Baada ya engagement ring mwenzenu nimemegewa

Duh Mzee hili halikuwa hata la wewe kusuburi mpaka wana JF wakushauri huyu ukimwacha tu hivi hivi atakuwa winner mtafute mchape vibao na umwambie kila atapokuwa akikuona akupishe njia otherwise kila ukimwona mchape vibao na huyo mtoto si wako unadanganywa.
 
Moja ya sifa ya penzi la dhati ni uvumilivu na kusamehe, jiulize nafsini mwako kweli umemdelete, na kwa nini hukusema kwenu na kwao, kila mwanadamu huteleza kwa namna yake sio kosa moja unapoteza ulichokipenda, kama inawezekana kumsamehe muuaji, utashindwaje kumsamehe mpenzio yaheee, ucfuate wanajf wote waropokaji tu, Ajuae kiatu kimembana ni yule aliekivaa, tuliza Nzuka weyee, hiyo mijihasira tuu itapita kama upepo yakhee, usiache mbachao kwa msaala upitao ndugu:nono:
 
Heshima zenu wote wana JF.

Hii ni story ya kweli. Jamani naomba ushauri kwa sababu mwenzenu nimechanganyikiwa. Nina mchumba wangu ambaye nimefahamiana takribani miaka miwil sasa. Miezi sita ilopita niliamua kutangaza nia ya kweli na kumfisha engagement ring tena mbele ya wanafamilia wote. Tlikua tunapendana sana. Katika harakati za kujiendeleza kimasomo, nlipata nafasi kwenda chuo kwa ajili kuchukua degree ya pili (masters). Na mchumba wangu naye akawa amepata chuo mkoa tofauti na wa kwangu. zengwe limeanza tukiwa likizo wote nyumbani. my wife to be amekuja nyumbani kwangu mida ya saa kumi na mja jion kama kaida yake alikua amependeza sana. Kapika msosi tukala. Yeye amepanga nyumba yake mbali na nyumbani kwao. Ghafla akaniambia, "honey unajua mamangu amekuja kunisalimia kwa maana hio ntaondoka muda sio mrefu kwenda kumuandalia chakula" Nkamwambia, hamna noma baby, nkamsindikiza kisha nkarudi home kwangu kuangalia TV. Tuna mazoae ya kupigianapigiana simu. Siku hio ikawa tofauti kwani hata mawasiliano hayakua smooth as usual, nkamuuliza swiry what are u exactly doin? kaniambia "whatching TV HONEY" Nkamuuliza which channel? Akaniambia "TBC). Kwa vile nlikua naangalia the same channel nkamuuliza anaaangalia nini. Hakujibu mara kigugumizi. Siku hio sikupata hata tone la usingizi. Ilipofika saa kumi na nusu alfajiri, nkachukua gari kwenda nyumbani kwake. Nlipofika getini kwake nkampigia simu kua niko nje aje anifungulie kuna issue muhimu sana nataka nimwambie. Akagoma kua hafungui kwa vile mamake yupo. Nkampigia mdogo wake aje anifungulie naye akakataa. Kwa vile mama mkwe mtarajiwa ananifahamu na ananiamini nkajua yeye sio tatizo la kutofunguliwa. Ok nkamwita atoke nje bila kunifungulia akagoma. Hapo ilikua inakaribia saa kumi na moja unusu. Nikamwambia kua sitoki getin kwake hadi asubuhi ili niweze kuonana naye. Baadae akazima simu yake. Ilipofika saa mbili akawa amewasha simu yake, nkamwambia bado niko getini namsubiria. Alivyoskia niko serious, akaniambia ukweli kua hayuko nyumban na hakulaa nyumbani kwake. Ni kweli hakulala kwake na sio kweli kua mamake alikua amemtembelea. I proved that beyond doubt. Nkaondoka zangu nyumbani nikiwa nimechanganyikiwa ile mbaya. Jioni yake akaja kwangu for reconciliation. Siku hio akanidanganya, nikamfukuza haraka kutoka kwangu na makofi na buti juu. The next day she came and told me nothing but the truth kua alikua na alilala kwa mshikaji (gentleman) ambaye wanafanya kazi pamoja (I know this guy). She apologized. Nkajifanya nmemsamehe ila kichwani nlikua nmeshamdelete. Badae akarudi chuoni, baada ya wiki tatu hivi akaniambia kua ana uja uzito wangu. Nlichomwambia ni kua siutambui huo uja uzito labda aende kwa jamaa yake(mwizi) ndo kamtia hio mimba. Honestly, am heartbroken na simtaki na wala simpendi tena huyu dada. She still instists that am the father hadi anakwenda nyumban kwetu kuambia kua she is expecting my baby. Sijamwambia ndugu yangu yeyote about this saga.

