitumbo na maharage ? Kuna tetesi kwamba ccm itaipoteza DSM yote 2015 !

ipoteze kwa kwa ubora upi wa hy cdm ha ha ha ndugu yangu cdm hakuna kipya tena
 
Uwezekano wa jimbo la Iringa mjini kurudi chama cha mashetani ni mkubwa. Wanyalu ni mashabiki mno wa hili chama la wauza unga; hata kama haliwasaidii lolote.

Ukiona wanachagua ujue inawasaidia.

CCM wanaji prove kwenye ilani yao, Chadema wanatoa ahadi ambazo hawawezi kutekeleza labda washike nchi na nchi hawajashika. Sasa mwenye akili timamu lazima achague CCM tu hapo kuliko gamble.
 
Inashangaza sana wana chadema kukata tamaa baada ya Kalenga;lile jimbo mbunge wake marehemu mgimwa alikuwa bado ni kipenzi cha wananchi, lakini pia ccm bado ina mizizi maeneo mengi ya vijijini nyanda za juu kusini; lakini muhimu zaidi ni kwamba tofauti na siasa za kuruthishana arumeru kwa sioi, kwa kalenga ni kitu cha kawaida kwani wahehe wanarithishana hata wake; chadema inahitaji kuwa well measured, organised and calculated katika uelewa wa geo-politics za nchi yetu; hakuna siasa za zitto kalenga, ni geo politics tu chadema hawakuzisoma;

Cc MTAZAMO, Candid Scope, JokaKuu, Jasusi

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Kuna wakati huwa natafakari na kujiuliza ni jimbo lipi linaongozwa na CDM ambalo linaweza kuwa mfano wa kuigwa kulitofautisha na kipindi cha uongozi wa CCM, huwa naishia kupata jibu la hakuna.
 
Inashangaza sana wana chadema kukata tamaa baada ya Kalenga;lile jimbo mbunge wake marehemu mgimwa alikuwa bado ni kipenzi cha wananchi, lakini pia ccm bado ina mizizi maeneo mengi ya vijijini nyanda za juu kusini; lakini muhimu zaidi ni kwamba tofauti na siasa za kuruthishana arumeru kwa sioi, kwa kalenga ni kitu cha kawaida kwani wahehe wanarithishana hata wake; chadema inahitaji kuwa well measured, organised and calculated katika uelewa wa geo-politics za nchi yetu; hakuna siasa za zitto kalenga, ni geo politics tu chadema hawakuzisoma;

Cc MTAZAMO, Candid Scope, JokaKuu, Jasusi

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Wahehe wapi wanaorithishana wake? Usiandike hadithi za kusadikika hapa.
 
Last edited by a moderator:
Juzi niliongea na jamaa zangu wa Iringa wanasema wazi chaguo lao ni Mwakalebela huyu Mchangaji wanasubiri muda wake uishe.
 
Uwezekano wa jimbo la Iringa mjini kurudi chama cha mashetani ni mkubwa. Wanyalu ni mashabiki mno wa hili chama la wauza unga; hata kama haliwasaidii lolote.

Kama CCM wakikubali UPINZANI kwa dhati na HAKI ikatendeka wakati wa uandikishaji na uboreshaji wa daftari la wpiga kura,uhuru ukawepo,vyomba vya usalama vikajua sheria na mipaka yao,fujo zikadhibitiwa, basi CCM itapoteza viti vingi zaidi kwa wapinzani.Naomba niseme wapinzani na si CDM.
 
Back
Top Bottom