Baada ya Chid Benzi, Ray C naye apelekwa sober house Bagamoyo

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
xRay-C.jpg.pagespeed.ic.L4MhKuJ2An.jpg

Muimbaji mkongwe wa muziki nchini, Rehema Chalamila ‘Ray C’ Ijumaa hii amepelekwa Life and Hope & Rehabilitation Centre (Sober House) iliyopo Bagamoyo kwa ajili ya kusaidiwa kuachana na matumizi ya Madawa ya kulevya, uongozi wa sober hiyo umethibitisha.

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku moja toka aonekane katika video iliyosambaa katika mtandao kionyesha jinsi anavyosaidiwa na jeshi la polisi baada ya kudaiwa kutaka kijichoma kisu.

Mmoja kati ya wasimamizi wa kituo cha Life and Hope & Rehabilitation Centre (Sober House) ambacho pia kilimsaidia Chidi Benz kuachana na matuzi ya Madawa ya kulevya, Karim Banji, ameiambia Bongo5 kuwa ni siku moja toka Ray C apelekwe katika kituo hicho.

“Kweli jana tumempokea Ray C, na kusema kweli kwa sasa siwezi zungumzia maendeleo yake kwa sababu ni siku ya kwanza, lakini leo mchana amekula vizuri na nimemuacha amepumzika,” alisema Karim.

Pia alisema bado hajajua Ray C atakaa kwa muda gani ndani ya sober house.

“Kusema kweli mgonjwa akiletwa hapa, atapimwa afya na baada ya hapo anawekwa katika chumba maalum kwa siku tatu ili aweze kukabiliana na hali ngumu, na baada ya hapo ataendelea na matibabu ya kawaida, kwa hiyo kikubwa ni kuombea tu,” alisema Karim.
 
Alipelekwa sober house sijui wapi, akapona akarudi uraiani.

Akapewa kazi ya kutangaza pale mawingu.

Sasa hivi ameamua kurejea tena kwenye maisha aliyoyazoea.

Kila mtu atawajibika kwa maamuzi anayoyafanya.

Wamuache.
 
Nanukuu, atapimwa afya kisha atawekwa kwenye chumba maalumu kwa siku tatu ili kuweza kukabiliana na hali ngumu ...Daah inabidi asaidiwe tu kuishinda hiyo tabia.
 
Ningekuwa na access na huyu binti au wazazi wake ningemshauri wampelke kwenye maombi na cancelling hii itasaidia sana wengi ni maroho yanawasumbua ambayo yanamwingia kutokana na maisha wanayoishi.Maombi ni muhimu pia
 
Viongozi wa hii Sober House ya Bagamoyo nao wambea wambea, sijui wanalipwa bei gani na Shigongo kutoa maelezo yote hayo? Mara Chidi Benz katoroka, Mara Babu Tale kamtelekeza Chidi, Mara sijui Ray C atawekwa chumba maalum, sijui na wao wanatafuta kiki!
 
Ningekuwa na access na huyu binti au wazazi wake ningemshauri wampelke kwenye maombi na cancelling hii itasaidia sana wengi ni maroho yanawasumbua ambayo yanamwingia kutokana na maisha wanayoishi.Maombi ni muhimu pia
Ulimaanisha 'Counselling' na sio 'cancelling'
 
Yes nilimaniisha counselling,asante kunisahihisha.si unajua simu za mchina zinakupa neno mbadala usipoangalia linasoma
 
Seriously, she needs some prayers.... Only God can deliver her soul from addiction of drugs
 
Kama ameenda kwa kulazimishwa ni sawa na kujaza maji kwenye gunia.
Mkuu upo sahihi, ki ukweli matibabu ya kwanza kwenye kuacha kitu chochote iwe Sigara,Pombe,Umalaya au wizi ni dhamira ya anayetaka kuacha sio watu wanaotaka uache. Hili ndio tatizo je,yeye mwenyewe yuko tayari kuacha ?????
 
Hivi huwa wanaanzaje kuamua kuacha kama muda mwingi wako bwii...huwa najiuliza. Labda kama ni wale ambao hawajaathirika sana wanaweza kukata shauri mapema, hawa walioharibikiwa sawa sio inabidi wakatishwe tu shauri?
 
Kuacha mapoda ni mtihani mgumu mno,tuwape hongera wanaoacha kiukweli sio sawa na kuacha bangi, sigara au pombe,lakini ndio hakuna option nyingine zaidi ya kuacha ili na wewe uwe mtu ktk jamii.
 
Back
Top Bottom