Baada ya JK, Rizwan naye alalama kung'olewa UVCCM

Mama Salma naye anadai lipi?
Rz 1 atalia na kusaga meno JK atakapoondoka.
Hawa wanaomuunga mkono Rz 1 ni njaa tu zinawasumbua watamgeuka vibaya mtajionea.

hapo kwenye red sidhani coz hawa watu wanalindwa na mfumo waliojiwekea
 
Watu wazima mnatumia muda mwingi kuongea non-sense. Kwa namna hii kwakweli hatutafika, Mimi nilifikiri ilitakiwa sasa hivi kila mtanzania aongelee Hussein mwinyi ajiuzulu kutokana na milipuko ya mabomu. Watu mnaanza kuongelea watoto wadogo ambao siyo hata wakuu wa wilaya. Ndiyo maana hata serikali ya CCM inafanya madudu ikijua watu wataongelea Serious issue for few days, then watarudi kulekule kwenye Udaku (Watanzania tunapenda udaku kuliko issues za maana zinazojenga taifa)

Mkuu hilo la kuzungumzia Hussein Mwinyi ajiuzulu lilizungumziwa sana tu lakini ukweli ni kwamba alikuwa hawezi kujiuzulu wakati wizara yake iliomba pesa za kulipua hayo mabomu ikanyimwa. Mzigo ule anaubeba moja kwa moja mkuu wa kaya. Sawa tuseme kweli Hussein alikuwa na makosa na hakufanya kazi yake sawasawa, mbona mwenye kaya hajamfukuza kazi mpaka leo?

Aliyeileta hii thread na wachangiaji wachache waliojibu hoja, nimegundua kwamba wako kwenye kundi lile lile la kutumwa na mafisadi kuitumia JF kutimiza malengo yao na kutafuta taarifa. Kwa taarifa yenu, HATUDANGANYIKI!!!!!

Tiba
 
Yule Dogo wa mkwere nae pia ni janga la Chalinze, cjawah ona kijana mwenye majungu na mnafik km yule duh! Alalamike? Mbona wao walimtimua Massauni uvcccm!
 
kama kuna mtu atalia kwa kuumbuka siku mh JK anaondoka ikulu ni RZ 1. RZ 1 dogo wa fitina,mwongo,majungu yaan ndani ya CCM wazee husema bora umchane (mpe ukweli hata kama inauma) JK live kuliko kuzozana na Rz 1 kwani atapaka chumvi kwa JK na TISS yaan utakoma.

Wazee ndani ya CCM wanamwogopa Rz 1 kuliko JK.
rostam aziz ni bepari fisadi king maker hufungua mlango wowote ndani ya CCM kwa hiyo hataadhirika sana kuondoka kwa JK.(alikuwa kundi la JK 1995 ila alipopita Mkapa akamkodia ndege binafsi kuja DSM na hapo akamsahau JK.Mshangao 2005 alirudi kundi la JK)
Lowassa alishaumbuka kwa hiyo hana tena la kuumbuka zaidi ya Richimondgate
 
Nimesoma gazeti la Jamboleo, likieleza kuwa UVCCM inakusudia kumng'oa mtoto wa mkwere kufuatia kuwa chanzo cha jumuiya hiyo kushindwa kufanikisha malengo yake. Kama Dot Connector inaonyesha familia hii ni ya walalamishi maana hata mkwere alilalama kuwa CDM inafanya maandamano ya kumng'oa na sasa mkwere mtoto anapiga mayowe hayo hayo. Tujadilini wakuu

Hizi hoja zingine hazina hata hoja yenyewe.

Wenzako wanaongelea Zitto kawasaliti wewe unaleta habari nje ya habari.
 
Watu wazima mnatumia muda mwingi kuongea non-sense. Kwa namna hii kwakweli hatutafika, Mimi nilifikiri ilitakiwa sasa hivi kila mtanzania aongelee Hussein mwinyi ajiuzulu kutokana na milipuko ya mabomu. Watu mnaanza kuongelea watoto wadogo ambao siyo hata wakuu wa wilaya. Ndiyo maana hata serikali ya CCM inafanya madudu ikijua watu wataongelea Serious issue for few days, then watarudi kulekule kwenye Udaku (Watanzania tunapenda udaku kuliko issues za maana zinazojenga taifa)

hizo habari za mwinyi ajiuzulu zilishaongelewa sana. Tafuta threads zake.
Tz imejaa matukio na watu hatuwezi kudiscuss tukio moja kila siku.
Kama unaona habari haina manufaa kwako unaipotezea. Ila jambo moja dogo linaweza kuwa na impact kubwa kwenye jamii. Usidharau.
 
Ndio safari yetu inaanza kwenda Dodoma kumaliza kazi kisha sasa aendelee kuropokaropoka! Huyu mtoto mjinga sana hafai kuharibu jumuiya kwa sababu ya baba yake. Tuliapa kuilinda na sasa ni wakati wa kuisafisha. Wajumbe wa Baraza wenzangu haya shime wote tukamalize kazi yetu mapeeema Dom kisha tukutane Chako ni Chako kwa nyama choma na bia bariiiiidiiiiii.
 
hizo habari za mwinyi ajiuzulu zilishaongelewa sana. Tafuta threads zake.
Tz imejaa matukio na watu hatuwezi kudiscuss tukio moja kila siku.
Kama unaona habari haina manufaa kwako unaipotezea. Ila jambo moja dogo linaweza kuwa na impact kubwa kwenye jamii. Usidharau.

Wewe ni wale wale mnaopenda umbea, kwani Misri na Tunisia waliandamana siku moja. Ili kufanikisha jambo lolote linalokosoa serikali lazima kitu kiongelewe kwa muda wa kutosha ikishindikana maandamano yafanyike. siyo unapiga porojo kidogo, then unakimbilia kwenye udaku. Kama unapenda udaku kachangnie kwenye Issa Michuzi
 
Inabidi wamvuti kasi kwanza hadi msure atoke madarakani, kwa sasa watamuonea noma mwenyekiti wa chama
 
Wewe ni wale wale mnaopenda umbea, kwani Misri na Tunisia waliandamana siku moja. Ili kufanikisha jambo lolote linalokosoa serikali lazima kitu kiongelewe kwa muda wa kutosha ikishindikana maandamano yafanyike. siyo unapiga porojo kidogo, then unakimbilia kwenye udaku. Kama unapenda udaku kachangnie kwenye Issa Michuzi

ama kweli nyani haoni kundule.
Udaku na wewe unaupenda ndio maana umerudi tena kwenye hii thread.
Nina wasiwasi kama ushawahi kuhudhuria hata hayo maandamano.
Usiishie kuyasikia jf na kuyaona kwenye tv tu.
 


KUTANO wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana (UV-CCM) mkoa wa Pwani umefanyika mjini Bagamoyo na kuibuka na matamko mazito yanayozua maswali mengi kuliko majibu.

