Baada ya huu mshikemshike, watakutana kweli?

Samia hana ubavu wa kukutana na Mbowe tena, ameshapoteza muelekeo na hajui wapi ataanzia kujenga imani yake kwa wapinzani na wananchi kwa ujumla, ukiondoa wale waimba mapambio wa lumumba.
Head of state ambae ni commander in chief anakosa ubavu wa kukutana na mbowe yupi huyo
Na hao wananchi ni wapi Waliokwambia hawana Imani na Raisi wao
 
So kudai katiba ni kosa?
Kudai katiba si kosa, lakini katiba ni ya wananchi na si ya chama kimoja. Mama hajakataa katiba mpya lakini msimpe presha ndiyo kwanza amechukua uongozi na ana vipaumbele vyake na hata CDM wao wangekuwa ndiyo wenye madaraka wasingekubali kupelekeshwa.
 
Bado una mawazo POTOFU. Tumefanya uchaguzi October 2020 ambao mimi ba Watanzania wtunauita UCHAFUZI kwani yaliyotokea wote tunayajua.
Nchi ina mfumo wa vyama vingi kwa miaka 30 sasa lakini bado ina katiba ya chama kimoja.
Kikwete aliunda Tume ya Warioba ili ikusanye maoni ya Watanzania nchi nzima na wakaifanya vizuri sana kazi ile na hata Kikwete akawapongeza kwa UZALENDO wake.
Kikwete huyo huyo ambaye aliiona rasimu ile nzuri sana lakini baada ya kutishwa na maccm kwamba rasimu ile ikipitishwa na kuwa Katiba ya nchi basi maccm hayatashinda tena uchaguzi nchini.
Sasa pressure iko wapi hapo wewe!? Huoni huu mwelekeo wa nchi uliojaa dhuluma na udhalimu wa kutisha.
Mbona maccm damu damu ambao waliwahi kushika nafasi mbali mbali za juu Serikalini Warioba na Butiku nao wanaifagilia Katiba mpya!? Hawa nao wanampa samia pressure ili iweje!? 😳
Kwa nini Rais Kikwete kama mwenyekiti wa CCM hakuiweka Katiba Mpya kama kipaumbele namba moja kwenye ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2015 na alimuacha mgombea wake wa urais asiizungumzie k katiba mpya wakati wa kampeni ?

Kwa kukunukuu, kama Rais (Kikwete) aliyekuwepo wakati wa mwanzo wa mchakato wa katiba mpya alitishiwa na "maccm", hao hao "maccm" wanashindwa nini kumshinikiza Rais wa sasa aachane na mchakato wa kuleta katiba mpya ?

Unafikiri Samia anakubalika 100% ndani ya chama chake kama mwenyekiti na Rais? Ndani ya siku 100 tu za uongozi wake kuna watu aliwasema wanaanza mbio za urais 2025 na kuwaonya, mara tusikie "Sukuma Gang" wanamhujumu

Kuleta mchakato wa katiba mpya sasa hivi kwa Rais Samia ndio ingekuwa "political suicide" yake....Kama unaulizia Mzee Warioba na Mzee Butiku, kuna msemo "Shetani akizeeks huwa malaika"...kwa sasa hawana kikubwa cha kupoteza ikitokea mabadiliko ya aina yoyote ya katiba.

Tunaweza tusikubaliabe mawazo mpaka mwisho,ila mimi naheshimu mawazo yako na wala sitokudhihaki kuwa una mawazo potofu, bali unamawazo yanayokinzana na mtazamo wangu. Na kila mtu ana haki na uhuru wa kuwa na mtazamo wake !
 
Watu unawaambia sawa subirini
Wanakuletea vurugu
Kutakua na kikao kweli?.

Mbona ni haki yao hao watu? Yani hilo jambo la kusubiria linapewa go ahead na mtu mmoja? Mpaka ajisikie? Ndio maana tunadai mabadiliko ya katiba aisee. Si kwa power kiasi hicho
 
Hebu acha kuonyesha ujuha wako hadharani Kwa kuendelea kuandika UPUUZI.

Kwa nini Rais Kikwete kama mwenyekiti wa CCM hakuiweka Katiba Mpya kama kipaumbele namba moja kwenye ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2015 na alimuacha mgombea wake wa urais asiizungumzie k katiba mpya wakati wa kampeni ?

Kwa kukunukuu, kama Rais (Kikwete) aliyekuwepo wakati wa mwanzo wa mchakato wa katiba mpya alitishiwa na "maccm", hao hao "maccm" wanashindwa nini kumshinikiza Rais wa sasa aachane na mchakato wa kuleta katiba mpya ?

Unafikiri Samia anakubalika 100% ndani ya chama chake kama mwenyekiti na Rais? Ndani ya siku 100 tu za uongozi wake kuna watu aliwasema wanaanza mbio za urais 2025 na kuwaonya, mara tusikie "Sukuma Gang" wanamhujumu

Kuleta mchakato wa katiba mpya sasa hivi kwa Rais Samia ndio ingekuwa "political suicide" yake....Kama unaulizia Mzee Warioba na Mzee Butiku, kuna msemo "Shetani akizeeks huwa malaika"...kwa sasa hawana kikubwa cha kupoteza ikitokea mabadiliko ya aina yoyote ya katiba.

Tunaweza tusikubaliabe mawazo mpaka mwisho,ila mimi naheshimu mawazo yako na wala sitokudhihaki kuwa una mawazo potofu, bali unamawazo yanayokinzana na mtazamo wangu. Na kila mtu ana haki na uhuru wa kuwa na mtazamo wake !
 
Rais Samia yupo madarakani sasa kwa miezi minne.

Katika muda wake huo madarakani, amekutana na makundi kadhaa sasa: vijana, wazee, maaskofu, akina mama, nk.

Sina hakika kama keshakutana na Waislamu wenzake. Nadhani bado hajakutana nao. I wonder why…maana tayari keshakutana na Wakristo!!

Miezi mitatu iliyopita Mheshimiwa Freeman Mbowe wakati akihutubia taifa alisema kuwa wamemwandikia barua mheshimiwa Rais na kuomba wakutane naye.

Mpaka sasa Bi. Mkubwa hajakutana nao. Sijui amepanga kukutana nao.

Na baada ya kukamatwa kwa Mbowe na hizo tuhuma za ugaidi tulizoambiwa, sijui kama huo mkutano wao utakuja kutokea!

Maana itakuwa ni maajabu Rais wa nchi kukutana na ‘gaidi’ na kufanya naye mazungumzo.

Bi. Mkubwa anaupiga mwingi huku kazi ikiendelea.

Nyani Ngabu,
Hilo deal limetengenezwa na Mahafidhina wa CCM ili kuhakikisha Bi Mkubwa hakutani na Mhe. Mbowe!!!CCM wana hofu sana na CDM hasa Mbowe. C C M wamechekecha wakaona Mwamba akikutana na Mama tu atafungwa magoli ya kushtukiza......hivo wakaona isiwe taabu BORA WAMTENGENEZEE ZENGWE ILI ASISUMBUE!
 
Rais Samia yupo madarakani sasa kwa miezi minne.

Katika muda wake huo madarakani, amekutana na makundi kadhaa sasa: vijana, wazee, maaskofu, akina mama, nk.

Sina hakika kama keshakutana na Waislamu wenzake. Nadhani bado hajakutana nao. I wonder why…maana tayari keshakutana na Wakristo!!

Miezi mitatu iliyopita Mheshimiwa Freeman Mbowe wakati akihutubia taifa alisema kuwa wamemwandikia barua mheshimiwa Rais na kuomba wakutane naye.

Mpaka sasa Bi. Mkubwa hajakutana nao. Sijui amepanga kukutana nao.

Na baada ya kukamatwa kwa Mbowe na hizo tuhuma za ugaidi tulizoambiwa, sijui kama huo mkutano wao utakuja kutokea!

Maana itakuwa ni maajabu Rais wa nchi kukutana na ‘gaidi’ na kufanya naye mazungumzo.

Bi. Mkubwa anaupiga mwingi huku kazi ikiendelea.

Unafiki alioufanya tangu aapishwe utamgharimu big time. Kuna risk kubwa sana ya nchi kumshinda!
 
Hebu acha kuonyesha ujuha wako hadharani Kwa kuendelea kuandika UPUUZI.

Hiyo ilikuwa ni wakati wa Kampeni ? Katiba mpya haikuwekwa kama kipaumbele kikuu cha CCM katika ilani ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na ndio maana haikutiliwa mkazo na Magufuli katika kampeni zake na ndio maana aliizika kabisa na hakukuwa na kelele zozote kutoka ndani ya CCM. Naendelea tu kusisitiza kutofautiana mtazamo haihalalishi kumdhihaki mwenzako unaweza kusema nina ujuha, nina upuuzi lakini haiongezi afya katika mjadala tunaoongelea. Tunaweza kushambuliana kwa matusi na kuishia kupigwa BAN na haitakuwa na manufaa kwa mtu yoyote, ninapokosea nikosoe unapokosea nitakukosoa, pale itakaposhindikana tunaweza kukubaliana kutokukubaliana, its quite simple...hakuna haja ya kugombana kisa tu tofauti ya mtizamo wa kisiasa !

Halijaisha. Ndio limeanza. Usijisifie. Uhuru wa Afrika Kusini haukuishia kwenye kifungo cha Mandela.
Tatizo Mbowe alikuwa na haraka sana ya kukutana naye..."mama" alivyoanza kuupiga mwingi akaona yeye na wenzake wanapoteza relevancy wakabadili gia angani na kuanza kudai katiba mpya kwa ubabe huku akijua kabisa matokeo yake.
 
Narudia tena acha kuonyesha ujuha wako hadharani. Maccm yanajua umuhimu mkubwa wa Katiba Mpya Watanzania. Na wanajua fika kama ikipatikana na Tume huru ya uchaguzi basi ndiyo itakuwa Kiama chao Tanzania. Sasa wewe umeshupaza shingo kuandika ujinga wako.

Kumbuka UHURU NA HAKI ya raia, vyama vya upinzani ba vyombo vya habari siku zote HUINUA Taifa, kuleta mshikamano, furaha na maendeleo kwa Taifa. Na udhalimu na udhalimu huvunja mshikamano, kuleta hofu ná majonzi na pia kukwamisha maendeleo katika Taifa.
Hiyo ilikuwa ni wakati wa Kampeni ? Katiba mpya haikuwekwa kama kipaumbele kikuu cha CCM katika ilani ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na ndio maana haikutiliwa mkazo na Magufuli katika kampeni zake na ndio maana aliizika kabisa na hakukuwa na kelele zozote kutoka ndani ya CCM. Naendelea tu kusisitiza kutofautiana mtazamo haihalalishi kumdhihaki mwenzako unaweza kusema nina ujuha, nina upuuzi lakini haiongezi afya katika mjadala tunaoongelea. Tunaweza kushambuliana kwa matusi na kuishia kupigwa BAN na haitakuwa na manufaa kwa mtu yoyote, ninapokosea nikosoe unapokosea nitakukosoa, pale itakaposhindikana tunaweza kukubaliana kutokukubaliana, its quite simple...hakuna haja ya kugombana kisa tu tofauti ya mtizamo wa kisiasa !

Narudia tena acha kuonyesha ujuha wako hadharani. Maccm yanajua umuhimu mkubwa wa Katiba Mpya Watanzania. Na wanajua fika kama ikipatikana na Tume huru ya uchaguzi basi ndiyo itakuwa Kiama chao Tanzania. Sasa wewe umeshupaza shingo kuandika ujinga wako.

Kumbuka UHURU NA HAKI ya raia, vyama vya upinzani ba vyombo vya habari siku zote HUINUA Taifa, kuleta mshikamano, furaha na maendeleo kwa Taifa. Na udhalimu na udhalimu huvunja mshikamano, kuleta hofu ná majonzi na pia kukwamisha maendeleo katika Taifa.
Sawa wewe "mwerevu" uwe na siku njema😊
 
Kuna vitu viwili vikubwa ambavyo Upinzani hawavielewi:
1. Katiba mpya sio mwarobaini wa matatizo yetu. Zipo nchi nyingi ambazo ziliandika katiba zao upya, lakini shida zao zimebaki palepale.
2. Rais hana uwezo wa kuwapa Upinzani katiba mpya. Anachoweza kufanya ni kuitisha Bunge la Katiba kisha wajumbe, kama walivyofanya 2015, wakapiga billions of TZS, wakatunishiana misuli na hatimaye kusambaratika bila kupatikana kwa katiba mpya. A replay of the 2015 wastage of taxpayers money is foolishness of the highest order!
 
Hahahahahaha Katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi itainua nchi yetu sana. Watanzania kura zetu zitaanza kuheshimiwa na hivyo kuchagua Viongozi watakao bila chama chochote kile kupora uchaguzi.
Chama kilicho madarakani KIKIVURUNDA uchaguzi unaofuata kinaondolewa na kuwekwa kingine.
Katiba itaheshimiwa na yoyote atakayeidharau wa chama chochote kile cha moto atakiona.
Watanzania tutakuwa na uhuru na haki ya kuikosoa Serikali ya chama chochote kile bila hofu ya kutekwa na kupotea au kuuawa.
Mahakama zitakuwa huru kufanya kazi kwa haki na si ilivyo hivi sasa ambapo zinatumika na genge la wahuni wa maccm kubambikia kesi FEKI za ugaidi, uchochezi, uhujumu uchu
Vyombo vya habari vitakuwa na uhuru na haki ya kufanya mijadala yoyote ile hata kama itaikosoa Serikali bila hofu ya kufungiwa au kutekwa.
Ripoti za CAGs zitaheshimiwa na kufanyiwa kazi vile ipasavyo hivyo kumaliza wizi, ubadhirifu na ufisadi uliokithiri ndani ya taasisi mbali mbali za Serikali.
Heshima yetu kama Nchi ambayo sasa imepotea itarudi tena na Tanzania na Watanzania kuheshimiwa tena popote pale duniani.
Hii ndiyo Tanzania niitakayo mimi.

Weekend njema Mkuu kumbuka kuchukua hatia zote za tahadhari dhidi ya COVID-19 ikiwemo kuvaa mask 😷 🙏🏾
Sawa wewe "mwerevu" uwe na siku njema😊
 
There's nothing more dangerous than a resourceful idiot.
Scott Adams
 
Samia hana ubavu wa kukutana na Mbowe tena, ameshapoteza muelekeo na hajui wapi ataanzia kujenga imani yake kwa wapinzani na wananchi kwa ujumla, ukiondoa wale waimba mapambio wa lumumba.
Wananchi wana imani na Mother iliyopitiliza, ndiyo maana hata wakiambiwa waingie barabarani kumtafuta Mwamba/Abubakari Mbowe hawajitokezi. And mbona KM wenu amepooza sana? Nakumbuka enzi za Slaa, Mbowe alikamatwa lile sakata la mabomu Arusha, Slaa alikuwa mbogo kweli kweli mpaka mbowe akaachiwa, Mnyika ana nini?
 
Hao wamarekani majambazi tu mzee, furaha yao ni kuona mataifa mengine yanafarakana. Wao ndiyo source ya migogoro mingi inayoendelea kwa sasa duniani, wakitumia hicho chombo chao cha fitina CIA
 
Ndiyo hata udhalimu na dhuluma zinazofanywa na maccm kwa miaka mingi sasa ikiwemo kupora chaguzi, wizi, ufisadi, ubadhirifu, kubambikia kesi, kuwapora billions Watanzania, kuminya uhuru na haki ya Watanzania, vyombo vya habari na vyama vya upinzani ni Marekani ndiyo wamewaambia maccm yafanye dhuluma na udhalimu huo wa kutisha. Usinizeeshe.

Hao wamarekani majambazi tu mzee, furaha yao ni kuona mataifa mengine yanafarakana. Wao ndiyo source ya migogoro mingi inayoendelea kwa sasa duniani, wakitumia hicho chombo chao cha fitina CIA
 
Ndiyo hata udhalimu na dhuluma zinazofanywa na maccm kwa miaka mingi sasa ikiwemo kupora chaguzi, wizi, ufisadi, ubadhirifu, kabambikia kesi, kuwapora billions Watanzania, kuminya uhuru na haki ya Watanzania, vyombo vya habari na vyama vya upinzani ni Marekani ndiyo wamewaambia maccm yafanye dhuluma na udhalimu huo wa kutisha. Usinizeeshe.
Ni wapi hamna ufisadi TZ hii? Huko kwenye vyama vyenu ndiyo majambazi yamejificha. Kama siyo mzee wa kiumri basi ni mzee wa jf (ref lini ulijiunga)
 
Back
Top Bottom