Obugwa Izoba
JF-Expert Member
- Nov 16, 2013
- 10,482
- 11,690
BAADA ya kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Kalenga, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimesema kinajiimarisha zaidi kirejeshe mikononi mwake, Jimbo la Iringa mjini mikononi mwake. Jimbo la Iringa Mjini linaloongozwa na Mchungaji Peter Msigwa aliyechaguliwa mwaka 2010 kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Awali, katika kura za maoni mwaka 2010, Frederick Mwakalebela aliyekuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ndiye alishinda, lakini akaenguliwa katika kinyanganyiro cha ubunge na badala yake akasimamishwa aliyekuwa mshindi wa pili, Monica Mbega. Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga alisema;
Hatuwezi kubweteka na ushindi wa Kalenga, ushindi huo tutautumia kujiimarisha ili mwaka 2015 majimbo yote ya uchaguzi yachukuliwe na CCM.
Mtenga alisema CCM inayo kazi ya kufanya katika Jimbo la Iringa Mjini na kuwepo kwa dalili za wananchi, kumchoka mbunge wa sasa. Tunatakiwa kujiimarisha zaidi,
Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu ambaye ni mwanzilishi wa mbio za bendera za chama hicho, alisema; Kazi iliyoko mbele yetu ni kulifikia kundi kubwa la vijana.
Alisema wana uhakika vijana wengi watajiunga na chama hicho, kabla ya uchaguzi mkuu ujao.
Mbio zijazo za bendera ya CCM tutazitumia kukutana na vijana, zitalenga kuwashawishi vijana kujiunga na CCM; Tunataka wajue historia ya CCM na taifa lao ili nao washiriki kujenga uchumi wa nchi, alisema.
Akizungumzia maendeleo ya vijana katika taifa hili, Msambatavangu alisema yataletwa kwa kufanya kazi na si kwa porojo za wanasiasa.
Hakuna mwanasiasa anayeweza kugawa mitaji kwa vijana wote, akanunua mavazi kwa vijana wote, akatoa posho ya kila mwezi kwa vijana wote; njia pekee ya kujiletea maendeleo ni kutumia fursa zilizopo kufanya kazi, alisema.
Alisema umaarufu wa vijana, utasifiwa kwa jinsi watakavyoonekana wakibadili maisha yao kwa kufanya kazi halali na si kwa kufanya maandamano ya kuvuruga amani na utulivu wa nchi.