Kwa kauli moja, Baraza la Vijana limeazimia sekretariati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iwajibike kwa kushindwa kumshauri mwenyekiti, Rais Jakaya Kikwete namna nzuri ya kuendesha chama.
Kwamba mawaziri wakuu wastaafu wafunge midomo yao vinginevyo watalazimishwa kufanya hivyo na chama kinachowatunza kwa fedha nyingi!
Kwamba gavana wa Benki Kuu (BoT), Profesa Benno Ndullu awajibike kwa kueleza na kufafanua hali ya uchumi badala ya kumwachia Rais Kikwete kujieleza mbele ya umma.
Akisoma tamko la Baraza la Vijana, Makamu Mwenyekiti wa UV-CCM, mkoani Pwani, Abdalah Ulega aliwashambulia baadhi ya viongozi wastaafu kwa kusema, “Kama wanataka urais wasubiri muda wachukue fomu na kuwashawishi wajumbe wawachague.
“Lakini kwa kumtukana mwenyekiti hawatapata kamwe kwa kuwa yeye ndiye anayejua ni nani muadilifu, hivyo wasiharibu nchi kwa maslahi yao. Wao wameshiba na sasa wamevimbiwa watuache na sisi tule kama wao.”
Miongoni mwa waliohudhuria mkutano wa Baraza la Vijana, ni Dk. Shukuru Kawambwa waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi na mjumbe wa Baraza Kuu la UV-CCM taifa, baadhi ya wabunge wa CCM na Ridhiwani Kikwete.
Kwa tuliobahatika kunyatia habari kutoka kikao cha Bagamoyo, tunalazimika kusema kuwa wapo watu waliopandikizwa kuvuruga chama baada ya kufanikiwa kufanya kazi hiyo katika dola.
Maneno aliyoyasema ni ushahidi tosha, kwamba Ulega ametumika kuivuruga UV-CCM, serikali na chama chenyewe.
Katika hali ya kawaida, huwezi kutegemea makamu mwenyekiti wa UV-CCM, tena katika mkoa akisimama hadharani kuwatuhumu na kuwakemea viongozi wastaafu kana kwamba walichokifanya ni uhaini.
Kwanza inashangaza kuona, njia aliyoitumia Ulega na wenzake ni njia ile ile ambao wazee wale waliitumia ya kutoa maoni yao kwa kudhani chama chao kitawasikiliza ili kuchukua hatua muafaka ya kunusuru hali ya mabo inayokwenda mrama kila kukicha.
Jambo jingine linalotisha katika hotuba ya Ulega ni pale wanapodai kuwa wastaafu wanaotoa maoni yao kuhusu kasoro za chama chao, wanafanya hivyo kwa sababu ya agenda ya urais wa mwaka 2015. Na kwamba kama hiyo ndiyo agenda yao, “wamechelewa” maana ni rais Kikwete tu anayejua rais wa mwaka 2015.
Haya ni maneno mazito lakini pia ya ajabu kwa sababu urais wa taifa hili si uchifu wala urithi wa shamba la bibi. Urais ni taasisi na ni rukra kuizungumzia kwa yeyote hata kama watakuwapo wasiopenda hilo kufanyika.
Hata kama Kikwete mwenyewe aliwahi kusema urais ni suala la familia na kwamba urasi wake hauna ubia na mtu yeyote, hilo ni suala lisilokubalika kuwa rais wa 2015 anayemjua ni Kikwete peke yake. Je, Ridhiwani na Ulega wamepata wapi jeuri ya kutamka maneno haya?
Lakini kuna hili pia. Kumbe suala zima na minyukano inayoendelea ndani ya chama inahusu kula kwa zamu. Sasa ni zamu ya mkoa wa Pwani na kipekee mji wa Bagamoyo! Mwingine akilipuka akasema ni zamu ya kabila fulani, dini fulani, kundi fulani, atakuwa amekosea?
Mkorogano huu ndani ya chama unazidi kukua na kuchukua sura mpya kila uchao. Kwa kuwa CCM ni taasisi, mikorogano ni jambo linalotazamiwa. Lakini hata hivyo, iko mikorogano mingine ni vigumu kuielewa hasa pale inapochukua sura ya familia kuvuruga taasisi.
Huko nyuma tumekuwa tunasikia watu mbalimbali wakiteta na wengine kupika majungu, juu ya tabia ya familia ya Rais Jakaya kuingilia masuala ya dola. Manung’uniko yalichukua sura mpya baada rais mwenyewe kuamua kumpatia kijana wake Ridhiwani Kikwete jukumu la kutembeza fomu ya udhamini wakati anagombea urais ndani ya chama chake.
Baadaye alipoulizwa ni kwa nini alifanya hivyo. Akasema, akasema kugombea ni suala la familia. Ikafuata ajabu pale mke wa rais Mama Salma Kikwete alipoanza kutumia raslimali za serikali kuzunguka nchi nzima kunadi mgombea urais ambaye ni mme wake. Kelele zilipopigwa, inadaiwa uchakachuaji wa risiti ulifanyika ili kuficha ukweli.
Hata hivyo, tayari chama kilikuwa kimepata sura mbaya mbele ya wapiga kura. Haikuishia hapo, mtoto mwingine wa Rais, aitwaye Miraji Kikwete ilidaiwa kukabidhiwa ofisi ya fedha na mikakati iliyokodishwa maalum katika mtaa wa Undali.
Kwa kuwa hii ilikuwa ni kinyume na taratibu za chama chetu, wenye hekima wakapisha ili familia iendeshe kampeni. Matokeo ya hatua hizi wote tunajua kwamba kinachodaiwa kuwa ni kushindwa kwa chama, kunaweza kuwa ni kushindwa kwa familia kuendesha kampeni.
Kwa jinsi sasa mambo yanavyokwenda, familia ya rais ikiongozwa na Ridhiwani inataka kuwaangushia watu wengine zigo hili wengine.
Siyo siri kuwa tangu Kikwete aingie madarakani, chama hiki kimeingia katika enzi mpya. Vitendo vya kibaguzi vilivyoasisiwa na kundi la wanamtandao, uliomwingiza yeye na maswahiba zake madarakani, sasa vimemgeuka na kuanza kumtafuna mwenyewe.
Hata kizunguzungu kinachomzonga sasa hadi kushindwa kuchukua hatua madhubuti katika kurejesha nidhamu katika chama na serikali, kinatokana kwa sehemu kubwa na serikali yake kugeuka kuwa ya washikaji.
Bahati njema wengi wanafahamu kinachotendeka nyuma ya kauli hizi. Kwamba ni vita ya urais wa mwaka 2015. Sasa mbona wameanza mapema kiasi hiki? Katika hali hii, chama kitaweza kupona kweli?
Je, kundi hilo linaloanza kuwatuhumu wastaafu kuwa wamekula na kushiba na hata kuvimbiwa, wanaweza kweli kujilinganisha na wao katika hili la kula na kuvimbiwa? Tulio karibu na watu hawa tunajua kuwa baadhi yao tayari wamekula la kuvimbiwa kupita kiasi na wanachotafuta sasa labda ni kutaka hisani kwa wanayemuona ataendelea kuwakumbatia.
 