Je niwambie ndugu zangu na marafiki zangu wa karibu full story juu ya huyu mdada? nyumban kwetu anakubalika sana. Ntashukuru sana kwa ushauri wenu


Do it now..or SHUT ur mouth forever
 
Moja ya sifa ya penzi la dhati ni uvumilivu na kusamehe, jiulize nafsini mwako kweli umemdelete, na kwa nini hukusema kwenu na kwao, kila mwanadamu huteleza kwa namna yake sio kosa moja unapoteza ulichokipenda, kama inawezekana kumsamehe muuaji, utashindwaje kumsamehe mpenzio yaheee, ucfuate wanajf wote waropokaji tu, Ajuae kiatu kimembana ni yule aliekivaa, tuliza Nzuka weyee, hiyo mijihasira tuu itapita kama upepo yakhee, usiache mbachao kwa msaala upitao ndugu:nono:

We mwenyewe umeropoka!!
Leo pete tu kalala nje.....akishaolewa sindo atamletea na watoto kabisa|?
Acha kumpotosha mwenzako ww:A S angry:....huyo bidada hafai.....

Pierre pole....mwaga....angalia kwingine!!!
 
Pambaff.... Au wewe ndo demu husika?????. hapo ni kulala mbele tu. Point of No Return
 
WE MAKALIO UNATOA USHAURI MCHAFU NA WA HOVYO HOVYO APA TENA WA KIHINI..
IVI UJISHTUKII KUWA UPO PEKE YAKO????
NAZAN UTAKUA WW NI MUHUSIKA ULIEMEGWA AU NI MDOGO MTU
>>>
Pichu yko........ dat y unawavulia wa2

gud sna,huyo hatakuwa ndio mmegwa bila shaka!
 
Pole sana Pierre la msingi acha mtoto azaliwe umpime DNA kama wako itabidi umtunze ...ila huyo mwanadada hakufai

Mi. Sidhan kwa sasa kama hilo la DNA ni muhimu nakushauri utafute utulivu kwanza na akishazaliwa mtoto unafanya DNA ya macho kwanza halafu unajiridhisha kabisa ndiyo kwa vipimo halisi halafi umtunze mtoto LAKINI SIYO KUMWOA HUYO MWANAMKE HAFAI. Nimeshawahi kupitia kitu kama hiki inauma sana usipime ndugu yangu kunguru hafugiki
 
Mh,pole sana. I can feel ur pain. N ngumu sana kusamehe maana amekuumiza sana. Wala ucjali pierre, as time goes all yo pain wil go. Hafai kuoa huyo maana inaonyesha hyo ni abia yake so ni ngumu kuacha hata akiolewa.
 
Hawa viumbe wadhaifu sana.Mi nimewahi ku mmega mchumba wa mtu one week kabla ya harusi.Alikuwa ameninyima mda mrefu sana ila wakati anajiandaa na sendoff akaamua kunimegea na mfululizo nilimmega kwa wiki tatu.Na hata baada ya sendoff kesho yake alimuacha mchumba wake njiani akimsindikiza na kunitaka tuonane.Haya mambo ya malove magumu sana jamani.
 
Pole sana,mwambie utalea mtoto ila baada DNA kusema mtoto ni wako,kaka ukweli ni kwamba huyo hakufai.
 
Aliyetubu na kukueleza kila kitu .......huyo anakufaa kwa sababu hawezi kurudia bali yule anayekuficha huyo ni balaa kwa sababu hana mpango wa kuacha dhuluma dhidi yako.........................
 
Pole sana,mwambie utalea mtoto ila baada DNA kusema mtoto ni wako,kaka ukweli ni kwamba huyo hakufai.

Mbona macho yanaweza kufanya uchunguzi wa awali kabla hujafika huko angalia usije kutumia pesa yako kwenye DNA fanya ya macho kwanza kabla hujafika mbali na usiwe na haraka na mtoto kama wako wako tu na mwache afike umri fulani ndiyo uchukue hatua hiyo baada ya kuona hafanani na wewe na kwa taarifa yako wanawake ni watu wajanja sana wanajua madhaifu yetu yote na wanajua namna ya kuyatumia pale wanapotaka kufanya hivyo kama vile kusingizia mimba au kuumwa presha sukari na nk. Ili tu mrudiane huyo kicheche hakufai mtu wangu angaza mbele utampata wako inagawa najua umemzoea na likuwa tatizo kumtoa akili mmwage hakufai na kama vipi amplekee yule aliyekuwa naye siku hiyo kama anampenda atampokea mtoto na kama ataua wa kwako akikua atamtafuta baake tumechoka na makahaba wanaojivika mavazi ya kondoo . Wameshanitesa sana na kuniharibia maisha na ilhali huko chuoni wanagawa mpaka kwa walinzi
 
pole sana ndugu yangu kwa mkasa huu mzito wa kimapenzi uliokukuta
kuna msemo ktk dini kuwa mke mwema anapangwa na Mungu, na katika ili Mungu amekuonyesha kuwa huyo sio mke mwema ili ubatilishe mipango ya ndoa kabla haujatamka kiapo kanisani au msikitini au serikalini
Nakushauri umwache huyo dada kwani umefunuliwa maono mapema sana, kitu kingine ni kuwa anatembea na mtu anayefanya nae kazi na nina uhakika mpaka sasa hivi wako nae ofisini wanachati tu thru mails huku wewe unaangaika huku jamii forum. Kwa taarifa yako kama huyo dada bado yuko hapo kazini ataendelea tu kumegwa mpaka atakapostaafu