Mkuu.... hayo unayosema yako kwenye tamko maalumu au yalikuwa tu mazungumzo ya ndani ya kikao?

Especially:
1. "Kwamba mawaziri wakuu wastaafu wafunge midomo yao vinginevyowatalazimishwa kufanya hivyo na chama kinachowatunza kwa fedha nyingi!"
2." Wao wameshiba na sasa wamevimbiwa watuache na sisi tule kama wao.”
3. “wamechelewa” maana ni rais Kikwete tu anayejua rais wa mwaka 2015.

Anyway hata kama walizungumza kwenye kikao lakini hayako kwenye tamko bado ni unbelivable...
 
Vyovyote iwavyo hao vijana wasifikiri ccm ni mali yao pekee,waulize hiki chama kimetoka wapi,vinginevyo ni matusi kwa wazee wetu wastaafu hata kwa mwalimu Nyerere..kweli hawana tofauti na funza,pili..wasiwatishie wastaafu eti waalipwa kwa hisani ya chama,la! hawa walikuwa viongozi waadilifu wa nchi hii na kama wanalipwa ni pesa ya serikali na si mfuko wa chama,labda Lowassa (kama analipwa)basi ndo anafadhiriwa na chama kwani aliachishwa kazi kufuatia kuhujumu nchi..hao uvccm wanaanza kutumikia laana za wazazi wao(mafisadi)
 
duuuuu
kama Uvccm imefikia hapo basi nadhani viongozi wenye ndani ya Uvccm hawajui nini wafanyalo,kwani Uvccm ni tanuru la kuandaa viongozi na sio tanuru la kukibomoa chama ambacho ndicho kinailea hiyo Uvccm
Uvccm watambue kuwa wao wanatakiwa kuwa mstari wa mbele ktk kukitetea chama na kuatangaza sera za chama ili hapo baadae chama kiweze kushika dora

lakini inaonyesha Uongozi husika wa Uvccm umejisahau na umechukuwa jukumu moja kwa moja la kukikosoa chama ambacho ndicho baba na mama pia

Uvccm ipo hapo kwa lengo la kulinda amani,umoja na uhuru uliopo na sio kufanya hayo wafanyayo sasa
watambue kuwa ile alama ya mwenge ina maana kubwa sana kwa uvccm,nadhani baadhi ya viuongozo wa uvccm hawaelewi nini maana ya alama hiyo na ndio maana wamafikia hapo walipo sasa
Riziwani-keepchange-mkwawa comlpex-siasa-duuuuuuuuu,hongera kiongoziiiiiiii kwa kukinyooosha chama
 
Mkuu.... hayo unayosema yako kwenye tamko maalumu au yalikuwa tu mazungumzo ya ndani ya kikao?

Especially:
1. "Kwamba mawaziri wakuu wastaafu wafunge midomo yao vinginevyowatalazimishwa kufanya hivyo na chama kinachowatunza kwa fedha nyingi!"
2." Wao wameshiba na sasa wamevimbiwa watuache na sisi tule kama wao.”
3. “wamechelewa” maana ni rais Kikwete tu anayejua rais wa mwaka 2015.

Anyway hata kama walizungumza kwenye kikao lakini hayako kwenye tamko bado ni unbelivable...

Uko sahihi kabisa, hii yote ni mbinu ya mafisadi kupotosha ili wapate kuzuia tamko la kutaka watimuliwe, sidhani kama inasaidia sana na kama wataendelea kuwapo ndio kaburi la CCM
 
mhmhmh!!!! its a shame,bora uzandiki...na sasa nakiona kile kitakachojiri punde,tena siyo kwa hatua bali kizima kizima...
CCM tuwe wavumilivu,najua na natambua yataka moyo sana na dhamira ya kweli kukubali ukweli na hasa ukweli wenyewe uwe adharani...na hatari zaidi awe anakukosoa mtoto mdogo...tena siyo wa jirani bali wa kumzaa,tena ambaye ukumlipia ada ya skuli ivyo akusoma bali kapata maarifa ya kujua kile kilicho bora mtaani,mtaa wenye majalala na vumbi tupu hakuna rami,hakuna skuli,hakuna umeme,hakuna maji,hakuna maduka,yanayoweza mfungua ubongo na kujulisha kile kinachojili duniani...ni utashi wake tu umempa kujua yale anayoyajua.
aksante tena aksante @ nngu007.
 
hayatuhusu haya; ni ya wafu na wafu wenzao; mafisadi na mafisadi wenzao; wanyonyaji na wanyanyaji wenzao; wote ni wale wale!!!
 
Back
Top Bottom