Nakushauri kuwa piga moyo konde waeleze ndugu zako wa karibu kuwa umeamua kuachana na huyo mpenzi wako na uwaeleze sababu bila kuficha na pia simama kwenye msimamo wako wa kuachana nae na usirudi nyuma tena

Kuhusu hiyo mimba, achana nae kabisa na akikueleza hiyo habari mweleze wazi kuwa utahudumia hiyo mimba mpaka mtoto atakapozaliwa na kupimwa DNA ili kama ikijulikana kuwa ni wako umtunze na sio yeye tena

Anatumia mimba kama kigezo cha kurudiana na wewe na jiulize kwa nn akukwambia kuwa ana mimba yako kabla hujamfumania na hicho kidume. Please achana nae huyo binti nakuombe tuwasiliana zaidi nikushauri (funzadume@yahoo.com) hapo unatakiwa kupata ushauri wa kisaikolojia na pia acha kabisa kuongea nae au kumpa nafasi ya kusumbua akili yako tena kama ni mtoto mwambie asubiri akizaliwa mkapime na akae mbali na wewe kwa muda huu maana ukizidi kumkaribisha akuvuruge ubongo unaweza kumrudia na kujuta maisha yako yote

Mwisho: Kapime kama huko salama songa mbele na maisha yako, na kama ukikutwa nao fuata masharti ya ugonjwa utaishi vizuri tu. Pole sana
 
Duh! Mshikaji kwa hasira niliyonayo na uzoefu wa maisha yangu binafsi nakushauri yafuatayo. Wewe subiri mtoto azaliwe kwa vile kama ni mtoto hana kosa, kwani huenda pia huyo mtoto sio wako, ila kwa bahati akiwa wako wewe inabidi ujipange kulea. Ila msichana mwenyewe...don't don't dare to let her again in your life.

Hakufai hata kidogo..achana nae..nasema haya nikiwa na uzoefu mkubwa....! Pole kwa hayo! Utajuta maishani ukimchukua huyo msichana.
 
Ndugu yangu,

Nakuita ndugu yangu kwa kuwa u mwanaume mwenzangu. Kwanza pole sana kwa mkasa uliokupata. Najua umeumizwa sana rohoni mwako, lakini kaza moyo, tulia kwanza utafakari. Hata mimi yalinikuta kama yako... lakini BAADA ya kuoa. Sikurudi nyuma... nilisonga mbele, na sijutii. Ukiwa na msimamo, ushikilie.

1. Suala la mimba ni tata. Je, umehakiki kweli kwamba anayo? Mwambie twende kwa daktari, akupime, na huyo daktari awe wako wewe, sio wake, kwani anaweza kuwa amepanga mpango matokeo yawe kwamba ana mimba.

2. Kama ana mimba, mwambie huna imani kwa kuwa alikucheza shere, kwa hiyo mwambie hutatoa matunzo mpaka ithibitishwe kwa njia ya DNA, kwamba mtoto ni wako. Amechezea shilingi ******, sasa apate adabu kidogo. Atalea mimba peke yake.

3. Suala la kurudiana hapo halipo. Umetangaza nia ya kuoa, yeye anakutenda? Kama kweli alikuwa na mapenzi ya dhati kwako, hata angetongozwa namna gani, ASINGEKUBALI! Mwanamke namsifia kwa msimamo wake, AKIPENDA. Akipenda amependa kweli, anaweza hata kufa kwa ajili ya ampendaye. HUYO HAKUKUPENDA! Short and clear!

Sina ushauri zaidi ya haya, ila nakutakia kila la kheri. Utampata wa kwako, aliyetulia, na nakuombea kwa Mola akupe faraja, upate kupona jeraha hilo kubwa ulilolipata.

-> Mwana wa Haki

P.S. Kuvishwa pete ya uchumba ni jambo ambalo wanawake wengi waliofikisha umri wa kuolewa wanalililia. Ni bahati kubwa kwao. Nadhani hapa wote mnanielewa. Huyu kavikwa pete, tena kwa shangwe zote, lakini anafanya mambo ya kihuni! Kaitia aibu familia yake! Nadhani huko kwao watakapojua kilichotokea, anaweza hata kutengwa kwa kuwaaibisha! Jamani, muwe na busara wanawake!
 
Nadhani umepata ushauri wa kutosha. Sasa hapa ni mbayuwayu principle tu itumike "ushauri uliopata changanya na yakwako then fanya maamuzi". All the best!
 
Daa! Mshauri akimaliza chuo, Agombee Ubunge viti maalumu. Maana! Mhhh heri ya kwako, wanaoumizwa wengi wapo kwenye ndoa kabisa. Mwanamke ni pambo na wadhaifu kweli kweli. Ukimegewa na wewe tafuta mnyonge ummegee hata ambaye utakuja kumuoa, lazima watu watammega tu. Msumari kwa msumari tu. Nimesha choka mimi
 
Nakushauri mtume Mohammed Al-baradey akamchunguze kama ana Weapon of Mass Destruction (WMD)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom